Vatican News
Jioni tarehe 31.12 .2019 Baba Mtakatifu Francisko ameongoza masifu ya jioni na sala ya Kushukuru "Te Deum" katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Jioni tarehe 31.12 .2019 Baba Mtakatifu Francisko ameongoza masifu ya jioni na sala ya Kushukuru "Te Deum" katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro  

Mungu alisimika hema lake na hajawahi kwenda mbali!

Maneno na ishara za wokovu alizotimiza katika mji zinatoa mshangao na shauku ya wakati huo,lakini hawakutambua maana kamili.Ni kwa kipindi kifupi tu hawatakumbuka wakati ule mkuu wa kirumi atakapo wauliza:“mnataka niwaachie Yesu au Barabba?”.Nje ya mji Yesu anasulibiwa juu ya Golgota ili kuhukumiwa na mtazamo wa wakazi na kumdhiaki sana kwa maneno.Ni katika tafakari ya Papa katika masifu ya kufunga mwaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro Vatican

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Lakini wakati ule maalum ulipotimia Mungu alimtuma mwanae aliyezaliwa na mwanamke akaishi chini ya sheria (Gal 4,4). Mwana aliyetumwa na Baba alisimika hema huko Betlehemu kama asemavyo: "wewe, Bethlehemu ya Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; (MI 5,1) Aliishi Nazareth kama mzalendo ambaye hakutajwa katika maandiko kama siyo kusema kuwa “laweza neno jema kutoka Nazareti? ( Yh 1,46). Aliyesulibiwa nje ya kuta zake. Uamuzi wa Mungu huko wazi kwa kuonesha upendo ambao yeye anachagua mji mdogo na mji ambao unadharauliwa na anapofika Yerusalemu anaungana na wadhambi na waliobaguliwa. Hakuna mkazi wa mji alitambua kuwa Mwana Mungu alijifanya mtu na yupo anatembea katika njia zake, labda hata kwa wafuasi wake ambao hawakutambua kikamilifu  hadi kufikia utufuko wa fumbo lililokuwa ndani ya Yesu. Ndiyo mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa sala ya masifu na shukurani kwa Mungu ( Te deum) ya kufunga mwaka jioni tarehe 31 Desemba 2019 katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro.

Ishara na wokovu vinashangaza

Papa Francisko akiendelea anasema maneno na ishara za wokovu alizotimiza katika mji zinatoa mshangao na shauku ya wakati huo, lakini hawakutambua maana kamili. Ni kwa kipindi kifupi tu hawatakumbuka wakati ule  mkuu wa kirumi atakapo wauliza: “mnataka niwaachie Yesu au Barabba?”. na hivyo ni  nje ya mji Yesu anasulibiwa, juu ya Golgota ili kuhukumiwa na mtazamo wa wakazi na kumdhiaki sana kwa maneno. Lakini ni hapo hapo msalabani, katika mti mpya wa maisha, nguvu ya Mungu itawavutia kwake wote. Hata Mama wa Mungu chini ya msalaba akiwa na uchungu ukitanda kwa waamini wote wa tumbo lake la umama. Mama wa Mungu ni Mama wa Kanisa,na huruma ya kimama inawafikia watu wote. Katika mwana wa Mungu alisimika hema lake… na hapo hajawahi kwenda mbali!  Uwepo wake katika mji, hata katika mji wetu wa Roma “kamwe hasitengenezwe, bali agunduliwe na kuoneshwa” ( Wosia wa evangelii gaudium, 71).

Sisi tunapaswa kuomba neema ya kuwa na macho mapya

Ni sisi ambao tunapaswa kuomba neema ya kuwa na macho mapya, anasisitiza Papa  yenye uwezo wa kuwa na  mtazamo mpya, ukiwa ni mtamzamo wa imani ambayo inagundua Mungu anayeishi katika nyumba zake, katika njia zake na katika viwanja vyake( Evagelii gaudium, 71). Manabii katika Maandiko, wanaonya juu ya kishawishi cha kufikiria uwepo wa Mungu hekaluni tu, ( Mw 7,4): na kumbe Yeye anaishi katikati ya Watu wake, anatembea na wao na kuishi maisha yake. Imani yake ni  thabiti ni ya ukaribu wa maisha ya kila siku ya watoto wake. Na zaidi Mungu anapotaka kufanya mambo mapya kwa njia yake kamwe aanzii katika hekalu, bali katika umbu kwa njia ya mwanamke aliye mdogo na maskini wa watu wake.

