Misa ya baba Mtakatifu Francisko katika kuadhimisha Siku ya Masikini duniani 2019 Misa ya baba Mtakatifu Francisko katika kuadhimisha Siku ya Masikini duniani 2019 

Baba Mtakatifu Francisko:maskini ni walinzi wa mlango wa mbingu

Baba Mtakatifu anasema ni jinsi gani ingekuwa vizuri iwapo maskini wangeweza kupata nafasi moyoni mwa kila mtu kama walivyo na nafasi ndani ya moyo wa Mungu.Kukaa na maskini,kuhudumia masikini tunajifunza radha ya Yesu,tunatambua nini kinabaki na nini kinapita.Maskini ni tunu na thamani ya Kanisa.Maskini ni walinzi wa mlango wa mbinguni.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika Injili ya leo Yesu anashangaza watu wa wakati ule na hata sisi. Hii ni kutoka na kwamba wakati wao wanasifia hekalu zuri  la Yerusalemu, Yeye anasema halitabaki jiwe juu ya jiwe. Je ni kwa nini anasema mananeo hayo katika jambo kubwa takatifu na wala si tu kama jengo, bali ishara yao ya kidini yaani nyumba ya Mungu na kwa ajili ya watu waamini. Kwa  nini Mungu anaacha uanguke uhakika na wakati dunia inabaki ikiwa bila kuwa na uhakika huo? Ndiyo mwanzo wa mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko,wakati wa kuadhimisha Misa Takatifu katika kilele cha Siku ya Maskini Duniani Jumapili tarehe 17 Novemba 2019 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican.

Yesu anasema yote yatapita lakini siyo yote

Baba Mtakatifu akiendelea na mahubiri anasema  katika hili ni kutafuta jibu katoka katika maneno ya Yesu. Leo hii anasema yote yatapita. Na karibu kila kitu , japokuwa siyo yote. Katika Jumapili hii inayokaribia  kufunga mwaka wa liturujia ya Kanisa Yesu anaeleza kuwa yote yatapita mambo ya karibu na mwisho, lakini siyo ya mwisho. Ni hekalu na lakini siyo Mungu. Ni falme na matukio ya ubinadamu na siyo mtu. Mambo yatapita yakiwa ya mwisho na ambayo ufikiriwa mara nyingi kuwa ya mwisho ,japokuwa siyo hayo. Ni hali halisi kubwa kama  ya mahekalu yetu na ya ajabu, kama vile tetemeko la ardhi  ishala za mbingu,na vita vya dunia ( Lk 10-11). Kufuatana na hiyo  utafikiri sisi  tuko katika kurasa za kwanza za habari , lakini Bwana anaweka ukurasa wa pili. Katika ukurasa wa kwanza unabaki yale ambayo hayatapita kamwe, yaani Mungu aliye hai,  aliye mkuu zaidi ya kila hekelu tunayoyajenga na mtu, jirani, mwenye kuwa na thamani zaidi ya habari zozote za dunia na kwa kusaidiwa kupokea kile kilicho cha muhimu katika maisha. Hata hivyo Baba Mtakatiofu Francisko amebainisisha kwamba katika hayo yote  Yesu mwenyewe  anataka  kutupatia  taadhali dhidi ya vishawishi viwili.

Haraka ni  kishawishi ambayo Yesu anataadhalisha

Baba Mtakatifu Francisko akianza kufafanua juu ya taadhali ya kishawishi cha kwanza anasema ni haraka na upesi.  Anatoa mfano kwamba ili kwenda kwa Yesu hakuna haja ya kwenda nyuma  ya yule  anayesema, mwishowe atakuja kwa haraka na kwamba wakati unakaribia…( Lk v 8)  Mtu huyo siyo wa kumfuata. Hii ina maana anayeeneza uvumi wa hatari na kuongeza hofu kwa wengine juu ya wakati ujao, kwasababu hofu inagandisha moyo na akili. Pamoja na hayo ni mara ngapi tunadanganywa na haraka ya kutaka kujua yote kwa haraka na upesi, kuwa na muwasho wa utukutu na wa habari ya mwisho ya kichocheo au kashfa, kwa kuwa na masimulizi makali, kupiga yowe kwa  anayetumia nguvu na kuwa na chuki zaidi. Baba Mtakatifu Francisko amesema lakini haraka hii yote haitoki kwa Mungu. Iwapo tunaanza kuangaika ya haraka tunasahau yale yanayobaki daima. Tunafuata mawingu yanayo toweka na tunapoteza mtazamo wa mbingu, kwa kupumbazwa na uchochezi wa mwisho; Na kwa maana hiyo huwezi kupata muda tena kwa ajili ya Mungu na kwa ajili ya ndugu anayeishi karibu nasi.

Ni kwa jinsi gani kuna ukweli huu?

