Tafuta

Vatican News
Makanisa ya kiorthodox ya mashariki na nchi nyingine zinajiandaa kuadhimisha mwaka mpya  tarehe 25 Januari 2020 ambapo Papa Francisko amewatumia salam za heri Makanisa ya kiorthodox ya mashariki na nchi nyingine zinajiandaa kuadhimisha mwaka mpya tarehe 25 Januari 2020 ambapo Papa Francisko amewatumia salam za heri   (AFP or licensors)

Papa Francisko:heri ya mwaka mpya kwa nchi za mashariki!

Maombi kwa ajili ya amani,majadilianao na mshikamano ndiyo wito wa Papa alioutoa wakati wa kumaliza katekesi yake akikumbuka tarehe 25 Januari kuwa ni maadhimisho ya Mwaka Mpya katika nchi za Mashariki na nchi mbalimbali zinazoafuata kalenda ya mwezi.Amekumbusha umuhimu wa malezi,hekima na busara ndani ya familia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Salam na heri na wito wa pamoja katika kusali  na kuomba zawadi ya amani, majadiliano  na mshikamano ni mambo yaliyotajwa na Papa Francisko mara baada ya katekesi yake kwa mahujaji na waamini waliofikia katika ukumbi wa Paulo VI, Vatican, akiwalenga yale makanisa na nchi ambazo wanaadhimisha Mwaka mpya tarehe 25 Januari 2020 hasa katika nchi za mashariki na nyingine zenye kalenda ya kutumia mwezi.

Aidha Papa Francisko anakumbuka familia

Kadhalika Papa Francisko amekumbuka familia zote ili ndani mwake paweza kuwa mahali ambao kunaoneshwa na kufundishwa na mfano wa elimu na fadhila ya ukarimu na hekima, heshima kwa ajili ya kila mtu na maelewano ya kazi ya uumbaji. Anaomba Mungu aweze kutoa zawadi ya lazima katika dunia ya leo. Hakusahau kama kawaida yake kuwasalimia mahujaji wote  kutoka pande zote za dunia, wakiwemo vijana, wazee, wagonjwa na wanandoa wapya.

22 January 2020, 12:56