Vatican News
Maisha ya binadamu,yana sababu yake ya milele,yanahifadhi thamani yake yote na hadhi yake yote, kwa hali yoyote na hata udhaifu kama vile ambao ni hadhi kubwa inayozingatiwa sana. Maisha ya binadamu,yana sababu yake ya milele,yanahifadhi thamani yake yote na hadhi yake yote, kwa hali yoyote na hata udhaifu kama vile ambao ni hadhi kubwa inayozingatiwa sana. 

Papa Francisko:ustaarabu wa jamii unajionesha katika mapambano dhidi ya ubaguzi!

Papa Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa,ambapo hotuba yake imejikita juu ya thamani msingi wa maisha ya binadamu katika kutunza wagonjwa ambao wako hatua ya mwisho wa maisha yao na ulazima kupyaishwa jitihada za nguvu ya kutunza watu wanoteseka.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 30 Januari 2020 Papa Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, ambapo amesema “tunaishi katika jamii ambayo inakosa mwelekeo wa kile kinachotoa thamani ya maisha”. Amesema hayo kwa kuangaziwa nakutokana na mada ya mkutano wao juu ya masuala ya utunzaji wa watu ambao wako katika hatua yao ya mwisho wa maisha, ambao ni katika mantiki ya sasa ya kijamii na kiutamaduni tunaouishi.

Katika mantiki hiyo ya maisha Papa Francisko anasititiza ni kwa namna gani jamii inathamanisha kwa jina kile kiitwacho“uzalishaji” na wakati huo  huo inakosa mwelekeo na uwajibikaji wa mshikamano na udugu. Na hiyo inawatazama wagonjwa ambao wako katika hatua yao ya mwisho na dharura hivyo anasisitiza Papa  kuwa ni lazima kuwa na mtazamo wa kina ndani ya moyo katika mwanga wa kuwa na huruma. Vile vile ametaja vituo vya makaribisho  kwa watu wa namna hiyo na tiba ya hadhi ambayo inatolewa. Anawashauri kuendelea kwa dhati juu ya mafunzo na tafiri za  marekebisho ya sheria ambazo zimeweka katika Waraka wa Motu proprio “Sacramentorum sanctitatis tutela” wa Mtakatifu Yohane Paulo II ili kuendelea na mchakato katika  njia hiyo ya wazi na kulinda hadhi ya walio wadhaifu.

Thamani kuu ya maisha isipungue kwa maana ya ustaarabu na mshikamano

Kwa sasa maisha yanayobaguliwa, maisha yasiyo stahili, kwa sababu hayaendeani na mantiki ya uzalishaji, katika jamii ya sasa inatumia kipimo na kupoteza  kile ambacho kina thamani ya maisha ya binadamu. Katika hali  ya kupoteza thamani hizi, pia hata uwajibika  msingi wa mshikamano na udugu wa kibinadamu na kikristo unapungua. Kwa hakika katika jamii inayostahili na staarabu, inaweza kuendelea iwapo inaweza kuzuia utamaduni wa kibaguzi; na ikiwa inatambua thamani msingi wa maisha ya binadamu; ikiwa mshikamano ni wa dhati na utekelezaji ambao unatunza msingi wa kuishi.

Mafundisho ni hali halisi inayoendelea

Papa amebainisha kuwa imani inahitaji kuwa mpokeaji wake anazingatiwa na kwamba anajulikana na kupendwa kikamilifu. Mafundisho ya Kikristo siyo mfumo mgumu na uliofungwa wenyewe, lakini pia siyo itikadi ambayo inabadilika na kupita kwa misimu; mafundisho ni ukweli wa nguvu unaoendelea ambao, unabaki kuwa mwaminifu katika msingi wake, unasasishwa kutoka kizazi hadi kizazi na muhtasari wa uso wake , katika mwili na kwa jina lake ambaye ni Yesu Kristo aliyefufuka!

Sarufi ya utunzaji ni ufunguzi wa matumaini na mafuta ya kulainisha kwa waliokata tamaa

Papa Francisko akitazama kipindi ambacho mgonjwa anakaribia kubisha  mlango wa maisha mapya ya Baba Mwenyezi, anakumbusha ni kwa jinsi gani kuna umuhimu wa kuwa na huruma, kama kiitikio kilichomo kwenye Injili na  uwepo wa mtu yoyote ambaye aweze kumpa mkono, kama Msamaria mwema, kama jukwaa la uhusiano wa kibinadamu na ambao unafungua matumaini na mafuta ya kulainisha  hisia za kukata tamaa na uchungu kiroho. Papa anahimiza kwamba “ Msiache yoyote katika kivuli cha mabaya yasiyo pona. Maisha ya binadamu, yana sababu yake ya milele, yanahifadhi thamani yake yote na hadhi yake yote, kwa hali yoyote na hata udhaifu kama ule ambao ni hadhi kubwa inayozingatiwa sana.

Tiba ya hadhi katika vituo vya kutunzia wagonjwa 

Anayetembea katika maisha ya hali hiyo hata kwa cheche ndogo ya giza la mtu siyo kuishi bure. Kwa maana hiyo hapa anatoa mfano na kumtaja Mama Teresa wa Kalcutta kwa njia ya mtindo wake wa ukaribu na ushirikishwaji ambao unasaidia kufa kwa hadi ya kibinadamu. Hili ni zoezi muhimu amesema Papa Francisko, na ambalo linatendeka katika vituo vyote vya wagonjwa kama hao. Katika mtazamo huo amekumbukwa kwa namna ya pekee  wahudumu wote hasa katika tiba shufaa, mahali ambapo wagonjwa wengi wanasindikizwa na kusaidiwa na madaktari, wanasaikolikia na watu wa kiroho ili kushi kwa hadhi, kuwatia nguvu na ukaribu wa kuendeleza hadhi kwa upendo na heshima ya maisha,

Sasisho la ‘Sacramentorum sanctitatis tutela’

Papa ameshukuru utafiti uliofanywa juu ya marekebisho ya sheria juu Motu proprio ya  “Sacramentorum sanctitatis tutela” ya Mtakatifu Yohane Paulo II . Ni jitihada ambayo iko katika mwelekeo wa kusasisha sheria ili kufanya taratibu ziwe bora zaidi, anaeleza Papa na kuongeza, kwamba kwa kuzingatia hali mpya na shida za muktadha wa sasa wa  jamii na kitamaduni. “Ninawasihi muendelee kwa nguvu katika kazi hii, kutoa mchango halali katika eneo ambalo Kanisa linashiriki moja kwa moja kuendeleza ukaribu na uwazi katika kulinda utakatifu wa sakramenti na hadhi ya binadamu iliyokiukwa, haswa watoto wadogo. Hatimaye Francisko ameipongeza Hati  iliyoandaliwa na  Tume ya Kipapa ya Biblia juu ya mada ya msingi kuhusu masomo ya  Biblia ambayo yanajikita kutazama maono ya ulimwengu wa mpango wa kimungu, na ambao ulianza na uumbaji na ambao unakamilisha kwa Kristo, binadamu mpya na kitovu cha ufunguo na mwisho wa historia yote ya wanadamu .

30 January 2020, 15:26