Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko Jumamoi tarehe 23 Novemba 2019 amewasili nchini Japan kwa hija ya kitume! Njiani ametuma salam na matashi mema kwa wakuu wa nchi mbali mbali. Baba Mtakatifu Francisko Jumamoi tarehe 23 Novemba 2019 amewasili nchini Japan kwa hija ya kitume! Njiani ametuma salam na matashi mema kwa wakuu wa nchi mbali mbali.  (ANSA)

Hija ya Papa Francisko nchini Japan: Matashi mema kwa viongozi

Baba Mtakatifu ametuma ujumbe na matashi mema kwa Marais na wakuu wa nchi wa Thailand, Laos, Vietnam, China, Hong Kong na Taiwan. Kwa namna ya pekee, amemshukuru Mfalme Maha Vajiralongkorn Rama X wa Thailand na watu wote wa Mungu nchini humo, kwa mapokezi makubwa na ukarimu waliomwonesha anapenda kuwahakikishia sala na sadaka yake kwa ajili yao!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko kuanzia tarehe 19-23 Novemba 2019 amekuwa akifanya hija ya kitume nchini Thailand iliyoongozwa na kauli mbiu: “Mitume wa Kristo, Wamisionari Mitume”, kama sehemu ya maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 350 tangu kuanzishwa kwa utume wa Vikarieti ya Siam kunako mwaka 1669 na huo ukawa ni mwanzo wa kuenea kwa Ukristo nchini Thailand. Jumamosi, tarehe 23 Novemba 2019 Baba Mtakatifu amehitimisha hija yake ya kitume nchini Thailand na kuanza kuelekea nchini Japan. Baba Mtakatifu katika ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii anasema, anawashukuru wale wote waliojisadaka bila ya kujibakiza ili kuhakikisha kwamba, hija yake ya kitume nchini Thailand inapata mafanikio makubwa.

Akiwa njiani, Baba Mtakatifu amepata nafasi ya kutuma ujumbe na matashi mema kwa Marais na wakuu wa nchi wa Thailand, Laos, Vietnam, China, Hong Kong na Taiwan. Kwa namna ya pekee kabisa, Baba Mtakatifu amemshukuru Mfalme Maha Vajiralongkorn Rama X wa Thailand na watu wote wa Mungu nchini humo, kwa mapokezi makubwa na ukarimu waliomwonesha tangu alipowasili nchini humo na kwamba, anawahakikishia sala na sadaka yake. Baba Mtakatifu anaiombea Thailand neema na baraka tele na Mwenyezi Mungu mwini wa huruma na mapendo aendelee kuwaongoza katika njia ya hekima, haki na amani.

Papa: Salam
23 November 2019, 16:28