Tafuta

Vatican News
Papa Franciski akiwa anahubiri katika  kanisa la Mtakatifu Marta Vatican tarehe 10 Junuari 2020 Papa Franciski akiwa anahubiri katika kanisa la Mtakatifu Marta Vatican tarehe 10 Junuari 2020  (Vatican Media)

Papa Francisko: jichafue mikono kwa matendo mema kwa wengine!

Wazo kuu la Papa Francisko wakati wa mahubiri ya asubuhi tarehe 10 Januari 2020 katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican ni juu ya upendo na kwamba ni wa dhati na hujifafanua kwa njia ya kutenda yaliyo mema kwa wengine.Ni katika kuongozwa na somo la liturujia ya siku.Papa amesema sintofahamu ni namna ya kujificha kutompenda Mungu na jirani.Kinyume chake ni lazima kujichafua mikono kwa ajili ya kutenda mema ukikumbuka ni Mungu aliyetupenda akiwa wa kwanza.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 10 Januari 2020, Papa Francisko ameadhimisha Misa katika Kanisa la Mtakatifu Marta, Vatican ambapo somo la liturujia ya siku kutoka Barua ya kwanza ya Mtakatifu Yohane, imemwongoza katika mada ya upendo na hivyo kutoa mwaliko kwa waamini kuona na kutafakari kwa kina juu ya upendo wa dhati. Mtume Yohane anathibitisha kutambua nini maana ya upendo.Yeye alipata uzoefu wa kuingia ndani ya moyo wa Yesu na alijua namna alivyojionesha. Katika barua yake anafundisha jinsi ya kupenda na jinsi tulivyopendwa.

Ni Mungu aliyetupenda akiwa wa kwanza

Papa Francisko katika kuthibitisha hayo ameweka bayana mambo mawili: msingi wa kwanza ni upendo. Sisi tunampenda Mungu kwa sababu Yeye alitupenda akiwa wa kwanza. Mwanzo wa upendo unatoka kwake. Mimi ninaanza kumpenda au ninaweza kumpenda kwa sababu ninajua kuwa Yeye alinipenda akiwa wa kwanza. Iwapo yeye asingetupenda kwa hakika nasi pia tusingeweza kupenda, amethibitisha Papa na baadaye kutoa mfano: “Iwapo mtoto ambaye amezaliwa punde na siku chache angekuwa anaweza kuzungumza, kwa hakika angeeleza hali halisi hii kwamba “ninahisi kupendwa na wazazi”. Na kile wafanyacho wazazi ni sawa sawa na anachofanyia Mungu. Kwani alitupenda akiwa wa kwanza. Jambo hili linafanya kuzaliwa na kukuza uwezo wetu wa kupenda. Hii ndiyo maana ya wazo la upendo, kwani tunaweza kupenda tu, kwa sababu Mungu alitupenda akiwa wa kwanza.

Ni mwongo asemaye kumpenda Mungu wakati anamchukia ndugu

Jambo la pili ambalo anasepa Mtume Paulo kuhusu juu ya kuficha ni hili: “Ikiwa mmoja anasema ninampenda Mungu na anamchukia ndugu, ni mwongo”. Papa Francisko anabainisha kwamba, Yohane hasemi kuwa hana adhabu au anakosea, bali anasema ni “mwongo” kwa maana hiyo hata sisi tunapaswa kujifunza hili: mimi nina mpenda Mungu, ninasali, ninaungana kiundani na kujisahu kabisa ndani mwake…? na baadaye ninabagua wengine, ninachukia wengine au siwapendi, kwa urahisi au mimi ninakuwa tofauti na wengine… Yeye hasemi “umekosea”, anasema “wewe ni mwongo”. Na neno la Biblia ni wazi kwa sababu neno la kuwa mwongo ndiyo tabia ya kweli ya ibilisi, ambaye ni mlaghai mkuu, kama lisemavyo Agano jipya kwamba Ibilisi ni baba wa ulaghai. Hili ndilo jina la Ibilisi litolewalo katika Biblia. Iwapo wewe unasema kumpenda Mungu na unamchukia ndugu yako, huko sehemu nyingine, wewe ni mwongo. Na Katika hili hakuna makubaliano amesisitiza Papa Francisko.

“Wengi wanaweza kutafuta samahani za kutopenda, na mwingine anaweza kusema: Padre mimi sina chuki, lakini kuna watu wengi wananifanyia vibaya au mimi siwezi kukubalina na watu au siwezi kukubali kwa sababu hana adabu au ubaya”. Papa anasisitiza, juu ya upendo huo akielekezwa na Mtakatifu Yohane anapoandika kuwa “asiyependa ndugu yake anayemwona, hawezi kumpenda Mungu hasiyemwona”. Kwa maana hiyo kama huna uwezo wa kupenda watu, ambao wako karibu na unaoishi nao, huwezi kusema unampenda Mungu usiye mwona kwa maana hiyo wewe ni mwongo”

Upendo ni wa dhati na wa kila siku

Papa Francisko akiendelea kufafanua juu ya upendo huo anasema, hata hivyo siyo tu hisia za chuki zinaweza kukataa kuchanganyikana katika mambo ya wengine. Lakini hii siyo nzuri, kwa sababu upendo huonyeshwa kwa kutenda yaliyo mema. Ikiwa mtu mmoja anasema: “ili niweze kuwa msafi ninakunywa maji yaliyochujwa”. Utakufa! Kwa sababu maji hayo hayasaidii katika misha. Upendo wa kweli siyo maji yaliyochujika. Ni maji ya kila siku, ambayo yana matatizo yake, upendo wake, chuki zake na ndiyo hiyo.  Kupenda kwa dhati siyo upendo wa maabara. Na mafundisho yake ya kitume yako wazi. Lakini kuna mtu ambaye siyo wa kumpenda Mungu na siyo wa kumpenda jirani na ambao kidogo wamejificha na sintofahamu. Kwa mfano mimi sitaki hili, sitaki maji yaliyochujika, Mimi sijichanganyi na matatizo ya wengine. Na kumbe unapaswa kusaidia na kusali. Kwa kuendeledela Papa Francisko ametaja msemo wa Mtakatifu Alberto Hurtado aliyesema kwamba: “Ni vema kutofanya vibaya, lakini kutotenda wema ni vibaya”. Kwa maana hiyo upendo wa kweli lazima ukupelekee kutenda yaliyo mema (…)  na zaidi kujichafua mikono wakati unatenda mantendo ya upendo, Papa ameelekeza.

Kupitia njia za imani tunashinda ulimwengu

Siyo rahisi lakini inawezakana kupita njia za imani, na kuna uwezekano wa kushinda dunia, fikira za ulimwengu ambazo zinazuia kushinda. Hii ndiyo njia, anayothibitisha Papa na kubainisha kuwa, katika njia hizi hakuna kuingia na sintofahamu kwa wale wanaonawa mikono yao dhidi ya matatizo, au wale ambao hawataki kujichanganya na matatizo katika kusaidia na kutenda wema; hapo hawaingii wenye manabii wa uongo wenye moyo uliochujwa kama maji, na ambao wanasema kumpenda Mungu lakini wanashindwa kuelewa kuwa upendo unaanzia kwa jirani. Kwa kuhitimisha Papa anamwomba Bwana aweze kutufundisha ukweli huu, uhakika wa kuwa tumependwa kwanza na Yeye na kuwa na ujasiri wa kuwapenda ndugu.

PAPA MAHUBIRI
10 January 2020, 12:42