Tafuta

Vatican News
Tarehe 15 Novemba,Baba Mtakatifu Francisko alikutana na washiriki wa Mkutano wa Chama cha kimataifa cha sheria ya makosa ya  jinai Tarehe 15 Novemba,Baba Mtakatifu Francisko alikutana na washiriki wa Mkutano wa Chama cha kimataifa cha sheria ya makosa ya jinai  (Vatican Media)

Msingi wa haki ya kweli ni mazungumzo si utamaduni wa ubaguzi!

Baba Mtakatifu wakati akitoa hotuba yake kwa washiriki wa Mkutano wa XX wa Chama cha kimataifa cha sheria ya makosa ya jinai amekumbusha juu ya tatizo la haki kibinadamu na maana ya haki katika mtazamo wa kikristo duniani.Hata hivyo ametoa onyo dhidi ya utumiaji wa mantiki ya upendeleo wa soko na hatari za mawazo ya kutoa hukumu kwa walio wadhaifu wasiokuwa na mtetezi.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Baba Mtakatifu Francisko alikutana na washiriki wa Mkutano wa XX wa Vyama vya Kimataifa vya Sheria ya makosa ya jinai tarehe 15 Novemba 2019 mjini Vatican. Katika hotuba yake amesema kwamba kwa  miaka miaka mingi sheria ya makosa ya jinai imekuwa ikipata mchango na changamoto kubwa juu ya  nidhamu nyingine na tofauti ya utambuzi wa matatizo yanayo husu hasa zoezi la uendeshaji wa michakato  wa kuweza kugundua na kutoa ushauri. Hata hivyo amekumbusha kwamba kati ya washiriki pia walikuwapo wengine na ambao masuala haya yalikuwa yameshazungumzwa katiia mkutano uliopita. Licha ya ufunguzi wa dunia ya sasa, anasema lakini baso  sheria ya jinai haijakidhi haja na ili  kuondokana na hatari ambazo zinaonekana katika nyakati zetu na mabazo zinatazama ndani ya udemokrasia na uhalali kamili wa sheria.

Sheria ya makosa ya jina bado haizingatii data halisi

Vile vile Baba Mtakatifu Francisko anasema licha ya hatua zake lakini bado sheria ya jinai haizingatii hata takwimu halisi na kwa maana hiyo inatoa mtazamo wa sura ya maarifa ya kibinafsi.  Katika kufafanua hili anaasema ni lazima kutazama mantiki  mbili za sasa  zinazo ikabili dunia. Mantiki ya kwanza inahusu suala la masoko. Hii ina maana kwamba mtu mdhaifu na ambaye ni mwathirika mara nyingi anajikuta hana msimamizi na mtetezi mbele ya wale wanaopenda biashara au fedha  na ndiyo kwao inakuwa kama kanuni yao (Rej.Evangelii gaudium, 56; Laudato si’, 56).

Baadhi ya sekta za kiuchumi zinaendesha shughuli kwa kutumia nguvu

Baba Mtakatifu Francisko vile vile katika hotuma yake alibainisha kuwa baadhi ya sekta za kiuchumi zinaendesha shughuli zao kwa kutumia nabavu, ambazo pia ndizo za serikali (Rej Laudato si’, 196). Na hii ni hali halisi ambayo inaonekana wazi katika nyakati za utandawazi wa ufujaji wa fedha.  Hata hivyo msingi wa kutaka kwa nguvu zote kuzidisha faida, unabagua kila aina ya kufikiria sehemu nyingine ambayo upelekea kuwa na mtindo wa kibaguzi na hadi kufikia kutumia nguvu dhidi ya wale wanaoteseka na gharama za kijamii na kiuchumi na wakati na wakati huo huo hata kuwakumbuka kizazi kijacho ambacho kitalipa hata gharama za mazingira.

