Tafuta

Vatican News
Historia njema ina uwezo wa kwenda nje ya mipaka katika nafasi na katika wakati,Papa anasema katika Ujumbe wa 54 wa Upashanaji habari 2020 anatoa wito wa kutengeneza historia ya kujenga badala ya kuharibu Historia njema ina uwezo wa kwenda nje ya mipaka katika nafasi na katika wakati,Papa anasema katika Ujumbe wa 54 wa Upashanaji habari 2020 anatoa wito wa kutengeneza historia ya kujenga badala ya kuharibu  (AFP or licensors)

Ujumbe wa Papa Francisko wa Siku ya 54 ya Upashanaji Habari Duniani 2020

Siku ya 54 ya Upashanaji Habari Duniani 2020 inaongozwa na kauli mbiu:"ili uweze kusimulia na kufanya kumbukumbu:Maisha ni historia”.Kwa kujikita ndani ya historia tunaweza kupata sababu ya ujasiri wa kukabiliana na changamoto za maisha.Tangu mwanzo historia yetu inatishiwa kwani katika historia ubaya unapitia.Papa Francisko katika Ujumbe huo anafafanua juu ya thamani ya kusimulia historia yenye kujenga na siyo kuharibu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko katika Ujumbe wake wa Siku ya 54 ya Upashanaji habari duniani 2020 ambao unaongozwa na kauli mbiu “Ili ninyi mpate kusimulia watoto wenu na wajukuu wenu:maisha ni historia” iliyotolewa katika kitabu cha Kutoka 10,2, Papa anasisitizia umuhimu wa thamani ya mwanadamu katika kusimulia historia tangu mwanzo hadi mwisho wa maisha yake. Anaanza akisema kuwa ujumbe wa mwaka huu ni mada ya kusimulia kwa sababu anaamini kuwa ili tusiweze kupotea, tunahitaji kupumua ukweli wa historia nzuri; historia zinazojenga, na sio za kuharibu, historia zinazosaidia kuota mizizi na nguvu ya kwenda mbele kwa pamoja. Katika mkanganyo wa sauti nyingi na ujumbe unaotuzunguka, kuna haja yasimulizi ya kibinadamu ambayo itambue kutazama dunia na matukio yake kwa mtazamo wa ukarimu; na ambayo isimulie sehemu yetu katika viumbe vyote vilivyo hai; historia ambayo inaonesha msukano kama nyuzi zinazounganisha mmoja na mwingine.

Kutengeneza historia nyingi

Papa Francisko anaandika kuwa, kwa asili mwanadamu ni wa kusimulia. Tangu tukiwa wadogo tunakuwa  na njaa ya historia kama ilivyo njaa ya chakula. Historia  iwe ya thamliya, ya riwaya, ya filamu, ya nyimbo, ya habari…; Na historia zinaainisha maisha yetu hata kama sisi hatutambui. Mara nyingi tunachagua ni jambo gani lenye haki  au makosa kulingana na wahusika na historia ambazo tumechagua. Hadithi zinatufundisha, zinatuunda kukubali kwetu na mwenendo, tunaweza kutusaidia kujua na kusema jinsi tulivyo. Mwanadamu sio pekee anaye hitaji nguo za kujifunika utupu wake (Mw 3,21), lakini pia ni wa pekee anayehitaji kujielezea, kujivika tena historia ili kuhifadhi maisha yake binafsi. Hatutengenezi nguo tu, lakini hata hadithi. Kwa hakika uwezo wa kibinadamu wa kusuka unapelekea kutengenezwa kwa  vitambaa hata katika maandishi. Historia za kila wakati zina watengenezaji wake wa pamoja katika muundo wa wenye ushujaa hata kila siku, na  ambao ili kufuata ndoto zao, lazima kukabiliana na hali ngumu, kupambana na ubaya huku wakisukumwa na nguvu zinazowafanya wawe jasiri kwa njia ya upendo.  Kwa kujikita ndani ya historia, Papa Francisko amesema, tunaweza kupata sababu ya ujasiri wa kukabiliana na changamoto ya maisha. Mwanadamu ni kiumbe cha hadithi kwa sababu yeye ni kiumbe wa kutengenezwa, na ambaye anajigundua na kujitajirisha katika mshindio wa siku zake. Tangu mwanzo historia, yetu inatishiwa kwa sababu katika historia ubaya unapitia

