Tafuta

Kardinali  Prosper Stanley Grech amefariki dunia tarehe 30 Desemba 2019.Alikuwa ni mwanashirika wa Mtakatifu Agostino na mmoja wa waanzilishi wa Taasisi ya Mafunzo ya Baba wa Kanisa Agostino Kardinali Prosper Stanley Grech amefariki dunia tarehe 30 Desemba 2019.Alikuwa ni mwanashirika wa Mtakatifu Agostino na mmoja wa waanzilishi wa Taasisi ya Mafunzo ya Baba wa Kanisa Agostino 

Salam za rambi rambi za Papa Francisko kufuatia na kifo cha Kard.Grech

Kardinali Prosper Grech amefariki dunia tarehe 30 Desemba 2019 katika Hospitali ya Santo Spirito,Sassia mjini Roma. Na Baba Mtakatifu Francisko ametuma salam za rambi rambi kufuatia na kifo chake kwa Padre ALEJANDRO MORAL ANTÓN,O.S.A Mkuu wa Shirika la Mtakatifu Agostino.Katika maandishi hayo anaonesha kusikitishwa kwake na kumwombea roho yake ipumzike kwa amani.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 31 Desemba 2019, Baba Mtakatifu Francisko ametuma telegram ya  salam za  rambi rambi kufuatia na kifo cha Kardinali Crech kwa Padre ALEJANDRO MORAL ANTÓN,O.S.A Mkuu wa Shirika la Mtakatifu Agostino. Katika telegram hiyo anaonesha kusikitika kwake kwa kuondokewa na Kardina huyo. Kwa njia hiyo anawatumia salam zarambi rambi kwa Mkuu wa shirika hili na Shirika zima la Wagostiniani, wanafamilia wake na wale ambao wamepata ushauri wa kiroho na kuongozwa na ushuhuda wake binafsi wa maisha ya kikristo na wakfu wake kama mfano wa kuigwa wa huduma yake ya mafunzo kwa vizazi vipya, hasa vya kikuhani.

Papa Francisko aidha katika kukumbuka kipindi kirefu cha maisha  na huduma yake aliyoitoa kama profesa kwenye vyuo vikuu mbalimbali vya Roma na kwingineko na kama pia kutoa huduma katika makao makuu Vatican anaamsha sala zake  juu kwa Bwana kwa ajili ya roho yake aweze kupokea roho yake katika  raha ya milele na kumpa amani. Kwa dhati anawatumia baraka ya kitume wote.

Kifo cha Kardinali Grech: Kardinali Prosper Grech amefariki dunia tarehe 30 Desemba 2019 katika Hospitali ya Santo Spirito, Sassia mjini Roma. Ni Kardinali ambaye hakuwa na sauti ya kupiga kura na hivyo kufuatia kifo hicho, Baraza la Makardinali linabaki na wajumbe 223 na kati yao 124 wa kupiga kura na 99 ambao hawana sauti ya kuchagua.

Kardinali Prosper Grech, alizaliwa  huko Birgu (Vittoriosa) katika kisiwa cha Malta kunako tarehe 24 Desemba 1925 na kubatizwa kwa jina la Stanley. Alibadilisha jina kuwa Prosper wakati alipojiunga kwenye shirika la wagostiniani. Amepata kushika nafasi mbali mbali na uongozi hasa kakama profesa na pia kama mmoja wa waanzilishi wa Taasisi ya Masomo ya Kitaalimungu na masomo ya Baba wa Kanisa Agostino Mjini Roma.

Amewahi kushika nafasi ya uhudumu katika Baraza la Kipapa la Mafundisho tanzu ya Kanisa wakati ule Rais alikuwa ni Josefu Ratizinger yaani Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI. Alichaguliwa kuwa Askofu Mkuu na tarehe 8 Februati 2012 akapewa wakfu wa kiaskofu katika Kanisa la Mtakatifu Yohane huko Malta. Na alitangazwa kuwa Kardinali tarehe 18 Februari 2012 na Papa Mstaafu Benedikto XVI.

Hata hivyo Baba Mtakatifu Francisko wakati hotuba yake Jumamosi  tarehe 16 Februari 2019 Katika ukumbi wa Clmentina Vatican kwa Maprofesa na wanafunzi wa Taasisi ya Masomo ya Baba wa Kanisa ya Mtakatifu Agostini Roma kati ya salam alimtaja mwanashirika mwenzao Kardinali Prospero Grech kama mmoja wa mwanzilishi wa Taasisi hiyo.

31 December 2019, 14:56