Tafuta

Katika tafakari ya Katekesi ya Papa Francisko tarehe 29 Januari 2020, ameanza hatua ya kufafanua Heri za Mlimani Mt 5,1-11. Katika tafakari ya Katekesi ya Papa Francisko tarehe 29 Januari 2020, ameanza hatua ya kufafanua Heri za Mlimani Mt 5,1-11. 

Papa:Heri ni ujumbe kwa ubinadamu wote!

Papa Francisko akifungua hatua mpya ya Katekesi zake kwa mwaka huu,amejikita na mada ya Heri.Amefafanua jinsi Yesu anavyo fundisha sheria mpya ya kuwa maskini,wapole,wenye huruma.Hatimaye Papa ametoa ushauri wa kusoma hizo Heri ili hatimaye kutambua njia hiyo nzuri sana,yenye uhakika wa furaha ambayo Bwana anapendekeza kwetu.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 29 Januari 2020 Papa Francisko amefanya tafakari yake katika Katekesi kwa waamini na mahujaji toka pande za dunia waliounganika kusikiliza kwenye ukumbi wa Paulo VI. Katika katekesi yake amenza hatua mpya ya tafakari kutoka Mwinjili Matayo. Kwa maana hiyo Papa Francisko amesema kusema: “Tunaanza leo hii mfululizo wa katekesi kuhusu Heri katika Injili ya Matayo 5,1-11). Maandiko hayo yanatufungulia Hotuba ya mlimani ambayo iliangaza maisha ya waamini  wengi hata  wengi  wasio amini. Ni vigumu kutoguswa na maneno ya Yesu, na ni haki ya kuwa na shauku ya kuyatambua, na kupokea daima kikamilifu. Ndani ya Heri hizo kuna “kadi ya utambulisho” wa mkristo na ndiyo kadi ya utambulisho wetu, kwa sababu ni maelekezo ya picha ya Yesu mwenyewe na ndiyo mtindo wake wa maisha”.

Heri ni ujumbe kwa binadamu wote

Papa Francisko katika sehemu hii amefafanua kwa ujumla maneno yake Yesu. lakini akibainisha kwamba wakati wa katekesi zijazo, tafakari zitajikita kufafanua  Heri moja moja. Awali ya yote ni muhimu kama ilivyotangza ujumbe huo, Yesu kwa kutazama umati uliokuwa unamfuata, alipanda kilima kidogo kilichokuwa kinazunguka ziwa Galilaya, alikaa na kuwahutubia  wafuasi wake akiwatangazia Heri. Hata hivyo ujumbe huo ukiwalenga wafuasi lakini  pia ni katika maono  kwa maana kuna umati, yaani ubinadamu wote. Ni ujumbe wa binadamu wote, Papa amesisitiza. Zaidi ya hayo, mlima unakumbusha mlimani Sinai, mahali ambapo Mungu alimpatia Musa Amri Kumi. Na katika mantiki hii, Yesu anaanza kuwakabidhi sheria mpya ya kuwa: maskini, wapole, wenye huruma…. Hata hivyo Papa amebainisha kwamba “Amri hizi mpya ni muhimu zaidi ya sheria”. Kwa hakika Yesu halazimishi kitu, bali anaonesha njia ya furaha ya maisha yake, kwa kurudia rudia mara nane heri, yaani ‘heri wao’, ‘heri wale’, ‘heri ninyi’…. “Ni mara nane anatamka hivyo”, Papa amebainisha.

Kila Heri imegawinyika sehemu tatu

Kila heri imegawanyika katika sehemu tatu, amesema Papa. Ya kwanza linaanza na  neno la “heri”; baadaye inafuata hali halisi ambamo wanakutwa wenye heri hao kama :maskini wa roho, wenye huzuni, njaa na kiu ya haki…; na mwisho kuna sababu ya heri hizo nayoungunaishwa na kiunganishi  maana, kusema Heri walio maana, Heri wale maana….  Na kwa maana hiyo ni Heri nane na ingekuwa vizuri zaidi kukariri na kuzirudia rudia ili kuwa kuzifahamu zaidi  katika akili na moyo, maana  hizi ni sheria za Yesu ambazo anatupatia, ameshauri Papa Francisko. “Lazima kuwa na makini kwa sababu Lengo la heri siyo hali ya sasa, hapana, walakini kwa kutazama hali ya Yesu, ni hali moja ambayo wenye heri wanapokea kama zawadi kutoka kwa Mungu, kwa maana Ufalme wa Mbingu ni wao, kwa maana watafarijika, kwa maana watairithi nchi…

Mantiki nyingine ya sababu  ya furaha

Katika mantiki nyingine ni sababu ya furaha ambayo Yesu anaitumia mara nyingi katika wakati ujao, ni ile kwamba:“watafarijika, wairithi nchi, watashibishwa, wanatasamehewa, wataitwa wana wa Mungu. Je neno Heri lina maana gani? Katika kujibu  Papa Francisko anasema kwamba: kila kila Heri nane hizo zinaanzia na neno heri. Asili ya neno hili haioneshi  kama kuna mwenye tumbo  limeshiba au kupata wema, bali ni  mtu  katika hali  ya neema, ambayo ni neema ya Mungu katika njia ya Mungu kwa uvumilivu, umaskini, katika kutoa huduma kwa wengine, katika kufariji… ni mwelekeo na mwendelezo wa njia hiyo Papa Francisko anafafanua. Kwa njia hiyo hawa wenye heri watakuwa na furaha na hawa watakuwa wenye heri!

Mungu anachagua njia zisizofikirika

Ili Mungu aweze kutoa zawadi kwetu sisi, anachagua mara nyingi njia zisizofikirika, na labda zile ambazo sisi tunaona vizingiti, kwa njia ya machozi yetu na kwa njia ya kushindwa kwetu. Ni furaha ambayo ndugu wa Mashariki wanazungumza, kwa maana ya zile zenye madonda, japokuwa ni hai. Ni  Yeye alipitia kifo na akafanya uzoefu wa nguvu ya Mungu. Heri zinatupeleka katika furaha daima. Ni njia ya kwenda katika furaha.  Kutokana na hiyo Papa anatoa ushauri kwamba itakuwa vema kutafuta Injili ya Matayo 5,1-11 na kusoma heri hizo,  labda  mara nyingi wakati wa wiki ili kuweza kutambua njia hii nzuri sana  yenye uhakika wa furaha ambayo Bwana anapendekeza kwetu! amehitimisha Papa.

29 January 2020, 13:42