Papa Francisko:uwajibu wa ukarimu kwa wageni ni upendo kama wa Mungu!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Papa Francisko katika katekesi yake yak ila Jumatano kwa waamini na mahijaji wote waliungunika katika ukumbu wa Paulo VI mjini Vatican tarehe 22 Januari 2020 ameanza kusema kuwa Kateksi ya lei inajikita ndani ya Wiki ya Kuombea umoja wa Wakristo. Mada iliyo chaguliwa mwaka huu ni ile ya ukarimu na ambayo imeweza kufafanuliwa kwa mapana katika jumuiya ya Malta na Goo kuanzia katika hatua ya Matendo ya Mitume ambayo inasimulia juu ya ukarimu uliotolewa na wakazi wa Malta kwa Mtakatifu Paulo na wenzake walionusurika akiwa nao. Kwa dhati katika tukio hilo Papa Francisko amethibitisha kuwa alijikita nalo katika katekesi ya wiki mbili zilizopita.
Uzoefu wa janga la kunusurika
Papa Francisko akianza na uzoefu wa janga wa kushangaza hasa la kunusirika kwa meli waliyo safiri nayo Paulo na wenzake ilikuwa kweli hatarini. Na hii ni kwa sababu Meli waliyokuwa wanasafiiri ilikuwa na vitu vingi. Kwa siku kumi na nne walikuwa baharini, ambapo liwe jua au nyota vilikuwa havionekani, na kwa maana hiyo wasafiri walihisi mfadhaiko, na wamepotea. Chini yao, bahari inazunguka kwa vurugu dhidi ya meli na wanaogopa kwamba itavunjika kutokana na nguvu ya mawimbi. Kutoka juu wanapigwa na upepo na mvua. Nguvu ya bahari na dhoruba ina nguvu sana na haijali hatima ya mabaharia na kulikuwa na zaidi ya watu 260! Lakini Paulo anayetambua kuwa siyo hivyo anaamu kuzungumza. Imani yake inamfanya atambua kuwa maisha yake yako mikononi mwa Mungu na kwamba Yesu aliyefufuka katika wafu alimwita Yeye Paulo apeleke Injili hadi miisho ya dunia. Imani yake inamwaminisha kwa Mungu na kwa upande wa Yesu aliye mwonesha ni Baba wa upendo. Kwa maana hiyo Paulo anawambia wenzake kuwa safari hiyo ni ya imani na anawatangazia kuwa Mungu hataruhusu hata unywele mmoja vichwani mwao upotee.
Unabii wa Yesu unajionesha katika kisiwa cha Malta
Unabii huo ulijionesha tu wakati Meli iliposimama katika mwambao wa Kisiwa cha Malta na wasafiri wote waliweza kufika sala salimini katika nchi kavu. Hapo waliweza kufanya uzoefu wa jambo jipya. Tofauti na vurugu za kikatili za bahari ya dhoruba, wanapata ushuhuda wa “ubinadamu ulio adimu” wa wenyeji wa kisiwa hicho, amesisitza Papa. Watu hawa, kwa upande wao ni wageni kwao, wanazingatia na kuwa makini kwa mahitaji yao. Waliweza kuwaashia moto ili wapate jotyo, waliwapatia chakula na makazi ili kutoka kwenye mvua.
Hata kama walikuwa hawajapata Habari Njema ya Kristo, walionesha upendo wa Mungu kwa matendo ya dhati na ukarimu. Na kiukweli, ukarimu wa hiari na ishara zinaonyesha kitu cha upendo wa Mungu. Na ukarimu wa wenyeji wa kisiwa cha Malta ulilipwa na miujiza ya uponyaji ambayo Mungu analifanya kazi yake kupitia kwa Paulo kwenye kisiwa hicho. Kwa hivyo, ikiwa watu wa Malta walipewa ishara kubwa ya utoaji wa upendo mkuu kutoka kwa Mungu kupitia kwa Mtume, hata yeye pia kwao alikuwa shuhuda wa upendo wa huruma ya Mungu, Papa Francisko amesema.
