Baba Mtakatifu Francisko anawataka vijana wa Thailand kusali na kutembea kwa kumwachia nafasi ya kwanza Mwenyezi Mungu katika maisha yao! Baba Mtakatifu Francisko anawataka vijana wa Thailand kusali na kutembea kwa kumwachia nafasi ya kwanza Mwenyezi Mungu katika maisha yao! 

Hija ya Papa Francisko Thailand: Ujumbe kwa vijana wa kizazi kipya!

Hata katika udhaifu wao, wanaweza kuteleza na kuanguka, lakini wawe na ujasiri wa kusimama na kuendelea na safari. Baba Mtakatifu anasema, vipande hivi vya ushauri viwasaidie kusimama mara moja na kusonga mbele kwa ari na moyo mkuu! Jambo la pili, Baba Mtakatifu anawataka vijana kuchakarika na kamwe wasibweteke na kuzeeeka huku wakiwa wamekaa kwenye makochi.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko kuanzia tarehe 19-23 Novemba 2019 anafanya hija ya kitume nchini Thailand inayoongozwa na kauli mbiu: “Mitume wa Kristo, Wamisionari Mitume”. Hija hii ni sehemu ya maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 350 tangu kuanzishwa kwa utume wa Vikarieti ya Siam kunako mwaka 1669. Baba Mtakatifu, Jumatano jioni, tarehe 20 Novemba 2019 amewatumia ujumbe vijana wa Thailand waliokuwa wanakesha kwa ajili ya ziara yake nchini humo kusali na kutembea ili waweze kuwa na moyo ambao uko wazi ili kutoa nafasi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Haya ni mambo makuu mawili ambayo vijana wanapaswa kuyazingatia katika maisha yao.

Hata katika udhaifu wao, vijana wanaweza kuteleza na kuanguka, lakini wawe na ujasiri wa kusimama na kuendelea na safari. Baba Mtakatifu anasema, vipande hivi vya ushauri viwasaidie kusimama mara moja na kusonga mbele kwa ari na moyo mkuu! Jambo la pili, Baba Mtakatifu anawataka vijana kuchakarika na kamwe wasibweteke na kuzeeeka huku wakiwa wamekaa kwenye makochi. Vijana wajitahidi kujenga na kufurahia maisha yao, tayari kusonga mbele. Vijana wajihusishe kikamilifu katika maisha na hapo watagundua “siri ya urembo” na furaha katika maisha!

Papa: Vijana
21 November 2019, 14:52