Tarehe 15 Desemba katika Dominika ya tatu ya Majilio, Baba Mtakatifu Francisko ameathimisha Misa takatifu kwa Jumuiya ya wafilippini wanaoishi Roma wakiwa wanaanza Novena ya Kuzaliwa kwa Bwana Tarehe 15 Desemba katika Dominika ya tatu ya Majilio, Baba Mtakatifu Francisko ameathimisha Misa takatifu kwa Jumuiya ya wafilippini wanaoishi Roma wakiwa wanaanza Novena ya Kuzaliwa kwa Bwana  

Baba Mtakatifu Francisko:wokovu ni zawadi inayotolewa kwa wote!

Wokovu ni zawadi iliyotolewa kwa wote lakini Bwana anaonesha huruma yake maalum kwa walioathirika zaidi,wadhaifu zaidi,na watu wake masikini zaidi. Kiitikio cha Zaburi kinaonesha waathirika wengine wana0stahili kuwa na mtazamo wa upendo maalum kwa upande wa Mungu Na hao ni wale wanaolemewa,wenye njaa, wafungwa, wageni, yatima na wajane.Ni maneno kutoka mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko katika misa ya Jumuiya ya Wafilippini wanaoishi Roma.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tunaadhimisha leo hii Dominika ya tatu ya Kipindi cha Majilio. Katika somo la  Nabii Isaya anaalika dunia nzima kufurahia kwa ajili ya kuja kwa Bwana, anayeleta wokovu kwa watu wake. Yeye anakuja kufungua macho vipofu na masikio viziwi, kuwaponya viwete na bubu ( Is 35,5-6). Wokovu ni zawadi iliyotolewa kwa wote lakini Bwana anaonesha huruma yake maalum kwa walioathirika zaidi, wadhaifu zaidi na watu wake masikini zaidi. Kiitikio cha Zaburi kinaonesha waathirika wengine ambao wanastahili kuwa na mtazamo wa upendo maalum kwa upande wa Mungu. Na hao ni walioelemewa, wenye njaa, wafungwa, wageni, yatima na wajane ( Za145,7-9). Ni wakazi wanaoishi pembezoni mwa maisha ya jamii  kama ilivyokuwa jana na leo hii, amebainisha Baba Mtakatifu Francisko.

Novena kwa ajili ya kujiandalia na Sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana

Huo ndiyo mwanzo wa mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Dominika tarehe 15 Desemba kwa Jumuiya nzima ya wafilippini wanaoishi Roma, ikiwa ni mwanzo wa utamaduni wao wa kusali Novena kwa siku tisa kwa ajili ya maandalizi ya sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana. Baba Mtakatifu akiendelea na mahubiri yake amesema, “Katika Yesu Kristo upendo wa wokovu wa Mungu unafumbatika kwa maana  “vipofu wanapata kuona, viwete wanatambea, wakoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuka, na masikini wanatangaziwa Injili” (Mt 11,5). Hizi ndizo ishara zinazo sindikiza utimilifu wa Ufalme wa Mungu. Haupigi kinubi au ushindi wa kijeshi, hakuna hukumu au laana kwa wadhambi, badala yake ni uhuru dhidi ya mabaya na kutunza huruma na amani. Hata mwaka huu, Baba Mtakatitu Francisko amebainisha kwamba, “ tunajianda kwa mara nyingine tena kuadhimisha fumbo la Mungu kutwaa mwili, Emanueli, Mungu pamoja nasi anaye tenda maajabu kwa ajili ya watu wake, kwa namna ya pekee walio wadogo zaidi na wadhaifu. Maajabu hayo ndiyo ishara ya uwepo wa Ufalme wake. Na kama wakazi wa maisha ya pembezoni wanaondelea kuwa wengi ni lazima kuomba Bwana ili aweze kupyaisha miujiza ya Kuzaliwa kwa Bwana kila mwaka, huku akitufanya sisi sote kuwa kama chombo cha upendo wake wa huruma kwa walio wa mwisho.

