Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kuwatakia matashi mema ya Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana wafanyakazi wote wa Vatican Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kuwatakia matashi mema ya Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana wafanyakazi wote wa Vatican 

Papa Francisko:Katika Noeli tushangazwe na tabasamu la Mungu!

Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 21 Desemba amekutana na wafanyakazi wa Makao Makuu na Serikali ya Mji wa Vatican.Ni katika muktadha wa utamaduni wa kutakiana heri na baraka za Siku kuu ya Noeli.Wazo kuu:“ubora wa kazi unaambatana na ubora wa kuwa na uhusiano wa kibinadamu na hiyo ndiyo inayohitajika hata kwetu sisi”,Baba Mtakatifu amewakumbusha.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa hotuba yake Jumamosi tarehe 21 Desemba 2019 alipokutana na wafanyakazi wa Makao Makuu na Serikali ya Mji wa Vatican ametoa  matashi yake mema kwa ajili ya siku ya kuzaliwa kwa Bwana kwa kujikita katika tafakari ya  neno  ‘tabasamu’. Anamethibitisha kwamba ushauri huu ameupata kutokana na ziara yake ya mwisho aliyotembelea nchini ya Thailand mwezi uliopita. Nchi hiyo inajulikana kama ya tabasamu kwa sababu watu wake wanatabasamu sana na wanayo karama  maalum ya ukarimu unaojionesha katika nyuso zao, amesema Baba Mtakatifu Francisko. Na kwamba uzoefu huo ulimshangaza sana hadi kufikia kufikiria kwa jinsi gani tabasamu ni kielelezo cha upendo ambacho ni tabia ya kibinadamu. Kwa maana hiyo tunapo mtamzama mtoto mchanga aliyezaliwa, tunajikuta tunatabasamu na zaidi  mtoto mchanga akitambasamu, kwani  tunaonja hisia kubwa na iliyo rahisi. Na mara nyingi tunapenda kumbembeleza kwa kutumia kidole ili naye atabasamu. Mtoto huyo anajibu kwa mtazamo wetu, lakini tabasamu lake ni lenye nguvu sana, kwa sababu ni jipya na safi kama maji angavu ya kisima  na sisi kwa namna hiyo tunaamsha hisia  zetu za za utotoni. Baba Mtakatifu Francisko amesema hisia hizo na tabasamu, ndivyo vilivyo watokea kwa namna ya pekee  kati ya Maria, Yosefu na Yesu.

Tabasamu midomoni mwa Bikira Maria na Yosefu kwa sababu ya mtoto aliyezaliwa

Bikira Maria na mchumba wake kwa upendo wao, walifanya kuchanua tabasamu katika midomo ya mtoto aliyezaliwa. Kufuatia na kile kilichotokea, mioyoni mwao walijazwa na furaha mpya kutoka mbinguni.  Na nyota au hori la Bethlehemu iliangazwa. Yesu ni tabasamu la Mungu Baba Mtakatifu amesisitiza. Alikuja kujionesha ule upendo wa Baba wa Mbinguni. Wema wake na mtindo wake wa kwanza ambao aliufanya ndiyo tambasamu kwa wazazi wake na kama kwa kila mtoto anayezaliwa katika dunia hii. Kwa upande wa Bikira Maria na Mtakatifu Yosefu, ilikuwa ni imani yao kubwa ambayo walitambua kuupokea ujumbe na walitambua tabasamu la Yesu huruma ya Mungu kwa ajili yao na kwa wale wote waliokuwa wanasubiri kuja kwa Masiha, Mwana wa Mungu na Mfalme wa Israeli. Tazameni katika pango Baba Mtakatifu Francisko ameshauri kuwa, “hata sisi tunaweza kuishi uzoefu huo”.  Ni kwa kutazama Mtoto Yesu na kuhisi kuwa Mungu yupo pale anatabasamu na kutabasamu kwa maskini wote wa dunia hii na kwa wale wote ambao wanasubiri wokovu huku wakitegemea dunia iweze kuwa ya kidugu zaidi, mahali ambapo hakuna tena vita na vurugu, mahali mbamo kila mwanaume na mwanamke wanaishi kwa hadhi yao kama wana wa Mungu.

Vatican inahitaji upyaisho wa tabasamu la Mtoto Yesu

Baba Mtakatifu akiendelea na hotuba yake amesema “Hata Vatican, katika ofisi mbalimbali za Makao Makuu Matakatifu, daima wamekuwa wakihitaji upyaisho wa tabasamu la Mtoto Yesu. Hii ni kuruhusu uzuri wake usio na silaha uweze kusafisha taka taka ambazo mara nyingi huchafua mioyo yetu na hutuzuia kujikamilisha na kutoa ubora wetu binafsi. Ni ukweli, kazi ni kazi na kuna maeneo mengine ambayo kila mtu hujielezea kikamilifu na tajiri; Walakini, ni ukweli kwamba  katika sehemu za kazi tunaweza kuzitumia vizuri kila siku  na tuna hakika kuwa ubora wa kazi unaambatana na hali ya uhusiano wa binadamu na kwa maana hiyo ndiyo  mtindo wa maisha. Hiyo inahusu hasa sisi ambao tunafanya kazi katika huduma ya Kanisa kwa jina la Kristo” Baba Mtakatifu amewakumbusha.  Vile vile  amebainisha ni kwa jinsi gani anatambua ilivyo vigumu kutabasamu kwa sababu nyingi. Lakini kwa njia hii tunahitaji tabasamu la Mungu na kwa Yesu ambaye anaweza kutusaidia. Ni yeye peke yake Mwokozi ambaye mara nyingi tunafanya uzoefu wa dhati katika maisha yetu. Mara nyingine mambo yanakwenda vizuri na kumbe pale kuna hatari ya kuhisi kuwa na uhakika na kusahau wengine walio na ugumu. Kwa maana hiyo kuna haja ya tabasamu la Mungu ambaye anatuvua ule uhakika wa uongo na kutupeleka katika radha ya urahisi na wa kutoa bure.

Ni katika Liturujia na kutafakari pango tunaweza kushangazwa na tabasamu la Mungu

Katika kubadilishana matashi mema ya sikukuu, basi ni kwa kushiriki Liturujia, hata kutafakari pango, ili tuacha tushangazwe na tabasamu la Mungu ambaye katika Yesu alikuja kulileta, amesema Baba Mtakatifu Francisko. Kama Maria, kama Yosefu na wachungaji wa Bethlehemu, tumpokee, tuache tusafishwe na kutakaswa na tutaweza hata sisi kulipeleka tabasamu rahisi  kwa wengine katika unyenyekevu. Amehitimisha kwa kuwashukuru wote na kuwaomba waweze kuwapelekea hata wapendwa wao nyumbani, hasa wagonjwa na wazee zaidi matashi mema ya tabasamu  ili waweze nao kuhisi faraja la tabasamu hilo. Kutabasamu ni kubembeleza; dhiki na moyo, mashaka na roho. Na tubaki pamoja katika maombi. Ninawatakia Sikukuu njema ya Kuzaliwa kwa Bwana!

21 December 2019, 13:14