Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 1 Desemba 2019 amezindua rasmi Waraka wake wa Kitume "Adimirabile signum" yaani "Ishara ya Kushangaza": Maana na Umuhimu wa Pango la Noeli. Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 1 Desemba 2019 amezindua rasmi Waraka wake wa Kitume "Adimirabile signum" yaani "Ishara ya Kushangaza": Maana na Umuhimu wa Pango la Noeli. 

Yaliyojiri wakati wa uzinduzi wa Waraka wa Kitume: Pango la Noeli

Waraka wa Kitume “ADMIRABILE SIGNUM” yaani “Ishara ya Kushangaza”: Maana na Umuhimu wa Pango la Noeli”. Kwa ufupi kabisa: Pango la Noeli ni alama ya kawaida kabisa lakini yenye kushangaza katika maisha ya Kikristo. Waraka huu wa Kitume ni nyenzo msingi kwa waamini katika Kipindi hiki cha Majilio sehemu ya mchakato wa imani kwa ajili ya maandalizi ya Sherehe ya Noeli.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko mara baa da Sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili ya kwanza ya Kipindi cha Majilio, tarehe 1 Desemba 2019, kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican aliwaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kumsindikiza katika hija yake ya kichungaji kwenye Madhabahu ya Wafranciskani huko Greccio, Rieti, Mkoani Lazio, nchini Italia. Hii ni mara ya pili kwa Baba Mtakatifu kutembelea Pango la kwanza kabisa la Noeli lililotengenezwa na Mtakatifu Francisko wa Assisi. Lakini wakati huu ametia mkwaju kwenye Waraka wa Kitume “ADMIRABILE SIGNUM” yaani “Ishara ya Kushangaza”: Maana na Umuhimu wa Pango la Noeli”. Kwa ufupi kabisa anasema, Pango la Noeli ni Ishara ya kawaida kabisa lakini yenye kushangaza katika maisha ya Kikristo. Waraka huu wa Kitume ni nyenzo msingi kwa waamini katika Kipindi hiki cha Majilio sehemu ya mchakato wa imani kwa ajili ya maandalizi ya Sherehe ya Noeli.

Baba Mtakatifu alipowasili Madhabahuni hapo, amelakiwa na viongozi wa Serikali na Kanisa kutoka Jimbo Katoliki la Rieti waliokuwa wameandamana pamoja na Askofu mkuu Salvatore Rino Fisichella, Rais wa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Uinjilishaji Mpya. Baada ya sala fupi Madhabahuni hapo, Baba Mtakatifu Francisko akitia mkwaju kwenye Waraka wa Kitume “ADMIRABILE SIGNUM” yaani “Ishara ya Kushangaza”: Maana na Umuhimu wa Pango la Noeli”. Baba Mtakatifu amepata pia fursa ya kuwasalimia watoto wa shule ya msingi waliopamba ujio wake kwa nyimbo za Noeli huku wakiwa wamevalia mavazi ya kitamaduni! Kwa hakika watoto walikuwa wanapendeza na mara nyingi hawa ndio wanaowahamasisha wazazi wao kutengeneza Pango la Noeli.

Papa: Greccio

 

02 December 2019, 10:54