Vatican News
Baba Mtakatifu tarehe 19 Desemba amepokea barua za utambulisho wa mabalozi kutoka Seychelles, Mali, Andorra, Kenya, Lithuania na Niger Baba Mtakatifu tarehe 19 Desemba amepokea barua za utambulisho wa mabalozi kutoka Seychelles, Mali, Andorra, Kenya, Lithuania na Niger  (Vatican Media)

Papa Francisko:mchakato wa amani unaanzia na ufunguzi wa upatanisho!

Safari ya kuelekea amani inaanzia na ufunguzi wa mapatano.Na ndiyo sababu inatakiwa kuachana na tamaa za kupenda madaraka juu ya wengine ili kujifunza kuongozana kwa pamoja kama watu, kama watoto wa Mungu na kama ndugu.Ni katika hotuba ya Papa Francisko alipokutana mjini Vatican tarehe 19 Desemba 2019 na mabalozi wapya kutoka nchi ya Seychelles,Mali,Andorra,Kenya, Lithuania na Niger kwa fursa ya uwakilishi wa barua zao za utambulisho mjini Vatican.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko alhamisi tarehe  19 Desemba 2019 amekutana na mabalozi wapya kutoka nchi ya Seychelles, Mali, Andorra, Kenya, Lithuania na Niger kwa ajili ya fursa ya uwakilishi wa barua zao za utambulisho mjini Vatican wakiwa wanawakilisha nchi zao. Katika hotuba yake Baba Mtakatifu Francisko amewaribisha na kuwaomba waweze kumfikishia salam zake za dhati kwa Viongozi wakuu wao wa nchi pamoja na kuwahakikishia sala zake kwa ajili yao na kwa ajili ya wazalendo wao wote. Mkutano wao amaesema umewadia  wakati wa kipindi cha wakristo duniani koea wanajiandaa kusheherekea kuzaliwa kwa yule ambaye ni Mfalme wa Amani, anasema Baba Mtakatifu Francisko. Amani ni pumzi ya familia ya kibinadamu. Ni mchakato wa safari ya matumaini ambayo inajumuisha kati ya mengine majadiliano, mapatano na uongofu wa kiekolojia( Rej, Ujumbe wa Siku ya Amani duniani kwa mwaka 2020).

Migogoro ya kiraia,kikanda na kimataifa

Katika dunia ambayo inaonesha migogoro ya kiraia, kikanda na kimataifa, migawanyiko kijamii na ukosefu wa usawa ni muhimu kurudi katika majadiliano ya kujenga na ubunifu unaojikita juu ya uaminifu na juu ya ukweli kwa lengo la kuhamasisha kwa kiasi kikubwa ule mshikamano kindugu kati ya watu na ndani ya jumuiya ya kidunia.  Kwa upande wake Baba Mtakatifu amesema,  Kanisa katoliki lipiga mbio ya kushirikiana  na kila mwajibikaji aliye mshiriki katika kuhamasisha wema wa kila mtu na wa watu wote. Ni matarajio ya Baba Mtakatifu kwamba, utume  wao katika  kuchangia isiwe tu katika kudumisha mahusiano mema yaliyopo baina ya  nchi zao na Vatican, bali hata katika ujenzi wa dunia ili iweze kuwa ya haki zaidi na amani ambayo inatakiwa katika maisha ya binadamu, hadhi na haki viweheshimiwe na kuthamaniwa!

Safari ya kuelekea katika amani inaanzia na ufunguzi wa mapatano

Safari kuelekea amani inaanzia na ufunguzi wa mapatano amesisitiza Baba Mtakatifu Francisko. Kwani hii ni hatua ile hatua ya kuweza kuachana na tamaa za kupenda kutawale wengine na ili kujifunza kungozana pamoja na wote kama watu na kama watoto wa Mungu na kama ndugu( Rej, Ujumbe wa siku ya amani 2020,3). Ni kwa njia hiyo tu ya kuweza kuwekwa pembeni zile tofauti na hofu, kwamba, tunaweza kukua na kutumaini hali ya kweli  na uya kuheshimiana, amesisitiza Baba Mtakatifu. Lakini hata hivyo amesema hiyo kwa mara nyingie inapelekea kuwa na maendeleo ya utamadunia wa kuunganisha na mfumo wa kiuchumi wa hali na fursa mbalimbali za ushiriki wa maisha ya kijamii na kisiasa. Uwepo wao katika eneo hilo anasema kuwa ni ishara ya suluhisho la Nchi ambazo wanawakilisha na Jumuiya ya kimataifa katika ukuu wake wa kuweza kukabiliana na hali halisi z ukosefu wa haki, uhalifu, umasikini, ukosefu wa usawa ambao unasumbua sana dunia yetu na kuhatarisha matumaini na matarajio ya kizazi endelevu.

Amani inapata kizingiti hata kupitia ukosefu wa kuheshimu nyumba yetu ya pamoja

Baba Mtakatifu akiendelea na hotuba yake kwa mabalozi hawa wapya amebainisha kwamba, mara nyingi na daima tunaona kuwa amani inapata kizingiti hata kwa sababu ya ukosefu wa kuheshimu nyumba yetu ya pamoja  na kwa namna ya pekee kuonyonya rasilimali zake za asili ambazo zinaonekana tu kama kisima cha kutafuta faida ya haraka binafsi bila kufikiria gharama kubwa ambazo zinapelekea kwa ujumla  jumuiya mahalia na kwa ajili ya asili yenyewe! Dunia yetu inaendelea kukabiliana na msululu wa changamoto ngumu hasa kwa ajili ya utunzaji wa mazingira, anasema Baba Mtakatifu na kuongeza kuwa, si tu kwa ajili ya wakati uliopo lakini pia hata kwa ajili ya wakati endelevu. Sinpdi ya hivi karibuni ya Kanda ya Amazonia imetoa wito wa kupyaisha  ambao unastahili katika uhusiano kati ya Jumuiya na ardhi, kati ya wakati uliopo na uliopita, kati ya uzoefu na matumaini. Jitihada kwa ajili ya uendeshaji kiuwajibikaji katika ardhi na rasilimali zake ambazo ni dharurazinahitajika kwa wote na kwa ngazi zote, kutoka katika elimu ya familia hadi kufikia maisha ya kijamii na kiraia na  hadi kuweza kufikia maamuzi ya sera za kisiasa na kiuchumi.

Wema wa pamoja ndiyo msingi wa nyumbani tunamoishi

Wema wa pamoja ni ule wa nyumbani ambao tunaishi na tunahitaji jitihada za kushirikiana kwa ajili ya kuendelea kuchanua maisha na maendeleo fungamani ya kila mtu katika maisha ya familia ya kibinadamu. Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu Francisko amesema ikiwa ndiyo wanaanza utume wao katika mji wa Vatican, anawatakia matashi mema na kuwakikishia msada wake wake katika ofisi mbalimbali za Vatican ili kuwasaidia ufanishi wa uwajibikaji wao. Na kwa wate katika  familia zao, wahudumu wao na raia wao amewabariki kwa furana na amani  huku akiwatakia matashi mema ya sikukuu za Kuzaliwa kwa Bwana!

19 December 2019, 12:18