Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wawakilishi wa Chama cha Vijana Katoliki Italia Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wawakilishi wa Chama cha Vijana Katoliki Italia 

Baba Mtakatifu Francisko:Safari ya mafunzo inawasaidia kuwa na unyofu wa dhimiri ya utume!

Katika siku ya Kuzaliwa kwa Bwana,jiunde katika sala na wakati huo huo kuwa na mshangao wa wachungaji,huku wakimtazama Mtoto Yesu ambaye amekuja dunia ili kuleta upendo wa Mungu anayefanya mambo yote kuwa mapya.Kuzaliwa kwa Yesu kumewezesha kuwa na daraja kati ya Mungu na watu,amepatanisha ardhi na mbingu.Ni maneno ya hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko wa wakilishi wa Chama cha Vijana katoliki Italia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Daima ni vizuri kuwapokea katika fursa ya Sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana. Ninawasalimia kwa upendo na kuwaomba ili kuwafikishia salam na matashi mema ya Sikukuu hii kwa vijana wenzenu wa Chama Katoliki ambao mnawawakilisha. Salam kwa Askofu Gualtiero Sigsmondo na Profesa Matteo Truffelli msimamizi wa Kitaifa na wakuu wengine ambao wanaowasindikiza. Ndiyo mwanzo wa hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu tarehe 16 Desemba 2019 alipokutana na vijana wa chama Katoliki cha Italia katika fursa ya kutakiana matashi mema ya Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana inayokaribia.

Mpango wa mafunzo kwa hakika katika safari yao unawasaidia kuwa na dhamiri ya wito wao kama mitume wamisionari

Akiendelea na hotuba yake, Baba Mtakatifu Francisko amesema, "Ninawashukuru kunitembelea  na ninawatakia heri na zaidi katika sala. Ni matarajio yangu kwamba Mwokozi anaweza kuwajaza furaha ambayo leo hii ninaitazama katika nyuso zenu". Baba Mtakatifu ameonesha kupendezw kwa chama hiki kutokana na jitihada zao ambazo kwa mwaka huu wamezionesha na hasa wakiwa wanaadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Chama ha vijana wadogo Katoliki nchini  Italia. Mpango wao wa mafunzo kwa hakika katika safari yao unawasaidia kuwa na dhamiri nyoofu ya wito wao kama mitume wamisionari. Na pia ni furaha ya Baba Mtakatifu Francisko ya kwamba vijana hao wameweza kufanya uzoefu wa mkutano waliouita “ vijana  katika Sinodi”. “Itakuwa ni vizuri sana kutambua kuwa kile kitakachotokea katika mkutano huo ni tunda la mawazo yao na mapendekezo yao.

Kazi ya kufanya wakati wa Sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana

Baba Mtakatifu Francisko aidha amependa kuwapa kazi ya kufanya nyumbani. Katika siku ya Kuzaliwa kwa Bwana, wajiundie katika sala na wakati huo huo wawe na   mshangao wa wachungaji, huku wakimtazama Mtoto Yesu ambaye amekuja dunia ili kuleta upendo wa Mungu anayefanya mambo yote kuwa mapya. Kuzaliwa kwa Yesu amesema Baba Mtakatifu  kumewezesha kuwa na daraja kati ya Mungu na watu, amepatanisha ardhi na mbingu, ameunganisha ubinadamu wote mzima. Leo hii Yeye anataka hata vijana wenyewe wawe madaraja madogo mahali ambapo wanaishi. Hata hivyo Baba Mtakatifu Francisko ameuliza swali: "je wao  tayari wanatambua kuwa daima kuna haja ya kujenga madaraja, Siyo kweli ?..... wamjibu ndiyo madaraja na siyo kuta. Na leo ninaomba hata ninyi muwe madaraja madogo mahali ambapo mnaishi! Tayari mnatambua hilo.Tayari mnatambua kuwa ni lazima hilo. Mara nyingi siyo rahisi amebainisha Baba Mtakatifu Francisko lakini iwapo tumeungana na Yesu tunaweza kufanya hivyo”

Mama Maria awasinidikiza katika safari

Baba Mtakatifu Francisko kwa kuhitimisha amesema "Ninamwomba Maria Mama wa Yesu na mama yetu awasindikize katika safari yenu. Kumbukeni kujifunza kutoka kwake nini maana ya kusema Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana. Yeye na Mtakatifu Yosefu wanaweza kutufundisha kweli namna ya kumpokea Yesu na namna ya kumwambudu na jinsi gani ya kumfuasa kila siku. Baba Mtakatifu Francisko amewabariki kwa Baraka takatifu na kuwaomba pia wasisahau kusali kwa ajili yake.

16 December 2019, 14:40