Tafuta

Vatican News
Nchini Brazil wanafanya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu Bwawa la madini ya  chuma kuporomoka na kusasabisha vifo vya watu 272 Nchini Brazil wanafanya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu Bwawa la madini ya chuma kuporomoka na kusasabisha vifo vya watu 272  (AFP or licensors)

Ujumbe wa Papa Francisko kuhusu Janga la Brumadinho,Brazili!

Papa Francisko katika ujumbe wake kwa njia ya video anakumbuka majanga ya asili yaliyotokea mwaka mmoja uliopita huko Brumadinho,Kusini Mashariki mwa Brazili na kuonesha ukaribu wake kwa familia na waathirika wote ikiwa pamoja na jumuiya nzima na Kanisa lote mahalia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mara baada ya mwaka mmoja tangu janga la mazingira huko Brumadinho, nchini Brazil Papa Francisko amependa kuwafikishia waathirika na Jumuiya nzima mshikamano na msaada wake.Katika ujumbe wake wa mshikamano ni matarajio ya Papa Francisko kwamba inawezekana kuwa na matendo ya dhati ya kukarabati na kuwa na ulinzi wa nyumba yetu ya pamoja.

Matarajio ya Papa ya kukarabati bonde hilo

Katika Ujumbe kwa njia ya Video Maneno yake Papa anasema:  “Katika mwaka wa kwanza wa kukumbuka janga la  Brumadinho, ninasali kwa ajili ya kaka na dada 272 waliobaki wamefunikwa hapo”.  “Na tunajuta sana kwa ajili ya kuharibiwa kwa wa bonde lote hilo  la mto. Tunatoa mshikamano wetu kwa familia za wahasiriwa, msaada kwa  Jimbo Kuu na kwa watu wote wanaoteseka na wanaohitaji msaada wetu. Kupitia maombezi wa Mtakatifu Paulo,Mungu anaweza kutusaidia kukarabati na kulinda nyumba yetu ya pamoja”.

Janga lilitokea tarehe 25 Januari 2019

Janga hili baya la mazingira lilitokea alasiri ya tarehe 25 Januari 2019 kufuatia kuanguka kwa bwana la bonde la uchimbaji wa madini ya chuma katika kijiji cha Córrego do Feijão, huko Brumadinho, mji wa Minas Gerais wa serikali ya  Brazili. Kuanguka kwa bwawa hilo lenye mita za ujazo wa  milioni 13  madini na kati yake  madini yenye sumu kama vile zebaki, kulisababisha vifo cha watu 272 na kati ya wafanyakazi wa mgodi huo, pia watu wa kujitolea na unaomilikiwa na kampuni ya Vale, na familia zao. Mtiririko wa matope na uchafu pia vilimwagika juu ya mkondo wa maji ambayo yanapita katika eneo hilo na kusababisha janga kubwa la mazingira.

25 January 2020, 13:56