Tafuta

Vatican News
Wakati wa sala ya Malaika wa Bwana tarehe 5 Januari 2020 Papa Francisko anabainisha kuwa vita inapelekea kifo kwa maana hiyo anasema inabidi kuepusha vivuli vya uadui Wakati wa sala ya Malaika wa Bwana tarehe 5 Januari 2020 Papa Francisko anabainisha kuwa vita inapelekea kifo kwa maana hiyo anasema inabidi kuepusha vivuli vya uadui  (AFP or licensors)

Papa Francisko:Vita inapelekea kifo,tuepushe vivuli vya uadui!

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana Papa Francisko ametoa ushauri wa kuepusha kivuli cha uadui,ikiwa na maana ya mivutano ambayo inaendelea katika kanda tofauti ulimwenguni.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ikiwa ni Dominika ya Pili ya kipindi cha Kuzaliwa kwa Bwana, tarehe 5 Januari 2020 mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana Papa Francisko ametoa ushauri ili kuepusha kivuli cha uadui. Katika kuanza amesema: “katika sehemu mbalimbali za dunia inasikika hali hewa ya kutisha ya mivutano. Vita vinapelekea kifo tu na uharibifu.” Kutokana na hiyo anatoa wito kwa sehemu zote ili kubaki wamewasha mwanga wa majadiliano katika kujidhibiti na kuzuia kivuli cha uadui. “Tuombe kwa kimya ili  Bwana atupe neema hii”….

Baada ya ukimya wa sala, Papa Francisko amegeukia mahujaji wote na waamini kutoka sehemu mbalimbali wakiwemo familia, vyama na makundi ya kiparokia kwa namna ya pekee vijana wa kipaimara kutoka Mozzo na Almè Jimbo katoliki la Bergamo Italia na wengine.

Katika Dominika hii ya kwanza ya mwaka, Papa amepyaisha matashi mema na utulivu wa amani ya Bwana. Papa anasema katika kipindi cha furaha na katika kipindi kigumu, tumkabidhi Yeye ambaye ni matumaini yetu!

Anakumbusha hata jitihada ambazo wamejiwekea wakati wa kuadhimisha sherehe za Mwaka Mpya katika Siku ya Amani duniani, inayoongozwa na kauli mbiu: “Amani ni safari ya matumaini, majadiliano, mapatano na uongofu wa kiekolojia. Kwa neema ya Mungu amebainisha: “tunaweza kweli kujikita katika matendo! Amewatakia Dominika njema na kuwaomba kama kawaida yake ya kusali kwa ajili yake. “Ninawatakia mlo mwema na tutaonana kesho kwa ajili ya maadhimisho ya Toleo la Bwana”

       

05 January 2020, 15:44