Tafuta

Vatican News
Katika siku ya kwanza ya mwaka Liturujia inaadhimisha Maria Mtakatifu Mama wa Mungu, Bikira wa Nazareth ambaye amemzaa mtoto Yesu Mwokozi Katika siku ya kwanza ya mwaka Liturujia inaadhimisha Maria Mtakatifu Mama wa Mungu, Bikira wa Nazareth ambaye amemzaa mtoto Yesu Mwokozi  (AFP or licensors)

Papa:Utakuwa mwaka wa amani na matumaini tukimfungulia Yesu mioyo yetu!

Katika fursa ya Sala ya Malaika wa Bwana kwa Mwaka 2020, wakati Kanisa linaadhimisha Sikukuu ya Maria Mtakatifu Mama wa Mungu,Papa Francisko anawaalika waamini kupokea mtoto na baraka ya Mungu anayoitoa kwa Kanisa na ulimwenguni.Aidha ameomba radhi kuhusiana na ishara ya ukosefu wa uvumilivu,iliyojitokeza wakati wa kusalimia na waamini tarehe 31 Desemba 2019 jioni akiwa anatembelea Pango katika uwanja wa Mtakatifu Petro.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Jana usiku tumehitimisha mwaka 2019 huku  tukimshukuru Mungu wa ajili ya zawadi ya muda na kwa ajili ya mema yake yote. Leo hii tunaanza 2020 kwa mtindo huo huo wa shukrani na sifa. Siyo kwa bahati mbaya katika sayari inaanza na mzunguko mpya wa kuzungukia jua na ili kama sisi binadamu tuweze kuendelea kuishi ndani mwake. Siyo kwa bahati mbaya na zaidi ni miujiza ambayo ni ya kushangaza na kushukuru.  Ndiyo mwanzo wa tafakari yaPapa Francisko kabla ya sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican Mosi Januari 2020.

Papa Francisko akiendela anamesema “ Katika siku ya kwanza ya mwaka Liturujia inaadhimisha Maria Mtakatifu Mama wa Mungu, Bikira wa Nazareth ambaye amemzaa mtoto Yesu Mwokozi”. Mtoto huyo ni baraka ya Mungu na kwa kila mwanaume na mwanamke,  kwa ajili ya familia kubwa ya binadamu na kwa ajili ya ulimwengu mzima. Yesu hakuondoa ubaya dunia, lakini alishinda mzizi wake. Wokovu wake siyo wa viini macho, bali wa uvumilivu ambao unapelekea uvumilivu wa upendo; Yeye  anayebeba mabaya na kuondoa wenye nguvu.  Upendo unatufanya kuwa wavumilivu. Mara nyingi tunapoteza uvumilivu, hata na  Papa anasema na kukikita   anaomba  radhi  kwa mfano mbaya alio uonesha jana yake.( Hata hivyo tukio hili lilitokana na mtu mmoja aliye mpa salam akamkandamiza na kumuumiza mkono) Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na tafakari amesema kwa  maana hiyo katika kutafakari Pango tunaona kwa macho ya imani dunia ilivyojipyaisha, iliyo huru dhidi ya kutawaliwa na uovu na kuwekwa chini ya ufalme wa kifalme wa Kristo, Mtoto ambaye amelala ndani ya hori la ng’ombe.

Papa amesema “ Mama wa Mungu anatubariki, je anatubariki namna gani? Kwa kutuonesha Mtoto. Mtoto yuko mikononi mwaka anatubariki”. Anabariki  Kanisa lote, anabariki ulimwengu wote. Kama walivyoimba Malaika huko Betlehemu, kwamba Yesu  ni “ furaha kwa watu wote duniani” ni utukufu kwa Mungu na amani kwa watu wote ( Lk 2,14). Kwa sababu hiyo  Mtakatifu Papa Paulo VI alipendelea kwamba  siku ya kwanza ya mwaka iwe ya amani, amebainisha Papa. Ni Siku ya Amani;  kwa ajili sala, kwa ajili ya kuwa na utambuzi na kuwajibika kuhusiana na amani. Kwa mwaka huu 2020, kauli yake mbiu inasema: “amani ni mchakato wa safari ya matumanini, safari ambayo inafanyika kwa njia ya majadiliano, mapatano na uongofu wa kiekolojia.

Papa Francisko anawaalika kuwa na mtazamo juu ya Mama na Mwanaye ambaye anatuonesha. Katika mwanzo wa mwaka anashauri kuwa tuache atubariki! Yesu ndiye baraka kwa wale wanaokandamizwa na nira ya utumwa, maadili na nyenzo. Yeye anaokoa na upendo. Kwa wale ambao wamepoteza kujithamini kwao kutokana na  kufungwa na mzunguko mibaya na Yesu anasema “ Baba anakupenda, usijiachie, subiri kwa uvumilivu usioanguka kurudi kwako (Lk 15,20).

Aliye athirika na kutokana na ukosefu haki na unyonyaji na haoni njia ya kutoka, Yesu anafungua mlango wa kidugu, mahali ambapo panapatikana nyuso, mioyo na mikono mikarimu, mahali ambapo wanashirikishana upendo, uchungu na mahangaiko na kuweza kurudisha kidogo ile hadhi. Aliye mgonjwa sana na kuhisi kuachwa na kukata tamaa, Yesu anakuwa karibu, anagusa majeraha na huruma, anaweka mafuta ya faraja na kubadilisha udhaifu kuwa nguvu ya wema na kufungua vifundo vilivyo vigumu zaidi. Anaye magerazani na kushawishika kujifunga binafsi, Yesu anamfungulia upeo wa matumaini, kuanzia na mwanga mfinyo sana.

Baba Mtakatifu Francisko kwa kuhitimisha ameomba waamini waweze kujishusha dhidi ya ukiburi kwa maana wote anasema “tuna kishawishi cha kuwa na kiburi”. Na ameomba baraka kutoka kwa Mtakatifu Mama wa Mungu, mnyenyekevu Mama wa Mungu. Kwake yeye anatuonyesha Yesu, na hivyo tuache atubariki, na tufungulie mioyo ya wema wake. Kwa kufanya hivyo mwaka unaoanza utakuwa ni wa safari ya matumaini na amani, sio kwa maneno, bali kwa njia ya ishara ndogo  ndogo za kila siku katika  majadiliano, mapatano na kulinda mazingira.

01 January 2020, 13:55