Tafuta

Vatican News

Papa kwa vijana wa Marekani:Enendeni pembezoni mwa maisha!

Kuanzia tarehe 21-23 Novemba huko Indianaolis nchini Marekani katika Kituo cha Mkataba wa India,unafanyika mkutano wa vijana uliondaliwa na Baraza la Chama cha Vijana Katoliki kitaifa kwa kuongozwa na mada ya Heri iliyovunjika.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tangu Alhamisi tarehe 21 hadi Jumamosi 23 Novemba 2019 huko Indianapolis nchini Marekani, katika Kituo cha Mkataba wa India, unafanyika mkutano wa vijana ulioandaliwa na Baraza la Chama cha Vijana Katoliki kitaifa (NCYC) kwa kuongozwa na mada ya “Heri iliyovunjika”. Katika ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa njia ya video kwa lugha ya kispanyola anawaalika waende mbali zaidi, hasa waweze kuwafikia watu wa Mungu wanaoteseka. Ujumbe wake unawalenga hao mamia ya vijana ambao wameunganika kwa pamoja na ambapo Baba Mtakatifu Francisko anasema kwamba mkutano huo ni fursa ya kuamsha mioyo yao katika jitihada za kimisionari na nguvu ya kiimani.

Ujumbe  Baba Mtakatifu amesema: “Vijana wapendwa, ninawatumia salam kwa upendo na sala zangu katika fursa ya mkutano wenu ambao mnaufanya. Mkutano huo iwe ni fursa ya kuongeza nguvu, kukua  kiimani na muungano; mkutano huo uwashe ndani mwenu mioyo ya kimisionari kwa ujasiri na nguvu ya kuishi ndani na Bwana  mkiwa kama Kanisa linalotoka nje! na daima. Leo hii kama ilivyokuwa tangu mwanzo, lazima kwenda kukutana na kila mtu na zaidi ni zoezi letu  la kufanya hivyo hasa kwa waliombali na wale ambao wanateseka zaidi. Lazima kufikia pembezoni mwa maisha katika dunia yetu!

Aidha mwaliko wa Baba Mtakatifu ni ule wa kwenda kwa maana hiyo anathibtisha kuwa: "kuna  haja ya kwenda na daima na silaha ya Roho na mwamko wa ushuhuda ambao unatangaza vema zaidi ya maneno elfu. Lakini  si kwa njia ya upropaganda unaleta uongofu kwa yoyote yule. Na hivyo kuna haja ya kwenda hasa kwa wale waliopeke yao, wagonjwa na kuelekea kwa yule anayeteseka pia kwa wale ambao bado hawamjuhi Yesu."

Kadhalika Baba Mtakatifu Francisko amesema: "Ninyi mnawajua rafiki zenu na mnatambua kuwa wengi wako peke yao, na wengi hawamjuhi Yesu. Nendeni, nendeni na kupeleka Bwana; nendeni na mjaze mazingira yenu hata yale ya kidigitali, lakini siyo kwa kulazimisha; siyo kwa kutaka ushindi na siyo kwa njia ya kufanya upropaganda, bali kwa njia ya kushuhudia kwa upole na huruma  yake  Yesu". "Ninawabariki kwa moyo na msisahau kusali kwa ajili yangu! Asante.

 

PAPA-MAREKANI
23 November 2019, 09:39