Tafuta

Katika maadhimisho ya Siku ya Mtakatifu Maria Mama wa Mungu tarehe Mosi Januari 2020 kiini cha tafakari ya Papa ni hadhi ya mwanamke kama mama wa maisha na pasipo yeye hakuna maisha! Katika maadhimisho ya Siku ya Mtakatifu Maria Mama wa Mungu tarehe Mosi Januari 2020 kiini cha tafakari ya Papa ni hadhi ya mwanamke kama mama wa maisha na pasipo yeye hakuna maisha! 

Papa Francisko:dhuluma dhidi ya wanawake ni kukufuru Mungu!

Katika Siku kuu ya Maria Mtakatifu Mama wa Mungu na Siku ya 53 ya Kuombea Amani Duniani Papa Francisko anashauri kutazama Bikira ambaye ni mwanga wa kuongoza safari ya Kanisa.Kwa kutazama mfano wake anawaalika kwa nguvu zote kuheshimu mwili wa mwanamke,unaonyonywa,unaodhulumiwa,unaotumiwa na kubakwa na ili kuulinda hadhi ya umama wake ambao mara nyingi pia unabezwa kwa kisingizio cha ukuaji wa uchumi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, (Gal 4,4). Alizaliwa na mwanamke na ndivyo alivyokuwa Yesu. Yeye hakuonekana katika dunia ya watu wazima bali kama isemavyo, Injili alitungwa mimba  (Lk 2,21). Ulijifanya mtu ili kuwa na ubinadamu wetu, siku hadi siku na  mwezi baada ya mwezi. Katika umbu la mwanamke, Mungu na ubinadamu vimeungana na ili visitengane kamwe. Hata sasa, Yesu anaishi mbinguni katika mwili ambao alichukuliwa kwenye tumbo la mama yake. Kwa Mungu kuna mwili wa binadamu. Ndiyo mwanzo wa mahubiri ya Papa Francisko, wakati wa misa takatifu ya sikukuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu tarehe Mosi Januari 2020 ambayo ni samabamba na Maadhimisho ya Siku ya 53 ya kuombea Amani duniani.

Siku ya kwanza ya Mwaka ni kuadhimisha pingu kati ya Mungu na mwanadamu

Akiendelea na mahubiri Papa anasema katika siku ya kwanza ya Mwaka, tunaadhimisha pingu kati ya Mungu na mwanadamu, aliyezinduliwa katika umbu la mwanamke. Ubinadamu wetu utakuwapo daima katika Mungu na daima Maria atakuwa Mama wa Mungu. Ni mwanamke na mama  hicho ni ndiyo muhimu. Kutoka kwa  mwanamke, ulikuja wokovu na kwa maana hiyo hakuna wokovu bila mwanamke!

Kuzaliwa kwa ubinadamu unaanzia kwa mwanamke

Papa Francisko akifafanua maana ya kuzaliwa  na mwanamke anasema,  kuzaliwa kwa ubinadamu unaanzia na mwanamke. Wanawake ni kisima cha maisha. Walakini kila wakati huwa wanachukizwa, wanapigwa, wanabakwa, wanalazimishwa kufanya ukahaba na kukandamiza maisha wanayoibeba tumboni mwao. Kila ukatili wowote, na  kudhulumiwa kwa wanawake ni kukufuru kwa Mungu aliyezaliwa na mwanamke.

Wokovu kwa ubinadamu ulitokana na mwili wa mwanamke

Na kwa jinsi tunavyouchukulia mwili wa mwanamke ndipo tuweza kuelewa kiwango chetu cha ubinadamu…Je! Ni mara ngapi mwili wa mwanamke unatolewa sadaka kwenye madhabahu mbaya ya matangazo ya kibiashara, mapato, picha mbaya, unyonyaji  ulio katika uso wa juu juu na kutumiwa? Mwanamke lazima awe huru dhidi ya ununuzi wa kibiashara na kutumiwa, lazima aheshimiwe na kutukuzwa; ni mwili mzuri kabisa ulimwenguni, Yeye alichukua mimba na akazaa Upendo ulio tuokoa! Leo hii umama pia umedhalilishwa, kwa sababu ya ukuaji pekee unaotuvutia ni ukuaji wa uchumi. Kuna akina mama ambao wanajihatarisha katika safari zisizo na kizuizi ili kujaribu kutafuta maisha kwa maangaiko makubwa katika kupata tunda la  maisha bora ya baadaye na wakati huo huo wanahukumiwa kuwa ni namba kubwa na watu ambao matumbo yao yamejaa lakini kuwa na vitu na moyo mtupu usio na upendo.

Ni mara ngapi mwili wa mwanamke unadhalilishwa katika matangazo ya kibiashara

Alizaliwa na mwanamke. Papa Francisko anasema kwa mujibu wa simulizi ya Biblia, Mwanamke alifika  wakati wa mwisho wa kazi ya  uumbaji kama inavyosimulia kitabu cha Mwanzo. Yeye kwa hakika anafunga mwisho wa kazi ya uumbaji. Yeye ni kizazi na ulinzi wa maisha, yeye ni muungano na kila kitu na kutunza kila kitu. Ndiyo anayoya fanya Mwanamke katika Injili ya siku. “Maria alikuwa anatunza yote na kutafakari kwa kina katika moyo wake”. Alikuwa anatunza yote, kwa maana ya kutunza   furaha kwa ajili ya kuzaliwa kwa Yesu na uchungu kutokana na kukosa ukarimu huko Betlehemu; upendo wa Yosefu na mshangao wa wachungaji; ahadi na  hukosefu wa uhakika wa wakati ujao. Yote hayo alikuwa akiyatafakari ndani ya moyo wake na ndani ua moyo kulikuwa na nafazi hiyo haya vizingiti.. Kwa sababu katika moyo wake alikuwa anaweza kuyasawazisha yote kwa upendo na alikuwa anamkabidhi Mungu yote.

