Baba Mtakatifu Francisko anasema, Noeli ni wakati muafaka wa ujenzi wa udugu wa kibinadamu, ukomavu wa imani na mshikamano wa upendo kwa maskini na wahitaji zaidi. Baba Mtakatifu Francisko anasema, Noeli ni wakati muafaka wa ujenzi wa udugu wa kibinadamu, ukomavu wa imani na mshikamano wa upendo kwa maskini na wahitaji zaidi. 

Papa Francisko: Noeli ni kipindi cha: Udugu, Imani na Mapendo!

Kwa wale wanaoishi mbali na wazazi wao ni wakati wa kurejea tena nyumbani ili kuungana na wazazi. Kwa upande mwingine, ni wakati kwa ndugu na jamaa kukutana na kusherehekea Noeli. Maadhimisho ya Sherehe ya Noeli ni muda muafaka kwa watu wote kujenga na kudumisha udugu wa kibinadamu; ukomavu wa imani na mshikamano wa upendo kwa maskini na wahitaji zaidi.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Jumapili tarehe 22 Desemba 2019 ametambua uwepo wa waamini, mahujaji na wageni kutoka ndani ya nje ya Italia. Kwa namna ya pekee, ametambua uwepo wa wawakilishi wa wananchi wanaoishi katika maeneo yenye uchafuzi mkubwa wa mazingira nyumba ya wote! Hawa ni wananchi wanaotamani kuishi katika mazingira bora zaidi sanjari na kulinda afya zao. Baba Mtakatifu amewakumbusha waamini kwamba, bado kitambo kidogo tu, waamini na watu wote wenye mapenzi mema wataadhimisha Sherehe ya Noeli kwa Mwaka 2019. Kwa wakati huu, mawazo yake ameyapeleka kwenye familia mbali mbali ambazo wakati huu wa Sherehe za Noeli na Mwaka Mpya, wanakutana. Kwa wale wanaoishi mbali na wazazi wao ni wakati wa kurejea tena nyumbani ili kuungana na wazazi.

Kwa upande mwingine, ni wakati kwa ndugu, jamaa na marafiki kukutana na kusherehekea Noeli. Maadhimisho ya Sherehe ya Noeli ni muda muafaka kwa watu wote kujenga na kudumisha udugu wa kibinadamu; ukomavu wa imani na mshikamano wa upendo kwa maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii. Mwishoni, mwa salam zake, Baba Mtakatifu anamwomba Mtakatifu Yosefu mtu wa haki, aweze kuwasindikiza katika hija hii ya maisha ya kiroho kuelekea katika maadhimisho ya Sherehe ya Noeli.  Bila shaka salam na matashi mema kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko yatawafikia hata wasikilizaji wetu kutoka Mkoani Kilimanjaro ambao kwa sasa wako njiani au tayari wamekwisha fika Kilimanjaro kwa ajili ya kusherehekea Siku kuu ya Noeli na Mwaka Mwaka Mpya wa 2020. Waambieni kwamba, Radio Vatican inawapa Big Up sana!

Papa: Noeli 2019
22 December 2019, 10:19