Tafuta

Vatican News
Mwana wa Mungu alifanyika mwili.Na si tu alikuja kukaa katikati ya watu lakini alijifanya kuwa mmoja wa watu, yaani mmoja wetu Mwana wa Mungu alifanyika mwili.Na si tu alikuja kukaa katikati ya watu lakini alijifanya kuwa mmoja wa watu, yaani mmoja wetu  (Vatican Media)

Papa:Injili siyo tamthiliya.Onesho la ishara ya Mungu kwetu!

Papa Francisko kabla ya sala ya malaika wa Bwana ameeleza jinsi gani Yesu anaendelea kuja katikati yetu ili kila mmoja aweze kujibu wito wake wa utakatifu kwa upendo na kushuhudia ile zawadi ya bure ambayo Mungu ametupatia.Ishara ya kushangaza ya Kuzaliwa kwa Bwana ni ile ya Neno la milele lililofanyika mwili.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko tarehe 5 Januari 2020 kabla ya sala ya Malaika wa Bwana kwa mahujaji na waamini walio kusanyika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro ameanza tafakari kwa kusema: “katika Dominika ya pili ya kipindi cha Noeli, masomo ya Biblia yanatusaidia kuelekeza mtazamo  wetu  ili kuwa na utambuzi kamili wa maana ya Kuzaliwa kwa Yesu. Injili kwa njia ya utangulizi wa Mtakatitu Yohane, inatuonesha mambo mapya ya kushangaza. Neno la milele, Mwana wa Mungu alifanyika mwili. Na si tu alikuja kukaa katikati  ya watu, lakini pia alijifanya kuwa mmoja wa watu, yaani mmoja wetu! Na baada ya tukio hili la  kuelekeza maisha yetu, hatuna haja tena ya kuwa na sheria peke yake, ya taasisi, bali ya mtu mmoja, Mungu mtu, Yesu ambaye anatuelekeza kuhusu maisha na kutufanya twende katika njia ambayo aliipitia akiwa wa kwanza".

Mungu anabariki ishara za upendo kwa njia ya Yesu

Papa Francisko akiendelea na tafakari yake amesema Mungu anabariki ishara za upendo uliotimizwa katika Yesu ( Rej Ef 1,3-6.15-18). Katika ishara hiyo kila mmoja anaweza kupata wito wake msingi. Je ni upi? Paulo anasema hivi:  "sisi ni washiriki pamoja wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili". Mwana wa Mungu alijifanya mtu kwa ajili yetu, wana wa Mungu. Kwa maana hiyo Mtoto wa milele alijifanyika mwili ili kutuonesha uhusiano wake wa utoto na Baba.

Injili ya Kristo siyo tamthiliya

Papa Francisko akieledelea kufafanua tafakari hii amesema "wakati tunaendelea kutafakari kwa kina ishara ya ajabu ya Pango, Liturujia ya leo inatuambia kuwa Injili ya Kristo siyo tamthiliya, siyo hadithi  au historia za kujenga hapana. Injili ya Kristo imejaa maonesho ya ishara ya Mungu. Ni ishara ya Mungu,  ya mwanadamu na juu ya dunia".  Na zaidi anaongeza kusema: "Ni ujumbe wakati huo huo rahisi na mkubwa mno ambao unatusukuma kujiuliza, je ni mpango gani wa dhati ambao umewekwa ndani mwangu na Bwana ili kuoona  kwa mara nyingine ule wa kuzaliwa kwake katikati yetu? Hata hivyo ni Mtatifu Paulo anashauri jibu lake Papa anasema. Jibu hili ni kwamba : " Mungu alitangulia kutuchagua …ili tuwe watakatifu na wasio na waa mbele yake katika upendo”. Na tazama ndiyo maana ya kuzaliwa kwa Bwana amebainisha Papa Francisko!

Ikiwa Bwana anaendelea kuja katikati yetu

Ikiwa Bwana anaendelea kuja katikati yetu na ikiwa anaendelea kujifanya zawadi kwa njia ya Neno ni kwa sababu kila mmoja wetu aweze kujibu wito huo wa kugeuka kuwa watakatifu katika upendo. Utakatifu ni wa Mungu na muungano na Yeye, ulio wazi na wenye wingi wa neema zisizo na mwisho. Utakatifu ni kuhifadhi ile zawadi ya Mungu aliyotupatia. Ni kwa njia hiyo tu ya kuhifadhi zawadi  ya bure na ndiyo maana ya kuwa Mtakatifu! Kwa maana hiyo anayepokea utakatifu kama zawadi ya neema hawezi kubaki bila kuifafanua katika matendo ya dhati ya  kila siku, Papa Francisko amesisitiza.

Zawadi hiyo ya bure niliyopewa ninaitafsiri vipi katika matendo?

Je zawadi niliyopewa bure ninaitafsiri vipi? “Zawadi hiyo, na neema ambayo Mungu amenipatia, ninaitafsiri katika matendo ya dhati ya kila siku katika kukutana na wengine”. Upendo huo , huruma hiyo kwa jirani, ndiyo kioo cha upendo wa Mungu na wakati huo huo inatakasa mioyo yetu na kutufanya kuwa na msamaha  na kutufanya siku hadi siku watu wasio na mawaa” Lakini je kutokuwa na mawaa ina maana ya kwamba: mimi ninapaswa kutoa doa. Kutokuwa na mawaa kwa maana ya kwamba Mungu anaingia ndani mwetu, aliye zawadi ya bure ya Mungu. Na anaingia ndani mwetu na sisi tunahifadhi  zawadi hiyo na kuwapatia wengine. Kwa kuhitimisha tafakari yake Papa amesema: "Bikira Maria atusiadie kupokea kwa furaha na shukrani ishara ya Mungu ya upendo uliotimizwa na Yesu Kristo.

05 January 2020, 14:10