Leo ni Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana katika Makanisa yote ya Mashariki katoliki na Orthodx.Papa Francisko amewatakia matashi mema ya Sikuu. Leo ni Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana katika Makanisa yote ya Mashariki katoliki na Orthodx.Papa Francisko amewatakia matashi mema ya Sikuu. 

Mawazo ya Papa kwa makanisa ya Mashariki:Noeli njema!

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, tarehe 6 Januari 2020 Papa Franisko mawazo yake kwa namna ya pekee yamewaendeea Makanisa ya mashariki katoliki na Kiorthodox ambayo mengi yao yanaadhimisha Siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana.Aidha amekumbuka Siku ya Utoto Mtakatifu wa kimisionari unaokwenda sambamba na adhimisho la Tokeo la Bwana kila tarehe 6 Januari ya kila Mwaka.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 6 Januari 2020 katika Maadhimsho ya Siku ya Tokeo la Bwana, mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana Papa Francisko  ameonesha wazo kuu kwa namna ya pekee ya kutoa matashi mema kwa ndugu  Makanisa ya Mashariki Katoliki na Kiorthodox ambayo mengi yanaadhimisha Siku Kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana. Kwa ajili yao na jumuiya zao anawatakia wawe na mwanga na amani ya Kristo Mwokozi.

Siku ya Utoto Mtakatifu

Katika siku hii ya Tokeo la Bwana sambamba na Siku kuu ya Utoto Mtakatifu ulimwenguni, Papa Francisko pia amewakumbuka na kuwatakia matashi mema kwa kusema: " leo hii inaadhimishwa Siku ya Utoto Mfakatifu kimisionari. Ni sikukuu ya watoto na vijana wadogo wamisionari ambao  wanafanya uzoefu wa kuishi wito ulimwenguni  wa utakatifu kwa kusaidia wenzao wenye kuhitaji zaidi, kwa njia ya sala na ishara ndogo ndogo za kushirikishana".

Salam mbalimbali na matashi mema ya Siku kuu ya Tokeo la Bwana

Salam pia zimewaendea na kuwakaribisha watu wote kutoka pande  zote za dunia. Aidha salam maalum kwa wale ambao wanaadhimisha kwa njia ya  maandamano ya kihistoria ya utamaduni katika sikukuu ya Tokeo la Bwana. Kwa  mwaka huu nchini Italia, toleo hili la Mamajusi limetokea katika eneo la Allumiere na Valle del Mignone, ambao wamefika mjini Vatican wakiwa wamevalia mavazi rasmi ya siku, kuwakilisha lile tukio la Mamajusi wa enzi hizo wanaosimuliwa katika Maandiko matakatifu ya Injili.

Vile vile ameongeza kukumbuka maandamano makubwa katika miji na vijijini nchini Poland! Katika fursa hiyo amewapa salam kwa ufafanuzi wa utamaduni wa siku hiyo, huku  akiwafikiria nchini Huispania, Amerika ya Kusini na Ujerumani, katika  kukuza utamaduni wao na ambao anawaomba waweze kuendelea kuhifadhiwa na urahisi wake wenye maana kikristo. Na kwa wote amewatakia sikukuu njema, lakini wasisahau kusali kwa ajili yake.

06 January 2020, 14:16