Tafuta

Maandishi ya Papa Francisko kwa mkono wake katika fursa ya kuwatakia matashi mema ya kufikisha miaka 170 ya Gazeti la "Civilta' Cattolica" yaani gazeti la 'ustaarabu katoliki' Maandishi ya Papa Francisko kwa mkono wake katika fursa ya kuwatakia matashi mema ya kufikisha miaka 170 ya Gazeti la "Civilta' Cattolica" yaani gazeti la 'ustaarabu katoliki' 

Ujumbe wa Papa kwa ajili ya miaka 170 ya Civiltà Cattolica!

Katika fursa ya kuadhimisha miaka 170 tangu kuanza kwa gazeti la Wajesuit (1850-2020),Papa Francisko ametuma ujumbe wake kwa Mkurugenzi wa Gazeti hilo ulioandikwa kwa mkono wake na ambao utaonekana hata katika ukurasa wa Makala yao ya Januari 2020."Asante kwa msaada mnao utoa hata kwangu.Ninawatakia muwe wabunifu na fanyeni mang’amuzi na kupambana na chuki,ubahili na hukumu zisizo na sababu”.

“Miaka 170 iliyopita Mwenyeheri Pio IX aliwaomba Shirika la Yesu ( Jesuit) kuanzisha Gazeti 'La Civiltà Cattolica' (yaani “ustaarabu katoliki”). Na tangu wakati huo linasindikiza kwa uaminifu Papa. Asante kwa msaada mnaoutoa hata kwa ajili yangu." "Endelea kuishi kwa nguvu kati ya maisha na mawazo mkiwa na macho ambayo yanasikiliza kwa kutambua kuwa: “Ustaarabu Katoliki” ni ule wa Msamaria mwema".

Ninawatakia muwe wabunifu katika Mungu kwa kufanya ugunduzi wa njia mpya,shukrani pia kwa roho mpya ya kimataifa inayoangazia gazeti hili: sauti nyingi za kurasa zinavuka mipaka mingi na kuwezesha kusikika.

Fanyeni mang’amuzi juu ya lugha, pambaneni dhidi ya chuki, ubahili na hukumu zisizo na sababu. Na zaidi ya yote, msiridhike na kutoa mapendekezo ya kulalamikia urekebishaji au uboreshaji usio wa kweli: badala yake, kubali changamoto ya kufurika kwa wasiwasi wa wakati huu, ambao Mungu anafanya kazi ndani mwake daima!

30 December 2019, 14:12