Maisha yaliyofichika ya Yesu yanaonekana

Katika Injili matendo ya Maria yanaonekana kwa mara nyingine tena. Mwisho wa maisha yaliyokuwa yamefichika ya Yesu, kwani wanasema kuwa Mariama alikuwa anayafikiri moyoni mwake. Marudio hayo yanatufanya kutambua kuwa huhifadhi na kutafakari ndani ya moyo ishara ambayo Mama alikuwa mara nyingi na ilikuwa ni kawaida , hii ni kuonesha kuwa maana ya  kushi siyo, tu kuendelea kutoa mambo, lakini hata kuyachukulia katika moyo jini mambo yalivyo na yaliyopo. Na hiyo ni kwa  yule tu anayetazama kwa moyo, anaona vizuri kwa sababu anatambua kuona ndani. Anatambua kuona mtu licha ya makosa yake aliyo nayo, kuona  ndugu zaidi ya udhaifu wake alio nao, matumaini na matatizo  na kuona Mungu kwa kila kitu.

Tuombe Mungu kuwa na mtazamo wa moyo

Papa Francisko anasema “ tunapoanza mwaka mpya tujiulize, je ninatambua kutazama mtu kwa moyo? Je watu ninaoishi nao wako rohoni mwangu? Au ninawaharibu kwa masengenyo yangu?  Na zaidi,  Je kiini cha moyo wangu ni Bwana? Au nina thamanisha mambo mengine kama vile  mahitaji yangu binafsi ya utajiri na mamlaka? Ni kwa njia hiyo tu ya kuwa na maisha  ya kina ndani ya moyo tutaweza kutunza na kushinda tofauti ambazo zinatuzunguka. Tuombe neema hii ya kuweza kuishi mwaka kwa shauku ya kuchukuliana kwa moyo na wengine na kutunzana mmoja na mwingine.

Mafanikio ya wanawake ni mafanikio ya ubinadamu wote

Na hiyo hayo yatawezekana, ikiwa tunataka dunia iwe bora zaidi, aidha nyumbani pawe na amani na siyo uwanja wa vita, hasa ikiwa tunaweka hadhi ya kila mwanamke katika moyo wetu. Kutoka kwa mwanamke alizaliwa Mfalme wa amani. Mwanamke ni mtoaji na mpatanishi wa amani na lazima ahusishwe kikamilifu na michakato ya kufanya maamuzi. Kwa sababau wanawake wakiwezesha  kuonesha zawadi zao, dunia hii itajikuta inaungana zaidi na kuwa na amani zaidi. Kwa maana hiyo mafanikio ya wanawake ni mafanikio ya ubinadamu wote. Yesu amezaliwa hivi karibuni, alijiangaza  katika kioo cha mwanamke katika uso wa mama yake. Kutoka kwake alipata kubembelezwa, kwake yeye alibadilishana tabasamu za kwanza. Na kwake yeye alizindua mapinduzi ya huruma. Kwa kutazama Mtoto Yesu, Kanisa linaalikwa kuuendeleza. Hata yeye kwa hakika Maria ni mwanamke na katika Mwanamke anapata sifa zake zinazofanana. Anaona kwake asiyekuwa na dhambi, anahisi kusema hapana dhidi ya  dhambi na katika malimwengu. Kwake yeye anaona matunda na anahisi kuitwa  ili kutangaza Bwana na  kuzaa maisha. Kwake Yeye Mama anahisi kuitwa kupokea kila mtu kama mwanae.

Kukaribia Maria Kanisa linajitambua na kupata kitovu chake cha umoja

Kwa kumkaribia Maria Kanisa linajitambua, linapata kitovu chake na cha umoja wake. Adui wa asili ya ubinadamu ambaye ni shetani kinyume anatafuta kuwagawanya, kwa kuweka mipango yake ya utofauti, itikadi, mawazo ya pembeni na ya vyama. Lakini hatambui kuwa Kanisa  linatazamia kuanzia katika miundo, mipango na tabia. Tunaweza kutambua jambo lakini si katika moyo. Na hivyo ni kwa sababu Kanisa ni moyo wa mama. Sisi kama watoto leo hii tumwombe Mama wa Mungu ambaye anaunganisha kama watu waamini. “Ee Mama unayetoa matumani kwetu, tupatie umoja. Mwanamke wa wokovu tunakukabidhi mwaka huu, uulinde katika moyo wako. Na kwa pamoja Baba Mtakatifu ameomba wasali mara tatu kwa Mwanamke Mtakatifu kwamba “Mama wa Mungu, Mtakatifu Mama wa Mungu, Mtakatifu Mama wa Mungu!

 

 

01 January 2020, 12:28