Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko akiwa na viongozi wakuu wa nchi ya Sudan wakati wa mafung ya kiroho yaliyfanyika mjini Vatican kunako Aprili mwaka huu Baba Mtakatifu Francisko akiwa na viongozi wakuu wa nchi ya Sudan wakati wa mafung ya kiroho yaliyfanyika mjini Vatican kunako Aprili mwaka huu  (Vatican Media)

Papa ametangaza ziara yake nchini Sudan Kusini mwaka kesho!

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana,Baba Mtakatifu Francisko ametoa wito kwa ajili ya upanisho wa kitaifa nchini Sudan Kusini na kutangaza juu ya ziara yake nchini humo mwaka kesho.Aidha ameombea nchi ya Bolivia.walio katika mgogoro mkubwa wa kisiasa.Wazo jingine ni katika Kanisa nchini Italia wakiwa wanaadhimisha Siku ya Kitaifa ya kutoa Shukrani kwa matunda ardhi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Jumapili tarehe 10 Novemba 2019, mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu Francisko ameelezea utashi wake wa kuitembelea nchi ya Sudan Kusini mwaka kesho. Hata hivyo katika fursa ya mkutano wake na Rais wa Jamhuri hiyo  Bwana Salva Kiir, katika maongezi yao alikuwa ameonesha utashi wake wa kutembelea nchi hiyo kama ingewahikikishia hali ya uwezekano wa kutembelea nchi hiyo kama ishara ya ikaribu wa watu na kuwatia moyo katika mchakato wa amani. Mapenzi ya Baba Mtakatifu ya kutaka kutembelea nchi ya Sudan Kusini, yamewaidia wakati siku hizi nchi imekumbwa na mafuriko makubwa na kusababisha karibia watoto 490,0000 kuwa na mahitaji ya kibinadamu. Dharura hii pia inaongezea ile hali mbaya ya kisiasa inayoonekana bado kuyumba katika  mazungumzo kati ya rais Salva Kiir na kiongozi wa zamani wa waasi Riek Machar ili kuweza kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Kukumbusha mafungo ya kiroho

Hata hivyo Baba Mtakatifu Francisko amekumbuka juu ya  mafungo yao ya kiroho yaliyofanywa na viongozi wakuu wa nchi mjini Vatican kunako mwezi April mwaka huu na kurudia kutoa mwalikokwa wadau wote wa mchakato wa kisiasa kitaifa ili kutafu kile kinacho unganisha na kushinda kile kinacho watenganisha katika roho ya udugu wa kweli na kuwashauri watu wote wasali sala kwa ajili ya nchi ya Sudan kusini. Watu wa Sudan: Kusini wameteseka sana katika miaka ya hivi karibuni na wanangojea kwa matumaini kuwa na  maisha bora ya baadaye, hasa mwisho wa mizozo na amani ya kudumu", amesema Baba Mtakatifu Francisko  na kuongeza kusema kuwa “nawasihi wale walio na jukumu ili kuendelea, bila kuchoka, jitihada kwao  kwa ajili ya kukuza majadiliano jumuishi katika kutafuta makubaliano kwa ajili ya wema wa taifa”. Na zaidi pia ni matumaini yake kuwa jumuiya  ya kimataifa haitakosa kuzingatia kuwasindikiza Sudan Kusini katika njia ya upatanisho kitaifa. "Ninawaalika nyinyi nyote kusali pamoja kwa ajili ya nchi hiyo ambayo kwa namna ya pekee ninaionea uhuruma"

Sala kwa ajili ya Bolivia

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na maelezo  vile vile amewakabidhi waamini wasali kwa ajili ya hali halisi inayoendelea nchini Boliva, mahali ambapo hatimaye Rais Evo Morales ametangaza kufanyika kwa uchaguzi mpya wa urais mara baada ya maandamano makubwa sana ya kura za tarehe 20 Oktoba 2019.

Uhusiano kati ya ardhi na kazi

Baba Mtakatifu hatimaye amehitimisha kwa kukumbuka Siku ya Kitaifa ya kutoa shukurani kwa Mungu kwa ajili ya Matunda ya ardhi na kazi, siku ambayo imeadhimisha nchini Italia Jumapili 10 Novemba 2019. Katika fursa hiyo Baba Mtakatifu Francisko  anaungana na maaskofu wote kuhusu wito wao "Katika kukumbuka uhusiano mkubwa kati ya mkate na kazi, tumaini la sera za kisiasa katika ujasiri wa kutafuta ajira zinazo zingatia hadhi na mshikamano na kuzuia hatari za ufisadi.

11 November 2019, 10:40