Tafuta

Tarehe 26 Januari 2020 Papa ameadhimisha Misa Takatifu katika Fursa ya Dominika ya Neno la Mungu. Tarehe 26 Januari 2020 Papa ameadhimisha Misa Takatifu katika Fursa ya Dominika ya Neno la Mungu. 

Dominika ya Neno la Mungu:Bwana anataka upokee neno kama barua ya upendo!

Katika Dominika ya kwanza ya Neno la Mungu,Papa Francisko ameeleza asili ya mahubiri ya Yesu.Ili kuelewa umuhimu wa kusikiliza ni lazima kuchota katika kisima cha maisha ambayo ni neno la Mungu.Neno linaoondoa giza na kukufikisha katika mwanga.Mungu hayupo mbali,alishuka duniani na kujifanya binadamu.Aliondoa kizingiti na kuondoa umbali huo. Yesu anabisha hodi mlangoni.Neno lake linafariji na kutia moyo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Yesu alianza kuhubiri (Mt 4,17) na kwa maana hiyo Mwinjili Matayo anatoa utangulizi wa huduma ya Yesu. Yeye alikuwa ni Neno wa Mungu na alikuja kuzungumza nasi kwa maneno yake na maisha yake. Katika Dominia ya Neno la Mungu tunakwenda katika asili ya kuhubiri kwake, kisima cha Neno la Maisha. Itusaidie Injili ya leo (Mt 4,12-23), ambayo inatueleza ni jinsi gani na mahali wapi, Yesu alianzia kuhubiri. Mwanzo ulikuwa namna gani? Ni kwa sentensi rahisi “ tubuni kwa maana Ufalme wa Mungu unakaribia (Mt 4,17). Huu ndiyo msingi wa hotuba zake, kwa kutaka kutueleza kuwa Ufalme wa Mungu unakaribia. Je ina maana gani? Ufalme wa Mbingu maana yake ni Ufalme wa Mungu kwa maana nyingine ni namna yake ya kutawala huku akijiwakilisha mbele yetu.

Ndiyo Mwanzo wa mahubiri ya Papa Francisko wakati wa Misa ya Neno la Mungu Tarehe 26 Januari 2020 katika Kanisa la Mtakatifu Petro Vatican. Ikiwa ni maadhimisho y amara ya kwanza ya Dominika ya Neno la Mungu kwa utashi wake ili iwe inaadhimishwa kila Dominika ya tatu ya Mwaka. Papa Francisko akiendelea na mahubiri amesema: “Kwa sasa Yesu anasema ufalme wa mbingu unakaribia na Mungu yuko karibu. Tazama  haya mapua , ujumbe wa kwanza: Mungu hayupo mbali ni yule anaishi mbinguni na alishuka duniani na kujifanya binadamu. Aliondoa kizingiti na uweka umbali kuwa sufuri. Hatukuwa tunastahili, Yeye alishuka na akuja kukutana nasi. Ukaribu huu wa Mungu kwa watu wake ndiyo tabia yake tangu mwanzo , hata katika Agano la Kale. Yeye alikuwa akiwambia watu wake “jinis gani alivyo na watu wake hivi karibu, kama jinis mimi nilivyo karibu nawe? Ukaribu wake huu ulifanyika mwili katika Yesu.

Ni ujumbe wa furaha

Ni ujumbe wa furaha amesema Papa. Kwani Mungu alikuja mwenyewe kututembelea kwa kujifanya binadamu. Yeye hakuchukuwa hali yetu ya kibinadamu kwa maana ya uwajibikaji, hapana, bali kwa ajili ya upendo.  Kwa ajili ya upendo alichukua ubinadamu wetu kwa maana unachukuliwa kwa kile ambacho kinapendwa. Mungu alichukua ubinadamu wetu kwa sababu anatupenda bure na kutupatia ule wokovu ambao peke yetu hatuwezi kuupata. Yeyey anatamani kukaa nasi,kutupatia uzuei wake wa kusihi, wa amani katika moyo , wa furaha ya kuwa tu mesamehewa na kuhisi kupendwa. Kwa maana hiyo tunaweza kutambua mwaliko wa moja kwa moja wa Yesu asemaye “TUBUNI “ kwa maana nyingine “badilisheni maisha”. Kubadili maisha kwa sababu ndiyo mwanzo mpya wa kuishi . Umekwisha muda wa kuhisi ubinafsi na kuanza kipindi cha kuishi na Mungu na kwa ajili ya Mungu, kwa ajili ya wengine, kwa upendo na upendo.

Papa Francisko anasisitiza kwamba Yesu anarudia hata leo hii kwako akisema: “ kuwa jasiri, mimi niko karibu nawe, nipe nafasi na maisha yako yatabadilika”. Yesu anabisha hodi mlangoni. Kwa maana hiyo Bwana anakupatia Neno lake, kwani anataka ulipokee kama barua ya upendo ambayo amekuandikia, amekufanya uhisi kuwa Yeye yuko karibu nawe. Neno lake linafariji, na kutia moyo. Na wakati huo huo linashawishi kuwa na uongofu. Zaidi neno husababisha ubadilike kwa njia ya uongofu, hututikisa, hutuokoa kutokana katika kupooza kwa ubinafsi. Kwa sababu Neno lake lina nguvu ya namna hii: hubadilisha maisha, kukupitisha ili uondoke kutoka gizani hadi kufikia  nuru. Hii ndiyo nguvu ya” Neno lake amesisitiza Papa Francisko.

