Tafuta

Vatican News
Kwa wajumbe wawakilishi kutoka Finland ameambia:kama wajumbe wa ubinadamu,kama wakarimu wa wema wa Mungu aliyefanyika mwili,tuko njiani pamoja katika jumuiya  ya waliobatizwa wote. Kwa wajumbe wawakilishi kutoka Finland ameambia:kama wajumbe wa ubinadamu,kama wakarimu wa wema wa Mungu aliyefanyika mwili,tuko njiani pamoja katika jumuiya ya waliobatizwa wote.   (Vatican Media)

Papa Francisko na Waluteri:atoaye kwa ukarimu ni tajiri mkuu!

Ijumaa tarehe 17 Januari 2020 Papa Francisko amekutana na uwakilishi wa kiekumene wa Kanisa la Kiluteri la Finland na kusisitizia juu ya ukarimu kwamba ni sehemu ya pamoja ya kushuhudia imani ya kikristo kwa wabatizwa wote!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Uekumene wa kiroho na mazungumzo ya kiekumene vinaanzia kujikita kwa kina katika uzoefu wa kukaa kwa pamoja. Amesisitiza hayo Papa Francisko kwa wawakilishi wa kiekumene wa Kanisa la Kiluteri kutoka Finland ambao amekutana nao mjini mjini Vatican tarehe 17 Januari 2020, wakiwa katika fursa ya hija mjini Roma katika muktadha wao wa kushehereka Mtakatifu Enrico mzimamizi wa nchi yao. Wakristo wote, amesema Papa, wanatembea katika muungano wa imani  

Jirani siyo mpinzani au adui

Papa Francisko pia amekumbusha juu ya Juampili iliyopita ambayo ilikuwa ni maadhimisho ya Sherehe za Ubatizo wa Yesu. Shukrani kwa Ubatizo huo, unatuunganisha katika Jumuiya ya wabatizwa wote. Ubatizo kwa ajili ya maondoleo ya dhambi pia ni wazi wa wito katika utakatifu. “Wapendwa marafiki wa Finland, kama wajumbe wa ubinadamu, kama wakarimu wa wema wa Mungu aliyefanyika mwili, tuko njiani pamoja katika jumuiya  ya waliobatizwa wote. Wakristo ni wale ambao wanaweza kutoa shukrani kubwa kwa ubatizo wao. Shukrani hii inatuunganisha na kupanua  mioyo yetu, inatuwafungulia kwa jirani, ambaye siyo mpinzani wetu lakini ni kaka yetu mpendwa, dada yetu mpendwa”. Amesisitiza Papa. Jumuiya  ya wote waliobatizwa sio kuwa karimu na kila mmoja  tu,  kwa hakika siyo kuwa na ugonvi dhidi ya wengine bali inataka  kugeuka daima kuwa karibu na kuwa pamoja.

Kila mmoja anatoa  bure na kupokea kwa mara nyingine

Ukarimu ni sehemu ya ushuhuda wa pamoja wa imani, anasema Papa Francisko.  Na Katika “Wiki ya Kuombea  Umoja wa Wakristo inayoanza kesho, inatuelekeza fadhila hizi za kiekumene na zaidi kwa kukumbushwa na kauli mbiu inayoongoza mwaka kuu kutoka Kitabu cha (Mdo 28, 2) ambapo Mtakatifu Paulo anaelezea wakazi wa Kisiwa Malta ambao walimpokea kwa ukarimu pamoja na mamia ya manusura”. Amebainisha Papa.

Yesu anakutana na manusura halisi katika maisha yao

Aidha amesema kuwa: “kama wakristo wabatizwa, tunaamini kuwa Yesu nataka kukutana kweli na watu ambao katika maisha yao wamekuwa manusura, kwa maana ya hali halisi. Anaye karinu si masikini, bali ni tajiri zaidi. Kwa hakika ubinadamu unajionesha kwa wengine ambao kimaajabu wanashiriki wema wa Mungu alioufanya kwa Mungu”.

17 January 2020, 13:44