Baba Mtakatifu Francisko kwa vijana:anayesahau kifo anaanza kufa!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Utamaduni unaosahau kifo ni kuanza kufa ndani mwake. Anayesahau kifo tayari anaanza kufa, ndiyo maneno aliyoanza nayo Baba Mtakatifu Francisko katika fursa ya Mkutano wa IV wa kimataifa kwa njia ya video kwa vijana na ambao umeitimishwa tarehe 31 Oktoba 2019 katika mji wa Mexico. Akiwaelekea vijana wa Scholas Occurentes, Baba Mtakatifu anasimamia juu ya maana ya kifo na kusema kwamba kama neno linavyozaliwa kutokana na ukimya na pale linaweza kuisha,huku likiruhusu kusikiliza maana yake, hiyo pia inajitokeza katika maisha! Na labda hii inaweza kueleweka tofauti, japokuwa ni kifo ambacho kinafanya maisha kubaki hai, amefafanua Baba Mtakatifu Francisko.
Kifo ni mwisho unaoruhusu kuandika historia
Kifo ni mwisho ambao unaruhusu kuandika historia na kuweza kuichora katika pichamambo mawili yanayokumbatiana. Lakini inabidi kuwa makini, kwa maana mwisho siyo mwisho na labda tunapaswa kuwa makini kwa kile kidogo ambacho ni maisha ya kila siku, anasema Baba Mtakatifu Francisko. Na siyo mwisho wa historia ambayo hatujuhi kila neno lililoandikwana kama ilivyo kwamba siyo mwisho wa kila neno la mwisho ambalo limo ndani ya ukimya. Ni kwa njia ya utambuzi wa dhamiri ya maisha ya sasa na ambayo yanaweza kuwa ndiyo maisha ya baadaye yaani ya mwisho, anabinisha Baba Mtakatifu.
Kifo kinatufundisha kuwa na uhusiano na fumbo
Katika Ujumbe wake kwa njia ya video Baba Mtakatifu Francisko zaidi anasema, kifo kinatukumbusha kuwa hatuwezi kutambua yote. Ni kama kupigwa kofi usilojua la mwenyezi Mungu. Na maisha yanatufundisha kuwa na uhusiano na fumbo. Pia ni kutufundisha kuwa, daima kuna mtu kule anayetusaidia. Mapema au baadaye kuna aina tatu za kifo. Hizi zinaweza kukung’uta au kukujaza maisha. Aina tatu hizo Baba Mtakatifu anazitaja kuwa ni kifo cha kila wakati; kifo cha ubinafsi na kifo cha ulimwengu ambacho kinatoa njia mpya katika ulimwengu mpya. Kwa kuhitimisha, amesema iwapo neno la mwisho siyo kifo ni kwa sababu katika maisha tumejifunza kufa kwa ajili ya mwingine.
Itambue Scholas Occurrentes:imenea nchi 190 duniani
Mkutano huo ulifunguliwa tarehe 28 Oktoba 2019 katika mji wa Mexico, uliondaliwa na Scholas Occurrentes na orld Ort. Tukio hili limeudhuria na zaidi ya wawakilishi 250 kutoka nchi 60 duniani kote. Scholas Occurrentes ni Taasisi ya Kipapa, iliyoundwa na Baba Mtakatifu tarehe 13 Agosti 2013 na tarehe 9 Juni 2017 ilizinduduliwa rasmi, yenye kuwa na lengo la kuhamasisha na kutetea, kwa njia ya elimu, sanaa na michezo, utamaduni wa kukutana kati ya vijana wa dini zote, ili kuchangia katika ujenzi wa jamii bora kupitia nguzo ya mazungumzo na katika kuhakikisha amani duniani. Leo hii Scholas Occurrentes imesimika mizizi katika nchi 190 ulimwenguni kote, ikiwa na mtandao zaidi ya mashule 500,000 na mitandao ya kielimu ya madhehebu yote ya dini, umma na binafsi ambapo Juni 2017 imekuwa na makao yake makuu katika mji wa wa Roma.