Wito kwa mahakimu ili kujiuliza nini la kufanya

Baba Mtakatifu Francisko  akiendelea na hotuba yake amewataka mahakimu wajiuliza  ni jambo gani linaweze kufanywa kwa njia ya fahamu zao  na ili kuweza kupinga tukio hili ambalo amethibtisha kuwa  linahatarisha Katiba za kidemokrasia na wakati huohuo hata kwa maendeleo ya binadamu. Kwa dhati amesema changamoto inayojitokeza kwa kila mwana sheria ni ile ya kufikiria ubaya wa adhabu na ambao unaojionesha hata hivyo katika ubaguzi kwa walio wengi.  Hawa ni:  waliorundikana na kupewa adhabu katika magereza, au kuhusiana na ugomvi na unyanyasaji wa vikosi vya usalama, upanuzi wa wigo wa adhabu, kuwahukumu watu kama wahalifu wale wanafanya maandamano kijamii, unyanyasaji kwa wale walioko vizuizini na kukataliwa kwa dhamana msingi  kufanya utaratibu wa mchakato kwa wahalifu.

Wazo la makosa ya jinai na hatari zake

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea kubainisha mantiki ya pili amesema ni kuhusu mawazo ya kudhania:"Moja ya changamoto ya sasa ya sayansi ya makosa ya jinai ni kuzusha maono ya mawazo ambayo utafikiri ni uhalisia", Baba Mtakatifu amebainisha. Hata hivyo amesema kwamba "uwekaji wa vikwazo hauwezi kuhalalishwa kimaadili na uwezo wa madai ya kuimarisha imani katika mfumo wa udhibiti na kwa matarajio kwamba kila mtu anachukua jukumu katika jamii na anafanya kulingana na kile kinachotarajiwa kwake". Na zaidi amekumbusha juu ya madhara ya moja ya kutomitimiza wajibu wa sheria ya jinai na matokeo yake.

Uharibifu kijamii wa uhalifu wa kiuchumi

Baba Mtakatifu Francisko pia amekumbuka kuwa mojawapo ya kuachwa mara kwa mara kwa sheria ya jinai, matokeo  ya upigaji kura wa sheria, uhaba au umakini kwa wale wanaopokea adhabu ya uhalifu kwa wenye nguvu  ni udhalilishaji mkubwa wa mashirika. Vile vile amesema mitaji ya kifedha ulimwenguni ni asili ya uhalifu mkubwa na siyo tu dhidi ya mali binafsi, lakini pia dhidi ya watu na mazingira! Hii inahusu uhalifu ulioandaliwa na kati ya mambo mengine ni kuhusu deni la nchi nyingi na uporaji wa mali ya asili ya sayari yetu.

Sheria za makosa ya jinai na uhalifu dhidi ya ubinadamu

Sheria ya makosa ya jinai haiwezi kubaki hivi hivi kama ngeni na zaidi inapofanyika kwa kutumia fursa za hali halisi, au kutumia nafasi kubwa inayotawaliwa na kudhulumiwa kwa uharibifu wa ustawi wa pamoja. Hii hufanyika, kwa mfano, wakati bei ya dhamana ya deni la umma inapunguzwa kwa nguvu, kwa njia ya kupeleleza bila kuwa na wasiwasi kwamba hii itasababisha au kuzidisha hali ya kiuchumi ya mataifa yote.  Aidha hii inatokea hasa kwa uzito wa uhalifu dhidi ya ubinadamu na zaidi inaposababisha njaa, umaskini, uhamiaji wa kulazimishwa na kifo kutokana na magonjwa  ambayo yangeweza kuepukwa, janga la mazingira  kuharibu mazingira ya watu asilia. Vile vile kuna madhara ya uchavuzi wa hali ya hewa, rasilimali za dunia na maji, uharibifu mkubwa wa mimea na wanyama na hatua yoyote inayoweza kuleta maafa ya kiekolojia au kuharibu mfumo wa ekolojia. Baba Mtakatifu Francisko amekumbuka kwamba hivi karibuni, wakati wa sinodi ya Kanda la  Amazonia, Mababa za sinodi walipendekeza suala hili kama dhambi ya kiekolojia na kama hatua au kumkosea Mungu dhidi ya wengine, jamii na mazingira.

20 November 2019, 09:56