Baba Mtakatifu Francisko aidha ameongeza kusema, ni kwa jinsi gani ulivyo ukweli huu leo hii? Tabia ya kukimbizana ili kuweza kupata kile kitu na upesi, inaudhi anayebaki nyuma na anayehukumiwa na kubaguliwa. Ni wazee wangapi, watoto wangapi, vitoto vichanga, watu walemavu, masikini ambao wanafikiriwa hawana faida. Ni kwenda kwa haraka, bila kuwa na wasiwasi kwamba umbali unaongezeka na uchu wa wachache unakuza umasikini wa wengi. Hata hivyo Baba Mtakatifu Francisko amesema,  Yesu kwa kuonesha dawa dhidi ya haraka anapendekeza leo hii kwa kila mmoja ili kuwa na uvumilivu kwa maana anasema, “katika uvumilivu wenu mtaokoa maisha yenu” . Uvumilivu ni kwenda mbele kila siku kwa mtazamo wa macho wa kile ambacho hakipiti , yaani Bwana na jirani. Tazameni! maana ya uvumilivu ni zawadi ya Mungu ambayo inatunza zawadi nyingine (Mtakatifu Agostino, De dono perseverantiae, 2,4). Baba Mtakatifu Francisko akizungumza juu ya udanganyifu wa pili ambao Yesu anataka kutuepusha ni pale anaposema “ wengi watakuja kwa jina langu na kusema ni mimi, lakini msiende nyuma yao ”(…)  Hiki ni kishawishi cha mimi. Mkristo hasiyetaka haraka, kwa maana hiyo, siyo mfuasi wa "mimi", bali wa wewe. Yeye hafuati mambo yake binafsi bali kufuata mwaliko wa upendo yaani sauti ya Yesu.

Je sauti ya Yesu inatofautishwa kwa namna gani?

Wengi watakuja kwa jina langu, asema Bwana, lakini siyo wa kufuatwa. Haitoshi kuwa na tiketi ya kikristo au ukatoliki ili kuwa wa Yesu, anasisitiza Baba Mtakatifu Francisko. Ni lazima kuzungumza kugha yake Yesu, ile ya upendo, lugha ya ukaribu. Anayezungumza lugha ya Yesu hasema “mimi” bali anayetoka ndani mwake binafsi. Je ni mara ngapi hata kwa kutenda wema tu, unatawala unafiki wa umimi? Kwa mfano: ninafanya vema kwa sababu ninataka nijulikane; ninatoa zawadi, ili baadaye nipate kurudishiwa; ninasaidia ili niweze kuvutia urafiki wa mtu muhimu!  Lugha ya umimi inazungumza namna hiyo, Baba Mtakatifu anabainisha. Neno la Mungu kinyume chake linatoa msukumo wa upendo na siyo kufanya unafiki  (Rm 12,9), na kumpati mtu ambaye hataweza kukurudishia (Lk 14,14),

Je mimi kama mkristo ninaye rafiki maskini?

Maskini ni tunu msingi machoni pa Mungu kwa sababu hazungumzi lugha ya umimi. Kwa mfano, wao hawajisaidii peke yao kwa nguvu zao,  wao wanahitaji mwenye kuwapa mkono wa kuwasaidia. Maskini wanatukumbusha kuwa Injili inaishi kwa maana hiyo, ni kama ombaomba kwa Mungu. Uwepo wa maskini utatupelekea katika hali ya Injili mahali ambapo kuna heri za maskini wa roho. Kwa maana hiyo badala ya kumwona ni msumbufu anapobisha mlangoni, tunaweza kuwafungulia na kuwasikiliza kilio chao cha kupata msaada kama wito wa kutoka nje ya umimi na kuwapokea kwa mtazamo ule ule wa upendo wa Mungu aliyo nao juu yao. Baba Mtakatifu anasema, ni jinsi gani ingekuwa vizuri iwapo maskini wangeweza kupata nafasi moyoni mwa kila mtu, na  kama jinsi walivyo na nafasi ndani ya moyo wa Mungu! Kukaa na masikini, kuhudumia maskini tunajifunza radha ya Yesu, tunatambua nini kinabaki na nini kinapita.

Masikini anayeomba upendo kwangu ananipeleka mbinguni

Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu Francisko kwa waamini ameomba kurudia katika swali la kwanza hata kwa kutazama ni kitu gani cha mwisho kinapita, kwa maana Bwana anataka kutukumbusha leo hii kile cha mwisho kuwa kinabaki daima. Ni upendo kwa maana Mungu ni upendo ( Yh 4,8) na masikini anayeomba upendo wangu ananipeleka moja kwa moja kwake. Maskini wanaturahisishia njia ya kuelekea mbinguni. Na kwa maana hiyo imani ya watu wa Mungu walikuwa wanamwona maskini kama mlinzi wa mlango wa mbingu. Tangia sasa maskini tayari ni tunu na tunu ya Kanisa. Wanafungasha kwa dhati utajiri ambao hauzeeki kamwe na ambao upo duniani na kule mbinguni na ambao unastahili kwa dhati kuuishi yaani upendo.

PAPA 17 NOV

 

17 November 2019, 10:50