Tafuta

Tuwaombee Marehemu wote waliotutangulia katika makao ya Bwana huko mbinguni Tuwaombee Marehemu wote waliotutangulia katika makao ya Bwana huko mbinguni 

Katika utamaduni hasi wa kisasa juu ya kifo twende makaburini kusali!

Katika siku hizi ambazo kwa bahati mbaya kuna mzunguko wa ujumbe wa utamaduni hasi kuhusu kifo na wafu,Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waamini wasiache iwapo kuna uwezekano wa kutembelea na kusali katika makaburi.Amesema hayo mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana,tarehe 1 Novemba 2019,wakati Mama Kanisa anadhimisha siku kuu ya Watakatifu wote!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mara baada ya tafakari yake, kwa waamini na mahujaji waliofika katika Kiwanja cha Mtakatifu petro Vatican  Baba Mtakatifu, wakati Mama Kanisa anaadhimisha Sikukuu ya Watakatifu wote, tarehe 1 Novemba 2019 amewasalimia mahujaji wote toka pande zote za dunia kuanzia na Italia kwa namna ya pekee kikundi cha Vijana wa Chama Katoliki cha vijana na viongozi wao waliofika wengi kutoka  majimbo yote katoliki nchini  Italia wakiwa wanaadhimisha Jubilei ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Vijana Katoliki.

Amewasalimia wanariadha ambao kila mwaka katika siku kuu ya watakatifu wote wanafanya mbio, katika  tukio linaloanadaliwa na Chama cha Kitume cha Don Bosco, ili kuthibitisha katika ukuu wa sikukuu ya watu watakatifu  ile thamani ya kidini inayojikita na maadhimisha ya Watakatifu wote. Anawashukuru wote, maparokia, na jumuiya ambazo kwa siku hizi wanahamasisha sala kwa ajili ya kuadhimisha Sikukuu ya watakatifu  wote na kufanya kumbukumbu ya waliokufa.

Sikukuu hizi za kikristo, Baba Mtakatifu Francisko anasema kwama, zina uhusiano kati ya  Kanisa na mbingu, kati yetu na ndugu zetu wapendwa ambao wamepitia katika maisha haya kwenda mengine. Vile vile amekumbusha kwamba Jumamosi Jioni tarehe 2 Novemba atakwenda katika Makatakombe ya Priscilla , moja ya maneo ya makuburi ya wakristo wa kwanza wa Roma. Na kwa maana hiyo pia amesema katika siku hizi ambazo kwa bahati mbaya kuna mzunguko wa ujumbe wa utamaduni hasi kuhusu kifo na marehemu, Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waamini wote wasiache iwapo kuna uwezekano wa kutembelea na kusali katika makaburi. Na kwa wote anawatakia siku kuu njema akiwa anawasikindikizwa kiroho na watakatifu. Kwa mara nyingine tena wasisahau kusali kwa ajili yake na amewatakia mlo mwema na mchana mwema.

01 November 2019, 13:35