Vatican News
Baba Mtakatifu amekutana na wahamiaji na wakimbizi kutoka Lesbo waliofika hivi karibuni Roma na wakati huo huo kuzindua msalaba ulivikwa Jaketi la okoa ili kukumbuka wakimbizi! Baba Mtakatifu amekutana na wahamiaji na wakimbizi kutoka Lesbo waliofika hivi karibuni Roma na wakati huo huo kuzindua msalaba ulivikwa Jaketi la okoa ili kukumbuka wakimbizi!  (ANSA)

Papa Francisko:Ni lazima kuokoa wahamiaji maana Mungu atauliza!

Wakimbizi waliofika hivi karibuni mjini Roma kutoka Lesbo kwa njia ya michakato ya mikondo ya kibinadamu wamekutana na Papa.Ukosefu wa haki umesababisha wahamiaji wengi kuacha nchi zao, pia kuwasababisha wasukumwe na kufia baharini.sKuzuia Meli siyo sululu la matatizo amesema Baba Mtakatifu. Kinachotakiwa ni lazima jitihada za kufanya uamuzi wa kweli ili kuondoa makambi ya wafungwa huko Libia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kikundi cha wakimbizi 13 kutoka Lesbo waliofika mjini Roma hivi karibuni wamekutana na Baba Mtakatifu Francisko tarehe 19 Desemba 2019. Hawa ni wakimbizi wanoomba hifadhi ya kisiasa na kati yao kuna  hata vijana wadogo wenye umri wa miaka 14, wakiwemo hata baadhi ya waamini wakristo. Hata hivyo Baadaye Baba Mtakatifu Francisko amezindua msalaba mwangavu uliovikwa jaketi ya okoa katika maingilio ya Jumba la Kitume la Belvedere Vatican, ili kuweka kumbu kumbu ya wahamiaji na wakimbizi. Na kila mmoja ajue kuwa anahusika kuokoa maana siku ya mwisho Mungu atauliza hilo.

Shukrani kwa zawadi ya Jaketi 

Wakati wa hotuba yake Baba Mtakatifu Francisko ameanza kutoa shukrani kwa Jaketi  alilopewa zawadi  na kusema ni mara ya pili kupata zawadi kama  hiyo, kwani zawadi ya kwanza alipewa mwaka mmoja uliopita kutoka kwa kikundi cha waokoaji. Na hawa ameeleza  walikuwa ni kikundi cha ambacho kilileta Jaketi lililokuwa la mtoto wa kike aliyemezwa na maji katika bahari ya Kimediterranea. Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa baadaye Jaketi hilo aliwazawadia  tena Makatibu wawili wasaidizi wa kitengo cha wahamiaji  na wakimbizi cha Baraza la Kipapa la Huduma Fungamani ya Watu. Na wakati anawakabidhi aliwaambia kwamba: “Tazama huu ndiyo utume wenu!” katika ishara hiyo alitaka kuonesha maana ya pekee ya Kanisa ambalo liko mstari wa mbele katika kuokoa maisha ya wahamiaji na kuweza kuwapokea, kuwalinda, kuwahamasisha na kufungamanisha.

Jaketi la Pili alipewa pia na waokoaji

Jaketi la pili Baba Mtakatifu amesema amelikabidhi kwa kikundi cha wakoaji siku chache zilizopita ambalo lilikuwa la mhamiaji aliyekufa maji baharini mwezi Julai mwaka huu. Kwa maana hiyo hakuna anayejua alikuwa ni nani na alikuwa anatokea wapi. Kinachojulikana ni jaketi lilookotwa katika forodha ya bahari ya Kati ya Mediterranea kunako tarehe 3 Julai 2019, kwa wahusika wa kijografia 34*16.518 na 13*42.289. Baba Mtakatifu anasema kwamba ,“tuko mbele ya kifo kingine ambacho kinasababisha ukosefu wa haki. Huo ni ukosefu wa haki ambao unalazimisha wahamiaji wengi kuacha nchi zao. Ni ukosefu wa hali  nzuri inayowalazimisha kupitia jangwani  na kupata manyanaso ya vipigo masumbuko  kwenye vituo vya magereza ya wafungwa. Huo ni ukosefu wa haki  ambao inasukuma na kuwafanya wafe baharini.

