Ikiwa ni sherehe za Tokeo la Bwana Papa Francisko wakati wa mahubiri yake katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro amejikita kufafanua maana ya kuabudu kama walivyofanya Mamajusi Ikiwa ni sherehe za Tokeo la Bwana Papa Francisko wakati wa mahubiri yake katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro amejikita kufafanua maana ya kuabudu kama walivyofanya Mamajusi 

Tokeo la Bwana:tupige magoti mbele ya Yesu ili tushinde utumwa

Kuabudu ni kuchota wema katika kisima,ni kupata kutoka kwa Mungu ujasiri wa kukaribia wengine.Kuabudu ni kujua kuwa kimya mbele ya Neno la Mungu ili kuweza kujifunza kusema neno ambalo haliumizi bali linatoa faraja.Kuabudu ni ishara ya upendo ambao unabadili maisha.Ni katika mahubiri ya Papa Francisko katika Kanisa la Mtakatifu Petro wakati wa kuadhimisha Tokeo la Bwana tarehe 6 Januari 2020.

Na Sr.Angela rwezaula – Vatican

Tarehe 6 Januari 2020, Mama Kanisa akiwa anaadhimisha sherehe la  Tokeo la Bwana(Epifania), Papa Francisko ameongoza misa Takatifu k   atika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, kwa waamini na mahujaji waliofika kutoka pembe zote za dunia. Akianza mahubiri yake amesema: “Katika Injili ya (Mt 2,1-12) Mamajusi wanaanza kusimulia kwa kuonesha nia zao ya kuwa:“tuliona nyota zikichomoza na tumekuja kuabaudu”. Kuabudu ndiyo upeo na hatima ya mchakato wa safari yao. Na hiyo kwa dhati baada ya kufikia Betlehemu “waliona mtoto na Maria mama yake, wakamsujudia na kuabudu”. Iwapo tunapoteza maana ya kuabudu, tunapoteza maana ya mchakato wa hatua za maisha ya kikristo ambayo ni safari kuelekea kwa Bwana na siyo kuelekea kwetu. Ni hatari ambayo tunaonywa na Injili ambayo karibu na Mamajusi inawawakilisha hata watu wasioweza kuabudu.

Herode anatumia neno kuabudu kwa sababu ya hila

Awali ya yote  Papa anaongeza kusema, yupo Herode ambaye anatumia neno kuabudu, lakini kwa namna yake ya hila. Yeye anawaomba mamajusi wamweleze mahali ambapo anapatikana Mtoto huyo kwa sababu anasema kuwa “na mimi niende kumwambudu”. Kiukweli Herode alikuwa anajiabudu mwenyewe na kwa namna hiyo alikuwa anataka kumwondolea mbali Mtoto huyo kwa ulaghai. Je kwa hilo tunafundishwa nini? Papa amejibu kuwa: Tunafundishwa kwamba mtu anaposhindwa kuabudu Mungu,anaanza kujiabude yeye mwenyewe yaanu (umimi). Na hata katika maisha ya kikristo bila kuabudu Bwana, yanaweza kugeuka kuwa ya mtindo wa kuelimika kwa kujiona binafsi na akili. Lakini n wakristo ambao hawajuhi kuabudu na ambao hawajui kusali wakiwa wanaabudu. Hata Hivyo Papa Francisko amesema kwamba: “Ni hatari kubwa kutumia Mungu kwa ajili yetu binafsi, badala ya kumtumikia Mungu” Je ni mara ngapi tumebadilishana masilahi ya Injili na yale yetu, je ni mara ngapi tumelimbikiza kile kizuri cha kidini ambacho tunaona kinafaa kwetu, ni mara ngapi tumechanganya nguvu kwa mujibu wa neno la   Mungu, ambalo ni kutumikia wengine na lile la nguvu kwa mujibu wa ulimwengu, ambalo linajikita juu ya  kujihudumia?

Herode anafanana kama wengine wasio jua kuabudu

Zaidi ya Erode ni kama watu wengine katika Injili ambao hawajuhi kuabudu. Hawa ni wakuu wa mahukani na waandishi wa watu. Hawa waliweza kumwelekeza kwa dhati Herode  ni  mahali gani ambapo alikuwa azaliwe Masiha yaani: “ Betlehemu ya Yuda”. Walikuwa wanatambua unabii na wanapataja kabisa. Hawa walikuwa wanajua ni mahali wapi pa kwenda, lakini hawakwenda.  Kutokana na hiyo Papa amesema, hata katika hili tunaweza kupata mafundisho. Katika maisha ya kikristo, haitoshi kujua, bila kutoka ndani yetu binafsi, bila kukutana, bila kuabudu huwezi kujua Mungu. Taalimungu na utendaji wa kichungaji, vinasaidia kidogo au hapana  iwapo hatuinami na kupiga magoti; iwapo hatufanyi kama Mamajusi, ambao hawakuwa wenye hekima ya kuandaa safari tu, lakini pia waliweza kutembea na kuabudu.  Inapokuwapo ile tabia ya kuabudu ndipo kuna utambuzi ya kwamba imani haishii kuwa juu ya upamoja wa mafundisho mazuri tu,  lakini pia ni kuwa na uhusiano na Mtu aliye hai wa kupenda. Ni kubaki  mbele ya uso kwa uso na Yesu ambaye tunamjua uso wake. Ni katika kuabudu ili kukugundua kuwa maisha ya kikristo ni historia ya upendo na Mungu, mahali ambapo haitoshi kuwa na mawazo mazuri, bali inahitaji kumweka Yeye katika nafasi ya kwanza  kama vile mtu amfanyiavyo yule ampendaye. Na vivyo hivyo Kanisa linapaswa kuwa mwabudu mpenda Yesu mchumba wake!