Umuhimu wa fadhila za kiekuemene
Papa Francisko akiendelea kufafanua amekazia kuwa ukarimu ni muhimu na zaidi ni muhimu wa fadhila za kiekumene. Awali ya yote maana ni kutambua kuwa wakristo wengine ni ndugu wa kweli, kaka na dada katika Kristo. Sisi sote ni ndugu. Hata hivyo Papa anatoa mfano kwamba: mwingine inawezakana kusema: “ huyo ni mprotestanti, hutìyo ni muorthodox…. Haijalishi kwa maana, sisi sote ni ndugu katika Kristo”. Na siyo tendo la ukarimu wa njia moja tu, kwa sababu tunapowakaribisha Wakristo wengine tunawakaribisha kama zawadi ambayo tumepewa. Kama ilivyokuwa kwa wenyeji wa Malta, kwa hakika ni watu wema amekazia kusema Papa.., na zaidi tunalipwa, kwa sababu tunapokea kile ambacho Roho Mtakatifu amepanda katika kaka na dada zetu, na hii inakuwa zawadi hata sisi pia, kwa sababu Roho Mtakatifu pia hupanda neema zake kila mahali.
Kukaribisha watu wa tamaduni nyingi ni kuonesha upendo wa Mungu
Kukaribisha wakristo wa tamaduni nyingine maana yake ni kuonesha upendo wa Mungu alio nao kwao na hivyo kwa sababu ni wana wa Mungu na ndugu zetu na zaidi maana ni kukaribisha kile ambacho Mungu alitimiza katika maisha yao. Ukarimu wa kiekumene utahitaji utayari wa kusikiliza wakristo wengine, kuwa makini katika historia binafsi za imani yao na katika historia yao ya kijumuiya, jumuiya ya imani na utamaduni tofauti na wa kwetu. Ukarimu wa kiekumene unapelekea shauku ya kutambua uzoefu ambao wakristo wengine wanafanya kwa Mungu na kusubiri kupokea zawadi ya kiroho itokanayo na ukarimu huo. “Hii ni neema na kugundua”, anasema papa na kurudia kuwa “hiyo ni neema”. Papa Francisko amekumbuka nyakati zilizopita katika nchi yake na kutoa mfano kuwa: “walipokuwa wanakuja baadhi ya wamisionari wa kiinjili, makundi ya wakatoliki walikuwa wanakwenda kuchoma mahema yao. Hii siyo ukristo. Kwa sisi sote ndugu na kama ni ndugu tunapaswa kukarimu mmoja na mwingine”.
Leo hii mahali ambapo Paulo alipitia na kunusurika bado kuna hatari ile ile
Leo hii baharini mahali ambapo Paulo alinusurika na wenzake, bado kwa mara nyingine tena ni mahali pa hatari ya maisha ya wasafiri tena. Duniani kote wanaume na wanawake wahamiaji wanakabiliana na safari ya hatari wakikimbia vurugu, wakikimbia vita na kukimbia umasikini. Kama Paulo na wenzake wanafanya uzoefu wa sintofahamu, ugumu wa jangwa, mito na bahari… na mara nyingi hawaruhusiwi kupita bandarini, Papa Francisko ameeleza wazi. Na zaidi amezidi kusema : “Lakini kwa bahati mbaya mara nyingi wanakutana na ugumu na na uadui mbaya zaidi wa watu”. Leo hii wananyanyaswa na wafanyabiashar haramu!. Leo hii wanatendewa kama idadi na kama tishio na baadhi ya watawala wengine! Wakati mwingine wanakosa ukarimu na kuwakataa na kuwatupa kama wimbi katika umaskini au hatari ambayo wameikimbia.
Wakristo lazima tufanye kazi kwa pamoja kuonesha wahamiaji upendo wa Mungu
Sisi, kama Wakristo, lazima tufanye kazi kwa pamoja ili kuwaonyesha wahamiaji upendo wa Mungu uliofunuliwa na Yesu Kristo. Tunaweza na tunapaswa kushuhudia kwamba siyo tu kuwapo uadui na kutojali, bali kwamba kila mtu ni ni mwenye thamani kwa Mungu na anapendwa naye. Mgawanyiko ambao bado upo kati yetu unatuzuia kuwa ishara kamili ya upendo wa Mungu. Inatakiwa kufanya kazi pamoja, ili kuishi ukarimu wa kiekuemene, hasa kwa wale ambao maisha yao yako hatarini zaidi, nazidi hali hii itatufanya sisi sote kuwa Wakristo hai ikiwa ni Waprotestanti, waorthodox, Wakatoliki, yaani Wakristo wote, kuwa wanadamu bora, wanafunzi bora na watu wakristo walio na umoja wa Kikristo. Hii itatuleta pamoja karibu karibu na umoja, ambao ndiyo mapenzi ya Mungu kwetu.