Tafuta

Vatican News
Tarehe 20 Desemba 2019 Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Guterres mjini Vatican Tarehe 20 Desemba 2019 Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Guterres mjini Vatican   (Vatican Media)

Tusikilize sauti za vijana wanaotusaidia kujiuliza nafsini mwetu!

Tarehe 20 Desmba 2019 Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Guterres.Mwisho wa mazungumzo yao wametoa ujumbe wa pamoja kwa njia ya video!

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 20 Desemba 2019 katika Jumba la Kitume mjini Vatican amekutana na Katibu wa Umoja wa mataifa Bwana Antonio Guterres na baada ya mkutano wao akakutana na na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican. Katika mkutano wao ni kama wa utamaduni wa mapapa naMakatibu wakuu wa Umoja wa Mataifa ambao wamekaa kwa mika mingi na zaidi hasa mkutano huu ukiwa katika matazamio ya maadhimisho ya miaka 75 ya Umoja wa Mataifa.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na makatibu wa Vatican 

Wakati wa mazungumzo yao  Katibu Mkuu na makatibu wa Vatican wameelezea na kutazama Vatican juhudi zake na Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya kufuatilia amani duniani. Vile vile mtazamoo wao ulikuwa ni kuhusu mchakato wa hali halis ya sasa ya kuweza kufikia Malengo endelevu na juu ya kipeo cha mataifa, kwa namna ya pekee kuonesha matatizokwa dhati ya uendeshaji kulingana na matatizo ya sasa ambayo yanatazama sana uhamiaji, biashara haramu ya watu, mabadiliko ya tabia nchi na kusitishwa kwa silaha. Vile vile wametazama hata baadhi ya hali halisi za migogoro, ukosefu wa msimamo kijamii na dharur mbaya za kibinadamu.

Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa njia ya video

Hata hivyo mara baada ya mazungumzo ya Baba Mtakatifu Francisko na Katibu Mkuu Bwana Guterres, wotrewawili wameweza kutoa ujumbe wapo wa pamoja kwa njia ya video unaosema kuwa: Ni vizuri mkutano huu unawadia katika siku ambazo zinakaribia Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana. Umefikia wakati wa mtazamo wetu unaangalia juu mbinguni kwa ajili ya kumkabidhi Mungu watu na hali halisi zilizopo ndani ya kina cha moyo. Ni katika mtazamo huo tunajitambua kuwa ni wana wa Baba mmoja na ndugu. Huo ndiyo  mwanzo wa maneno ya Baba Mtakatifu wakati wa kutoa pamoja kwa njia ya Video na Bwana Antonio Gueterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mara baada ya kufanya mkutano wao na Baba Mtakatifu. Ujumbe wao ameendelea kusema kuwa tumshukuru Mungu kwa mema mengi yaliyomo duniani, kwa ajili ya jitihada ambazo zinatolewa bure na kwa wale ambao wanatumia nafasi na nguvu zao za maisha katika kutoa huduma, kwa yule ambaye hakatii tamaa na kujenga mshikamano zaidi wa kibinadamu na wa haki zaidi. Tunatambua ya kwamba hatuwezi kujiokoa wenyewe!

Tusigeukie upande mwingine mbele ya ukosefu wa usawa, njaa na  umaskini 

Hatuwezi na hatupaswi kugeukia sehemu nyingine mbele ya ukosefu wa hali halisi ya usawa, mbele ya kashfa ya njaa duniani, umaskini, watoto wanaokufa kwa sababu hawana maji, chakula na matibabu ya lazima. Hatuwezi kugeukia upande mwingine wowote mbele ya kila aina  ya manyanyaso dhdi ya watoto wadogo. Tunapaswa wote kupambana na janga hili. Hatuwezi kufunga macho mbele ya ndugu zetu wengi ambao kwa sababu ya migogoro ya vurugu, njaa au mabadiliko ya tabianchi, wanaacha nchi zao na wanakwenda wakati  mara nyingi kukutana na hali halisi mbaya ya maisha. Hatupaswi kubaki na sintofahamu mbele ya hadhi ya kibinadamu inayokanyagwa na kunyonywa, mashambulizi dhidi ya maisha ya binadamu, yawe ya yule ambaye hajazaliwa  na kama ya yule mtu mwenye kuhitaji matibabu.

Tusigeukie upande mwingine wakati waamni wa imani nyingi wanateswa

Hatuwezi na hatupaswi kugeukia upande mwingine wakati waamini wa imani nyingi wanateswa katika sehemu mbalimbali za dunia. Kilio cha kulipiza kisasi mbele ya  Mungu kinasika dhidi ya kutumia dini ili kuchochea chuki, vurugu, kusongwa, itikadi kali na ushupavu kipofu, hadi kufikia kulazimisha watu wakimbie makwao na kuhahama. Lakini anapaza sauti kwa kisasi ya Mungu hata dhidi ya mbio za utengenezaji wa silaha na utengenezaji wa  nyuklia. Na siyo tu maadili ya utumiaji hata kumiliki silaha za kinyuklia ambazo zinapelekea uharibifu, hata kuleta hatari ya ajali inayowakilisha wasiwasi na  kutaharisha ubinadamu.

Tusibaki na sintofahamu mbele ya idadi nyingi za vita

Tusibaki na sintofahamu mbele ya idadi nyingi za vita ambavyo vinaendelea na mapigano na kuwakumba wengi wasio kuwa na hatia. Imani katika majadiliano kati ya watu na mataifana katika lugha nyingi, katika nafasi za mashirika ya kimataifa, katika diplomasia ni kama chombo  cha uelewa na kuwa na umuhimu kwa ajili ya ujenzi wa dunia yenye amani. Tunajitambua kuwa wajumbe  pekee wa ubinadamu na kujitambua kutunza nyumba yetu ambayo kizazi baada ya kizazi, tulikuwabidhiwa na Mungu ili kuilinda na ili kutunza na kuweza kuicha katika urithi wa watoto wetu.Jitihada za kupunguza hewa chafu na kwa ajili ya kuwa na ekolojia fungamani ni dhaurura na lazima tufanya lolote mapema kabla ya kuchelewa!

Tusikilize sauti ya vijana wengi ambao wanatusaidia kujiuliza ndani ya nafsi zetu

Tusikilize sauti ya vijana wengi ambao wanatusaidia kujiuliza na  ndani ya dhamiri zetu kwa kile ambacho kinaendelea kutokea leo hii katika dunia na wanaoomba ili waweze kuwa wapanzi wa amani na wajenzi pamoja lakini  siyo kuwa wao peke yao katika ustaarabu wa kibinadamu zaidi na wa haki zaidi. Siku ya Kuzaliwa kwa Bwana, katika urahisi wake, inatukumbusha ambacho ni muhimu sana katika maisha ya kwamba ni upendo.

20 December 2019, 14:09