Jaketi lililovika msalaba linaelezea uzoefu wa kiroho

Jaketi lililovika msalaba mwangavu  uliotiwa rangi unataka kueleza ule uzoefu wa kiroho ambao  alipewa  kutoka kwa maneno ya wakoaji. Katika Yesu Kristo msalaba ni kisima cha wokovu  na jambo la kipumbavu kwa walio kwenye mkumbo wa kupotea, lakini kwetu sisi tulio katika njia ya wokovu ujumbe huo ni nguvu ya Mungu (Rej, 1Cor 1:18). Katika utamaduni wa kikristo msalaba ni ishara ya mateso na sadaka, lakini hata ukombozi na wokovu.  Msalaba huu ni angavu,  amethibitisha Baba Mtakatifu na kuelendelea, kwa maana  hiyo unajikita kama changamoto ya kuwa makini sana na kutafuta daima ukweli. Msalaba ni mwanga angavu kwa sababu unataka kuimarisha imani katika ufufuko, ushindi  wa Kristo dhidi ya kifo. Hata wahamiaji wasiojulikana waliokuwa na matumaini katika maisha mapya wanashiriki ushindi huu. Baba Mtakatifu Francisko amesimulia kwamba, waokoaji walimsimulia ni kwa jinsi gani kila utume wao wanagundua uzuri wa kuwa wa pekee na ukuu wa familia ya kibandamu inayoungana katika udugu wa ulimwengu.

Maana ya jaketi la okoa katika msalaba

Baba Mtakatifu amependa kufafanua maana ya kuweka  Mtakatifu amsema jaketi hilo la okoa katika msalaba huo kwa  sababu ya kutaka kukumbuka kuwa ni lazima kubaki macho wazi… kuwa na moyo uliofunguka…na kwa ajili ya kukumbusha wito juu ya jitihada ya kuokoa kila maisha ya binadamu na kwamba ni wajibu kimaadili ambao inaunganisha waamini na wasio kuwa waamini. Ametoa tafakari kuwa: Je tunawezaje kusikiliza kilio cha wanaoangaika na  daima ambao wanaamua kukabiliana na bahari yadhoruba, badala ya kuendelea kufa pole pole katika makambi ya wafungwa huko Libia, sehemu za mateso na utumwa wa kiajabu. Je tunawezaji kubaki na sintofahamu mbele ya kisima cha manyanyaso na vurugu dhidi ya waathirika wasio kuwa na hatia na kuwaacha katika bidhaa ya biashara haramu bila moyo wa huruma? Tunawezaje kutambua yule anayepitia mbali  kama kuhani na mwandishi kwenye Injili kuhusu Msamaria mwema, ili kuweza kuwajibika kwa dhati juu ya kifo chao? Uvivu wetu ni dhambi! Baba Mtakatifu amethibitisha

Shukrani kwa wale wote wenye mapenzi mema ya kujikita kukabiliana na kuokoa

Baba Mtakatifu Francisko ametumia fura hii kuwashukuru wale wote ambao wameamua kutobaki na sintofahamu na kujikita kukimbilia ili kuokoa katika njia ya Yeriko bila kujiuliza maswali mengi, kwa nini maskini anakufa, au ameishia barabarani. Tendo la kuzuia Meli  siyo sululu la matatizo amesema Baba Mtakatifu. Kinachotakiwa ni lazima jitihada za kufanya uamuzi wa kweli ili kuondoa makambi ya wafungwa huko Libia na kutathimini kwa kutoa suluhisho linalowezekana! Ni lazima kushtaki na kufuatilia wahalifu wa biashara haramu na unyonyaji ambao wanatesa wahamiaji bila hofu yoyote  ya kuweza kutambuliwa  na wakati huo huohuo wakiwa na ubia ndani ya taasisi. Ni lazima kuweka pembezoni zile maslahi za kiuchumi kwa ajili ya kuweza kuweka kama kitovu cha mtu na watu,ambamo ni maisha na hadhi ya binadamu  yenye kuwa na thamani machoni pa mwenyezi Mungu. Ni lazima kukimbilia na kuokoa kwa sababu wote  tu wahusika wa maisha ya kila mmoja na siku ya hukumu ya mwisho Bwana yupo atauliza.

19 December 2019, 14:00