Tafuta

Vatican News
Wakati wa tafakari ya Baba Mtakatifu tarehe 1 Novemba 2019 anasema,waliotutangulia wapo mbele ya kiti cha enzi wakisifu Mungu na kuimba utukufu wake Wakati wa tafakari ya Baba Mtakatifu tarehe 1 Novemba 2019 anasema,waliotutangulia wapo mbele ya kiti cha enzi wakisifu Mungu na kuimba utukufu wake  (ANSA)

Baba Mtakatifu:Watakatifu wengi wako milango ya jirani zetu!

Katika Sikukuu ya Watakatifu Wote,Baba Mtakatifu Francisko wakati wa tafakari yake kabla ya sala ya Malaika wa Bwana amekumbuka mashuhuda wengi na ambao anathibitisha kwamba wanaishi karibu na sisi na ndiyo kioo cha uwepo wa Mungu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kila ifikapo tarehe Mosi Novemba ni sikukuu ya watakatifu wote, ambapo Mama Kanisa anafanya kumbu kumbu ya marehemu wote waliotutangulia na ambao wapo mbele ya kiti cha enzi huku wakisifu Mungu na kuimba utukufu wake. Kwa maana hiyo  Baba Mtakatifu Fransisko kabla ya kusali Sala ya Malaika wa Bwana kwa mahujaji na waamini waliofika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro ametoa tafakari yake na kusema kuwa, Sikukuu ya watakatifu wote inatukumbusha kuwa tunaalikwa  wote katika  utakatifu. Watakatifu wa kila nyakati na ambao wanaadhimishwa leo hii, kwa pamoja, siyo ishara rahisi tu ya ubinadamu ambao huko mbali na ambao hauwezi kufikiwa. Kinyume chake ni watu walioishi wakiwa wamesisimama na  miguu yao ardhini; walifanya uzoefu wa ugumu wa kila siku, katika maisha yenye mafanikio hata kushindwa na hatimaye wakapata nguvu kutoka kwa Bwana na daima wakiamka na kuendelea na safari. Kitu ambacho unaweza kutambua ni kwamba maisha ya utakatifu ndiyo mtazamo japokuwa hauwezi kuendelea kwa njia ya nguvu binafsi, bali ni tunda la Mungu na jibu letu katika uhuru kuhusu hilo. Kwa maana hiyo utakatifu ni zawadi na wito.

Utakatifu ni neema na zawadi ya Mungu

Kwakuwa ni neema ya Mungu yaani zawadi yake, Baba Mtakatifu Francisko amesema ni jambo ambalo hatuwezi kulinunua au kubadilishana, bali kupokea kwa kushiriki kwa namna hiyo ya maisha ya Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu anayeishi ndani mwetu, tangu ubatizo wetu.  Hii ni inahusu kukomaaa daima zaidi katika utambuzi kuwa sisi tunaungana katika Kristo, kama mzabibu na matawi yake na kwa maana hiyo tunaweza na lazima kuishi na Yeye na katika Yeye kama watoto wa Mungu. Mbegu ya utakatifu ni ubatizo wenyewe! Kwa maana hiyo utakatifu ni kuishi kikamilifu  na muungano na Mungu wakati wa hija hii duniani.

Licha ya utakatifu kuwa zawadi pia ni wito

Baba Mtakatifu akiendelea na sehemu ya pili kuhusu utakatifu amesema licha ya utakatifu kuwa zawadi, pia ni wito. Na huu ni wito wa pamoja wa wafuasi wa Kristo, ni njia ya utimilifu ambayo kila mkristo anaalikwa kupitia kwa imani kuu, kuelekea hatima ya mwisho, yaani ya muungano kamili wa mwisho na Mungu katika maisha ya milele. Utakatifu kwa maana hiyo unageuka kuwa jibu la zawadi ya Mungu, kwa sababu unajionesha hasa katika kuwajibika. Kwa mtazamo huo ni muhimu  kuwa na wajibu kwa dhati na jitihada za kila siku kwa ajili ya utakatifu katika hali zote za maisha yetu, huku tukitafuta kuishi kila si na kila kitu kwa upendo na kwa huruma.

Watakatifu ni ndugu kaka na dada

Baba Mtakatifu Francisko akifafanua zaidi juu ya watakatifu anasema, watakatifu tunaoadhimisha leo hii katika liturujia  ni ndugu, kaka na dada ambao katika maisha yao walitambua kuwa ni wahitaji wa  mwanga wa Mungu, wakajikabidhi kwake kwa imani kuu. Na sasa wako mbele ya kiti cha enzi cha  Mungu (Uf, 7,15) wakiimba mielele utukufu wake. Hawa wanatengeneza:“mji Mtakatifu” ambao tunautazamia kwa matumaini, kama ndiyo hatima yetu ya mwisho. Ni kutembea kuelekea ule mji mahali ambapo wanatusubiri ndugu, kaka na dada watakatifu. Ni kweli sisi ni wanahija katika mji wa dunia hii, tukiwa na hali ngumu na uchovu kutokana na ugumu wa safari.

Kwa kutazama maisha yao tunachochewa kuwaiga

Baba Mtakatifu Francisko anasema, kati yao kuna mashuhuda wengi wa utakatifu katika mlango wa jirani, na wa wale wanaoishi karibu na sisi, na wanaangazia uwepo wa Mungu ( Gaudete et exsultate,7). Kumbukumbu ya watakatifu inatupeleka kuamsha kuinua macho juu mbinguni,  na siyo kusahau hali halisi ya ardhi hii, lakini kwa ajili kukabiliana zaidi kwa ujasiri na matumaini. Kwa kuhitimisha ameomba tusindikizwa na Mama Mtakatifu Maria kwa njia ya Maombezi yake na ishara ya faraja na matumaini  hakika.

 

01 November 2019, 13:30