Katika kujiandaa kwenye kipindi cha neema Kanisa linatoa fursa ya kuwa na majilio

Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa, ili kuweza kujiandaa vema katika neema ii iliyoenea, Kanisa linatoa kupindi cha Majilio ambapo wote wanaalikwa kukesha katika mioyo yao ili kusubiri na kuongeza sala zetu kwa kina. Katika mtazamo na lengo hilo, katika utajiri wa tamaduni tofauti ,Makanisa maalum wameanzisha mambo mengi ya ibada ya kufanya. Kwa mfano katika nchi ya Ufilippini, tangu kale kumekuwapo na novena ya kujiandalia na Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana inayoitwa Simbang-Gabi maana yake (Misa ya usiku). Kwa siku tisa mfululizo, waamini wa Ufilippini wanakusanyika pamoja kila alfajiri na mapema katika maparokia yao ili kuadhimisha misa ya Ekaristi takatifu. Kwa miaka kumi ya mwisho, Baraka ya wahamiaji wa ufilippini imezidi kuvusha ibada hiyo katika  mipaka ya kitaifa na kuingiza katika nchi nyingi.  Na kwa miaka sasa wanaadhimisha Simbang-Gabi hata katika Jimbo la Roma na ambapo leo hii tunaaadhimisha pamoja katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro”.

Tunaalikwa kuwa chachu katika jamii ambayo haiwezi kuona tena uzuri wa Mungu

Baba Mtakatifu Franciskokwa kusisitiza zaid  amesema kuwa kwa njia ya maadhimisho hayo tunataka kujiandalia Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana kwa mujibu wa Roho ya Neno la Mungu ambalo limesikika, kwa kubaki kidete hadi kuja kwa Bwana siku ya mwisho kama anavyo bainisha Mtume Yakobo (Yak 5,7). Aidha tunapaswa kujibidisha ili kuonesha upendo na huruma ya Mungu kwa wote hasa kwa walio wa mwisho. Tunaalikwa kuwa chachu katika jamii ambayo mara nyingi haiwezi tena kuonja uzuri wa Mungu na kufanya uzoefu wa neema ya uwepo wake. Aidha Baba Mtakatifu Francisko anatambua kuwa waamini hao wameaacha nchi zao kwa ajili ya kutafuta hali bora ya maisha na hivyo anasema wanao utume maalum. Imani yao iwe “chachu” katika jumuiya ya kiparokia mahalia ambapo wao wanatoka leo hii.

Waongeze nguvu mara dufu kukutana na kushirikishana utajiri wa utamaduni wao

Baba Mtakatifu Francisko amewatia moyo ili kuongeza nguvu mara dufu ya kukutana na kushirikishana utajiri wao wa utamaduni na kuacha wakati huo huo kutajirishwa na uzoefu wa wengine. Kwa wote wanaalikwa kujenga kwa pamoja jumuiya katika utofauti ambao ndiyo unaangaza moja kwa moja Ufalme wa Mungu uliotabiriwa na Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliyejifanya mtu. Wanaalikwa wote kufanya matendo ya upendo kwa ajili ya wakazi wa pembezoni mwa maisha na kujikita katika huduma ya zawadi tofauti kwa namna ya kupyaisha ishara za uwepo wa ufalme wa Mungu. Wote wanaalikwa kutangaza kwa pamoja Injili, ambayo ni Habari Njema ya wokovu kwa lugha zote  na ili kuweza kuwafikia watu wote iwezekanavyo. Kwa kuhitimisha amsema “Mtoto Mtakatifu ambaye tunajiandaa kumwambudu aliyevikwa kimasikini na kulala holini awabariki na kuwapatia nguvu ya kupeleka mbele furaha ya ushuhuda”. Na mara baada ya Baraka Takatifu Baba Mtakatifu Francisko ametoa salam kwa jumuiya nzima ya Wafilippini kwa maneno haya “Na endeleni kuwa wapenyezi wa imani. Asante”

16 December 2019, 09:42