Kutazama mahali Yesu anaanzia ili kugundua sababu za giza

Papa Francisko amesema ikiwa tunatazama mahali ambapo Yesu alianzia kuhubiri, tunagundua kwamba ailianza kwa usahihi katika  mikoa ambayo ilichukuliwa kuwa  ni ya “giza”. Katika Somo la Kwanza na Injili vinazungumza kwa hakika wale ambao walikuwa wanaishi katika Kanda na giza la kifo”. Hawa ni wakazi wa  maeneo ya Zabulon na  Neftali, katika njia ya bahati ya Yordani , Galilaya ya watu  (Mt 4,15-16; cfr Is 8,23-9,1). Galilaya ya watu , ni kanza ambayo Yesu alianza kuhudubu na ilikuwa inaitwa namba hiyo kwa sababu ni eneo ambali wakazi wake walikuwa ni tofauti, na ilikuwa ni matokeo ya mchanganyiko wa kweli wa watu, lugha na tamaduni tofauti. Kulikuwa na njia ya bahari iliyokuwa inawakilishwa na wavuvi, wafanyabiashara na wageni. Kiukweli haikuwa mahali ambapo kulikuwa na usafi wa kidini wa watu waliochaguliwa.  Walakini Yesu alianza kuhubiri kutoka hapo: na  siyo katika uwanja  wa jengo la hekalu huko Yerusalemu, lakini kutoka upande wa pili wa nchi, kutoka Galilaya ya watu, yaani  eneo la mpaka, na kwa maana nyingine kuaznisha pembezoni.

Ujumbe wake

Tunaweza kupata ujumbe huu kwamba Neno ambalo linaokoa haliendi kutafuta mahali pa faragha, safishwa na penye usalama. Linakuja katika ugumu wetu, na katika giza letu.  Leo hii kama zamani Mungu anatamani kuttembelea maneneo hayp mahali ambamo tunafikiria Yeye hawezi kufika. Ni mara ngapi sisi tunafunga milango na kupendelea kujifucha katika mchanganyiko wetu, katika vuli wetu, na mchanganyo wa maisha. Tunaweka muhuri ndani mwetu wakati tunakwenda kwa Bwana kufanya sala ndogo lakini za  kijuu juu, na kuwa makini ili ukweli wake usije tingisha ndani mwetu. Huu ni unafiki wa kujificha, anasema Papa, lakini Yesu leo hii anasema katika Injili “ alikuwa akizunguka katika Galilaya yote(…) akihubiri habari njema  na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu.

Kuzunguka kanda yote maana yake yenye watu wengi, kanda ngumu. Na wakati huo huo Yesu hana hofu ya kugundua mioyo yetu, mahali petu pachungu na pagumu. Yeye anatambua kusamehe tu na kutuponyesha. Ni kwa njia ya uwepo wake tu unatubadili, ni kwa njia ya Neno lake tu linatupyaisha. Yeye aliyezungukia njia ya bahari tumfungulie njia kwa dhati,  tumfungulie njia zetu za dhuluma zaidi, zile ambazo tunazo ndani na ambazo hatutaki kuona au kuficha. Tuzifungue njia zetu za kudhulumu zaidi, huku tukiruhusu Neno lake liingie kwetu, ambalo ni “hai,” na dhati kuchang’anua hisia na mawazo ya moyo» (Heb 4,12).

Je Yesu alianza kuzungumza kwa nani: wavuvi kwanza

Katika kuhitimisha Papa Francisko ameelezea matiki ya tatu Yesu alizungumza na nani? Injili inasema kuwa “ wakati Yesu alipokuwa akitembea kandao ya bajari ya Galilaya aliona ndugu wawili (…) wakitupa jarifa baharini, kwa maana walikuwa wavuvu. Akawambia , Nifuateni nami nitawafanya wavuvi wa watu”. (Mt 4,18-19). Watu wa kwanza waliotuwa walikuwa ni wavuvi na siyo watu ambao wamechanguliwa kwa uangalifu kulingana na uwezo wao au waliotakasika ambao walikuwa hekaluni wakisali, bali watu wa kawaida ambao walikuwa wanafanya kazi. Hapa tunaweza kuona kuwa Yesu aliwaambia kuwa “nitawafanya wavuvi wa watu”. Anazungumza na wavuvi na kutumia lugha yao inayoeleweka. Anawavutia kuanzia katika maisha yao. Anawuta hao mahalia ambao wapi na jinsi walivyo ili kuwahisisha katika utume wake mwenyewe.  Na kwa haraka wakaacha nyavu za ona kufuata (Mt 4,20)

Kwa nini mara moja? Kwa sababu tu walihisi kuvutiwa. Hawakuwa wepesi na tayari kwa sababu walikuwa wamepokea agizo, lakini kwa sababu walikuwa wamevutiwa na upendo. Ili kumfuata Yesu, haostoshi kuwa ahadi nzuri, bali, lazima mtu asikilize wito wake kila siku. Ni kwa njia yake tu anayetutambua anatupenda kwa kina, anayetufanya tuelekee makubwa katika bahari ya maisha. Kama alivyofanya kwa wale wafusia ambao walikuwa wanamsikiliza. Kwa njia hiyo tunahitaji Neno lake, kusikiliza hata katikati ya maelfu na maelfu ya maneno ya kila siku, neno tu ambalo halizungumzi juu ya mambo bali linazungumza kuhusu maisha.  Papa Francisko anaalika kutengeneza nafasi ndani mwetu kwa ajili ya Neno la Mungu! Kilisoma kila siku haya ndogo ya Biblia. Tuanze na Injili, ibaki imefunguliwa katika meza ya nyumbani, tuipeleke katika mifuko yetu au katika miokba yetu, tuitazama katika simu za mikononi, tuache kila siku ituongoze. Tutagundua kuwa Mungu yuko karibu nasi, anatuangazia giza letu na kwa upendo anatuongoza mahali pakuu katika maisha yetu

 

 

 

26 January 2020, 14:01