Papa amekutana na wawakilishi wa Wavuvi kutoka Mtakatifu Benedikto wa Tronto nchini Italia waliosindikizwa na Askofu Askofu Carlo Bresciani na baadhi ya mpadre wanawahudumia katika safari yao ya kiroho. Papa amekutana na wawakilishi wa Wavuvi kutoka Mtakatifu Benedikto wa Tronto nchini Italia waliosindikizwa na Askofu Askofu Carlo Bresciani na baadhi ya mpadre wanawahudumia katika safari yao ya kiroho.  

Papa Francisko:lazima kuthamanisha kazi ya wavuvi na kuwalinda!

Papa Francisko amekutana mjini Vatican na uwakilishoiwa wavuvi kutoka Mtakatifu Benedkto wa Tronto nchini Italia.Amewaalika wasipoteze matumaini mbele ukosefu wa kazi na hali ngumu wanayokumbana nayo baharini.Amewapongeza kwa jitihada za kutengeneza chombo cha kuvua plastiki baharini.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko tarehe 18 Januari 2020 amekutana katika Jumba la Kitume Clementina mjini Vatican na  wawakilishi wa wavuvi karibia 60 kutoka eneo la Mtakatifu Benedikto wa Tronto, wakisindikizwa na Askofu Carlo Bresciani na baadhi ya mpadre wanawahudumia katika safari yao ya kiroho. Katika hotuba yake Papa Francisko amesema “kazi ya uvuvi mara nyingi ni  ya hatari na ngumu, ambayo inapaswa ithamanishwe na  wao kusaidiwa haki zao na kanuni  msingi ili wasipoteze matumaini mbele ya usumbufu na kutokuwa na uhakika, hadi kuwafanya  wawe na tamanio la kufanya kazi kwenye nchi kavu.

Aliyezaliwa baharini ni vigumu kuondoa mzizi wake ndani ya moyo

Papa Francisko akitazama hali yao amebainisha ni kwa jinsi gani wavuvi wanaanza mapema  kazi,  iwe katika hali nzuri ya hewa au mbaya na wanaingia baharini kwa ajili ya kutafuta namna ya kuishi, kwa upendo mkuu, sadaka nyingi na wakati huo huo hata hatari. Na ndugu wao wapendwa wanashirikishana na matatizo na hali ya maisha ambayo inahusisha kama wavuvi. Papa Francisko amesema “ ni jamii muhimu katika maisha ya kijamii ya eneo lenu, ambalo, hata hivyo, katika maendeleo yenye tabia ya jamii ya kisasa, wakati mwingine unaweza kujaribiwa kutafuta kazi salama na kuacha mashua”.Lakini wakati huo huo Papa Francisko amekumbusha, kila mtu aliyezaliwa baharini hawezi kuondoa mzizi moyoni mwake kutoka baharini. Kwa maana hiyo anawalika wasipoteze matumaini mbele ya matukio hayo na ukosefu wa uhakika ambao kwa bahati mbaya wanapaswa kukabiliana nao.  Ameongeza kusema :“ Ujasiri hauwakosi! Na  hivyo “ni lazima  kazi yenu ipate kuthamanishwa ambayo mara nyingi ni hatari na ngumu, kutetea haki zenu na matarajio halali”.

Shukrani kwa utengenezaji wa chombo cha kuvua taka  baharini

Papa Francisko akiendelea na hotuba yake ameonesha shukrani kwao  kwa shughuli ya ukarabati wa chombo cha majini cha kukusanya taka, ambacho pamoja na mashirika mengine na kwa kushirikiana na viongozi, kinaitwa “A Pesca di Plastica”, yaani kivua Plastiki, kilichotengenezwa na watu kwa kujitolea. Mpango huu ni muhimu sana, kwa kiasi kikubwa cha taka, hasa plastiki, ambazo wameweza kuziondoa  na ambapo kwa upande wake amesema: “tayari huo ni mfano unaoweza kurudiwa  na kufanywa katika maeneo mengine ya Italia na nje ya nchi”.

Wavuvi ni kazi ya zamani inayooneshwa katika Injili

Papa Francisko ambaye amesifu mpango huo wa chombo cha kukusanya plastiki,  amethibitisha kuwa,wamefikia hadi tani 24 za taka zilizokusanywa na ambazo anasema zinajieleza kama mfano wa jamii ya raia ambayo inaweza kuchangia  kukabiliana na masuala ya ulimwengu huu  bila kuchukua chochote, na zaidi  kuchochea jukumu la uwajibikaji wa taasisi zote.  Na katika kumaliza  na salamu zake,  kwa kukumbuka kuwa ya uvuni ni kazi ya zamani sana na kwamba hata kwenye Injili tunasoma matukio yanayohusiana na maisha na ulimwengu wa wavuvi. Wafuasi wa kwanza wa Yesu walikuwa ni wenzao, anasema Papa na kuongeza,” ninapendelea kufikiria kuwa hata leo hii kama wakristo muhisi uwepo wa kiroho wa Bwana karibu nanyi”. Aidha amesema  imani yao inaongoza thamani msingi na ambayo ni ya utamaduni unaojieleza katika imani kwa Mungu kwa maana ya sala na elimu ya kikristo kwa watoto; kupenda familia; maana ya mshikamano ambao wao wanahisi uhitaji wa kusaidiana na kukimbiliana katika mahitaji hayo. Amewasihi sana wasipoteza thamani hiyo.

18 January 2020, 14:48