Uchaguzi wa Mungu ni maalum

Uchaguzi wa Mungu ni maalum sana! Habadilishi historia kwa njia ya watu wenye nguvu, au wa taasisi za kiraia na kidini bali anaanzia na mwanamke wa pembezoni mwa ufalme kama vile Maria na kwa walio tasa kama vile Elizabeth. Katika Zaburi ya 147 iliyosmowa, Papa amesema, mzaburi anawaalika Yerusalemu  kusifu Mungu kwa sababu Yeye anatuma duniani Neno lake, ujumbe wake kwa haraka. Kwa njia ya Roho wake Mtakatifu, anayetangaza kwa kila moyo wa binadamu Neno lake, Mungu anawabariki wana wake na kuwatia moyo wafanye kazi kwa ajili ya amani katika mji.

Jitihada za Roma katika kuhamasisha udugu na mshikamano

Papa Francisko anawaalika jioni  hiyo kuamsha mtazamo wao juu ya mji wa Roma ili uweze kupokea na kutazama hali halisi ya wema ambayo inatendeka kila siku na jitihada za nguvu  na majitoleo katika kuhamasisha udugu na mshikamano. Hata hivyo Papa anabainisha kwamba Roma siyo mji peke yake ulio mgumu na wenye matatizo yake mengi, kama vile hukosefu wa usawa, ufisadi na mivutano ya kijamii. Roma ni mji ambao Mungu anatuma Neno lake ambalo linakita kwa njia ya Roho Mtakatifu katika mioyo ya wakazi na kusukuma waweze kuamini na kutumainia, licha ya hayo yote na kupenda kupambana kwa ajili ya wema wa wote.

Ujasiri wa waamni na wasio waamini 

Papa Francisko amekumbuka watu jasiri, waamini na wasio waamini ambao amekutana nao  kwa miaka hii na ambao wanawakilisha mioyo inayodunda ya Roma. Kwa hakika Mungu hajawahi kuacha kubadilisha historia na uso wa mji wetu kwa njia ya watoto wadogo na masikini ambao wanaishi. Yeye anachagua wao na kuwahimiza, anawawapa ari ya kujikita katika matendo na kuwafanya wawe na mshikamano; anawasumawatoto wake wawe na ari  ya kuunda mitandao na kujenga uhusiano wa fadhila na kujenga madaraja na siyo kuta. Kwa hakika ni kwa njia ya mito hii elfu ya maji hai ya Roho ambayo Neno la Mungu linatoa matunda katika  miji na kuwa “mama anayefurahi wa watoto. ( Zan 113,9)

Bwana anaomba nini katika Kanisa la Roma

Papa Francisko anatoa swali. Je Bwana anaomba nini Kanisa la Roma?  Yeye anaikabidhi Neno lake na kuisukuma ili  kujitupa katika mchanganyiko na kujihusisha kwenye makutano na katika uhusiano na wakazi wa mji, ili ujumbe wake uweze kukimbia kwa haraka”. Papa Francisko amesema kuwa wote wanaalikwa kukutana na wengine na kujiweka katika usikivu wa kuishi kwao na kilio cha mahitaji yao. Usikivu ni tendo la upendo! Kuwa na muda kwa ajili ya wengine, kujadiliana, kutambua kwa njia ya mtazamo wa tafakari ya uwepo na matendo ya Mungu katika maisha yao, kushuhudia, kwa matendo zaidi ya maneno ya maisha mapya ya Injili. Kwa hakika ni huduma ya upendo ambayo inabadilisha hali halisi. Kwa kufanya hivyo katika mji na hata katika Kanisa, inaweza kuzunguka hali mpya ya kuhisi kujikita kwa upya katika mwendo na kuweza kushinda mantiki za zamani za upinzaji na kupima, ili kuweza kushirikiana kwa pamoja na kujenga jiji la haki na la kidugu. Hatupaswi kuogopa au kuhisi hatuwezi kwa ajili ya utume muhimu kama huu, amehimiza Papa Francisko. Na hatimaye anasema:  "Tukumbuke: Mungu hachagui kwa sababu ya “ustadi” wetu, lakini hasa ni kwa sababu sisi tunahisi udogo. Tumshukuru kwa neema yake ambayo ametutegemeza katika mwaka huu na kwa shangwe tuinue kwake wimbo wa sifa".

31 December 2019, 18:31