Mwanzoni mwa mwaka tugundue kwa upya kuabudu kama hitaji la imani

Katika mwanzo wa mwaka  Papa Francisko anashauri tugundue kwa upya kuabudu kama hitaji la imani. Iwapo tutatambua kupiga magoti mbele ya Yesu, tutashinda vishawishi vya kuendelea kwa kasi mbele kila mmoja katika njia yake. Kubudu kwa hakika ni kutimiza ile safari ya kutoka kwenye utumwwa mkubwa sana, ule wa ubinafsi . Kuabudu ni kimweka Yesu katikati ili tusiweze tena kujihesabu sisi binafsi tu. Kuabudu ni kutoa radha katika mpangilio wa mambo na kuacha Mungu katika nafasi ya kwanza. Kuabudu ni kuweka mipango ya Mungu  iwe ya kwanza kabla ya muda wangu, haki zangu na nafasi zangu. Ni kupokea mafundisho ya Maandiko Matakatifu yasemayo:“ Bwana Mungu wako na utamwambudu (Mt 4,10), ni  Mungu wako utamwadu kwa maana, kuabudu ni kuhisi kushiriki pamoja na Mungu. Na kumpatia jina la wewe ndani ya kina cha moyo ni kumpelekea maisha kwa kuruhusu yeye aingie katika maisha yetu. Ni kumfanya ashushe faraja zake katika ulimwengu. Kuabudu ni kugundua kuwa ili kusali inatosha kusema tu: “Bwana wangu na Mungu wangu”(Yh 20,28)na kuacha kukumbatiwa na huruma yake.

Kuabudu ni kukutana na Yesu bila orodha ya maombi

Papa Francisko akiendeleza maana ya kubadu amengeza kusema: “Kuabudu ni kukutana na Yesu bila orodha ya maombi, bali kuwa na maombi pekee ya kukaa na Yeye”. Ni kugundua ile furaha na amani inayozidi kuongezeka kwa njia ya sifa na shukrani. Tunapoabudu tunamwezesha hata Yesu atuponeshe na kutubadili. Kwa kuabudu tunampatia Bwana ule uwezekano wa kutubadilisha kwa njia ya upendo wake, wa kutuangazia katika giza letu, wa kutupatia nguvu dhidi ya udhifu na ujasiri katika majaribu.  Kuabudu ni kwenda na kujali yaliyo ya muhimu. Ni njia ya kutoa sumu dhidi ya mambo mengi yasiyo na maana, ya kutegemea na ambayo yanafanya moyo uwe mgumu na kuweka sumu ndani ya akili. Kwa kuabudu kiukweli ni kujifunza kukataa kile ambacho hakipaswi kuabudiwa, kwa mfano fedha, miungu ya matumizi mabaya, miungu ya anasa, miungu ya mafanikio na miungu ya umimi. Kuabudu ni kujifanya wadogo mbele ya Mwenye enzi aliyejuu, ili kugundua mbele yake kwamba ukuu wa maisha hautokani na kuwa navyo bali kwa kupenda. Kuabudu ni kujigundua kama kaka na dada mbele ya fumbo la upendo ambao unashinda kila umbali. Kuabudu ni kuchota wema katika kisima, ni kumpata Mungu aliye karibu ujasiri wa kukaribia wengine.  Kuabudu ni kujua kunyamaza mbele ya Neno la Mungu ili kuweza kujifunza kusema neno ambalo haliumizi bali linatoa faraja.

Kuabudu ni ishara ya upendo ambao unabaidili maisha

Papa Francisko akiendelea na mahubiri yake amesema kuabudu ni ishara ya upendo ambao unabadili maisha. Ni kufanya kama Mamajusi, ni kupeleka kwa Bwana dhahabu ili kumwambia kuwa hakuna lolote lenye thamani zaidi yake: Kumtolea uvumba, kwa kumwambia kuwa ni Yeye maisha yetu yanayotolewa huko juu; Ni kumtolea manemane, ambayo yalikuwa yanapaka miili iliyojeruhiwa na kugagaa ili kutoa ahadi kwa Yesu ya kuweza kukimbilia jirani zetu waliobaguliwa na wenye kuteseka kwa maana Yeye yupo pale. Papa Franciso kwa kuongeza anasema, sisi kwa kawaida tunajua kusali, tunomba na kushukuru Bwana, lakini bado Kanisa linapaswa kwenda mbele zaidi ya kwa sala ya kuabudu. Tunapaswa kukua katika kuabudu, amesisitiza. Ni hekima ambayo tunahitaji kujifunza kila siku.Kusali kwa kuabudu ni sala ya kuabudu.

Je mimi ni mkristo anayeabudu

Kila mmoja wetu leo hii anaweza kujiuliza “je mimi ni mkristo anayeabudu? Wakristo wengi ambao wanasali hawajuhi kuabudu. Amebainisha Papa Francisko. Tujiulize swali hili: Je tunapata muda kwa ajili ya kuabudu katika siku zetu na tunatafuta nafasi kwa ajili ya kuabudu katika jumuiya zetu? Hili ni jukumu letu kama Kanisa kujikita katika matendo ya neno ambalo lilikuwa katika kiitikio  cha Zaburi ya Siku  “Mataifa yote ya ulimwengu, watakusujudia, Ee Bwana”. Kwa kuabudu tutagundua hata sisi kama Mamajusi maana ya safari yetu. Na kama Mamajusi tutahisi, “ furaha kubwa sana”(Mt 2,10).

PAPA-TOKEO LA BWANA
06 January 2020, 12:31