Siyo historia zote ni nzuri

Papa Francisko katika kipengele cha pili anafafanua kuhusu historia akigusia kitabu cha Mwanzo. “Ikiwa ukila, utakuwa kama Mungu” (Mw 3,4). Majaribu ya nyoka yanaingia ndani ya mshindio wa historia na ambalo ni fundo gumu la kufungua. “Ikiwa wewe utapata, utageuka, utafikia”  ndizo sauti ambazo zinavuma hata leo hii kwa kile kitwacho storytelling,  kwa malengo binafsi ya kutumia, amebainisha Papa Francisko. Ni historia ngapi tunajuzwa na kutuaminisha kuwa ili uweze kuwa na furaha unahitaji kuwa navyo, kumiliki, na kutumia! Na karibu hatutambui jinsi gani tulivyo na tamaa ya kuwa na mazungumzo mengi na masengenyo. Je ni virugu ngapi na ulaghai wa kutaka kutumia hivyo. Mara nyingi wafanyakzai wa mawasiliano, badala ya kutengeneza simulizi za kujenga, na ambazo zinaunganisha pamoja kijamii na zile za kiungo cha utamaduni wanazalisha simulizi za kuharibu na kuchochea na hizo haziunganishi,bali zinakata nyuzi za kuweza kuishi kwa pamoja. Anatoa mifano kwamba na hii ni katika kuweka pamoja habari ambazo hazina uhakika, kurudia rudia hotuba zisizo na maana na ushawishi wa kugushi, huku wakizidi kuchochea na matangazo ya chuki, hawa kwa hakika hawasuki historia ya kibadamua, bali wanavua hadhi ya mtu. Lakini historia zinazotumiwa kwa lengo binafsi na zenye madaraka maisha yake ni mafupi. Historia njema ina uwezo wa kwenda nje ya mipaka katika nafasi na katika wakati. Licha ya umbali wa sasa lakini, maisha bado yanamwilishwa.

Katika nyakati ambazo tendo la kugushi kwa habari  kunaendelea kujitokeza zaidi hadi kufikia nguzo ya kina  (il deepfake),  Papa FRancisko anasema, kuna haja ya kuwa na hekima ili kupokea na kuunda historia nzuri, za kweli na njema. Kuna haja ya kuwa na ujasiri wa kusukuma zile za uongo na mbaya sana. Kuna haja ya kuwa na uvumilivu na kufanya mang’amuzi ili kugundua historia ambazo zinasaidia kutopoteza ule uzi kati ya zile zinazochanika leo hii; historia ambayo inaweza kuleta mwanga wa kweli kwa kile ambacho kinaonesha sisi ni nani na mashujaa wanaodharauliwa kila siku.

Historia ndani ya historia nyingi

Andiko takatifu ni Historia kati ya  historia nyingi. Je ni matukio mangapi, na watu ambayo yanatuwakilisha! Hii inajionesha wazi kuwa tangu mwanzo Mungu ni muumbaji na wakati huo huo ni msimuliaji. Yeye kwa hakika alitangaza Neno lake na mambo yote  yaliyomo  (Mwa 1). Kwa njia ya kusimulia Mungu analiweka vitu  vyote katika maisha na hatimaye akaumba mtu na mwisho mwanake kama watu wake wa karibu na wa walio huru, wa kutunga  historia pamoja na Yeye. Katika Zaburi , mwandamu anasimulia juu ya Muumbaji na kusema :“Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu. Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana, (…)15 Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi;(Zab 139,13-15). Papa Francisko anaandika kuwa: Maisha tuliyopewa kama zawadi ni mwaliko wa kuendelea kusuka yale maajabu ya jinsi gani sisi tulivyo. Kwa maana hiyo Biblia ni historia kubwa ya upendo kati ya Mungu na binadamu. Katika kiini chake kuna Yesu. Historia yake inapelekea ule  utimilifu wa upendo wa Mungu kwa binadamu na wakati huo huo ni historia ya binadamu kwa ajili ya Mungu.

Kizazi hadi kizazi kutakuwa na simulizi

Mtu atakuwa hivyo, kizazi hadi kizazi katika kusimulia na kufanya kumbu kumbu kwa matukio muhimu ya Historia katikati ya  historia nyingi, zenye uwezo wa kuwasilisha maana ya kila ambacho kilitokia. Papa Francisko anabainisha kuwa ujumbe huu umetolewa katika kitabu cha Kutoka ambacho simulizi ya Biblia msingi inayotazama Mungu akiingilia kati katika historia ya watu wake. Kwa hakika wana wa Israeli waliokuwa ni watumwa walimlilia Yeye, na Mungu akasikiliza na kuwakumbuka. Mungu anakumbuka ahadi zake na Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Mungu alitazama hali ya Waisraeli, na kuwakumbukumbuka  (Kut 2,24-25).  Kutoka katika kumbu kumbu ya Mungu inatokea uhuru dhidi ya kukandamizwa na uhuru unakuja kwa njia ya ishara na miujiza. Na ndiyo kiini ambacho Bwana anamkabidhi Musa maana ya ishara hizo kwamba ili waweze kusimulia na kufanya kumbukumbu : nawe upate kusema masikioni mwa mwanao, na masikioni mwa mjukuu wako, ni mambo gani niliyotenda juu ya Misri, na ishara zangu nilizozifanya kati yao; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana! (Kut 10,2). 

Uzoefu wa Kutoka unatufudisha kuwa utazambuzi wa Mungu unajifafanua hasa kwa kusimulia kuanzia kizazi hadi kizazi kama Yeye anavyo endelea kuwapo. Mungu wa maisha anajifafua kwa njia ya maisha. Yesu mwenyewe alikuwa anazungumza juu ya Mungu, si kwa hotuba zisizo na mshiko, bali kwa kutumia mifano na hadithi ambazo zilitolewa na kugusa maisha ya kila siku. Maisha hapa ndiyo yanafanywa  na historia na baadaye katika kusikiliza, historia inakuwa maisha! Simulizi ile inaingia katika maisha ya yule anaye sikiliza na kumbadili. Hata Injili si kwa bahati mbaya ni kama simulizi. Wakati inatufahamisha kuhusu Yesu, inatuunda pia  kwa Yesu na kutufananisha Naye. Injili inataka wasomaji wawez kushiriki imani ile ile ili kushirikishana maisha hayo hayo. Injili ya Yohane inatueleza kuwa msimuliaji wa dhati ni Neno na  ambaye alijifanya kuwa msimuliaji, yaani “Mwana  wa pekee  mzao wake wa kwanza na ambaye ndiye Mungu aliye katika kifua cha Baba, ndiye yeye aliyesimulia (Yh1,18). Papa Francisko anasema kwamba, ametumia neno “kusimulia” kwa sababu asili yake ni exeghésato ambayo inaweza kutafsiriwa kama “tokeo” au “kusimulia”. Mungu yeye binafsi anajikita ndani ya ubinadamu wetu kwa kutupatia namna hii mpya ya kusukwa katika historia zetu.

Hakuna historia yoyote isiyo na maana machoni pa Mungu

Papa Francisko anasema kuwa kwa njia ya Roho Mtakatifu anaifikisha historia hata ile iliyosahulika  na ambayo iinaweza kuzaliwa kazi nzuri na kuwa kiini cha Injili. Kwa hili anataja baadhi ya historia ambazo zimekuwapo kwa njia ya  kukutana kwa dhati na uhuru wa Mungu na ule wa mwanadamu, kwa mfano kuanzia maungamo ya ‘Mtakatifu Agostino’ hadi wa ‘Ndugu Karamazov’.  Anawaalika wote kusoma historia za watakatifu na kushirikishana zile historia zenye manukato ya Injili na ambazo kila mmoja anazitambua. Kusimulia historia zetu Mungu, siyo kwa bure kwa sababu hakuna aanayepotea katika uwanja huu wa dunia na historia ya kila mmoja imefunguliwa wazi na yenye uwezo wa kubadilika anasema Papa. Kwa njia hiyo anabainisha kwamba hata tunaposimulia mabaya, tunaweza kukutana na wema na kumpatia nafasi. Ujumbe wa Papa unahitimishwa kwa Sala ya Bikira Maria ili aweze kusikiliza historia zetu na kuzilinda Akiangaziwa na sura ya Bikira Maria anayefungua mafundo akiwa na maana ya maisha yetu yaliyo jaa mafundo na ili atusaidie kujenga historia ya amani na ya wakati endelevu.

24 January 2020, 11:04