Papa Francisko anasisitiza kuwa hakuna utamaduni wa kutumia na kutupa, badala yake uchumi urudi kuwa mantiki kimaadili. Papa Francisko anasisitiza kuwa hakuna utamaduni wa kutumia na kutupa, badala yake uchumi urudi kuwa mantiki kimaadili. 

Baba Mtakatifu:uundaji wa nafasi ya kazi ni sehemu muhimu ya huduma kwa faida ya wote!

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wa mkutano juu ya uchumi jumuishi na kuwakumbusha ulazima wa kuwa na mtindo wa wa uchumi jumuishi zaidi,ambao unaruhusu kila mtu awe na sehemu ya rasilimali ya dunia hii na kuweza kujikamilisha binafsi.Hakuna utamaduni wa kutumia na kutupa,badala yake uchumi urudi kuwa mantiki ya kimaadili.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu tarehe  11 Novemba 2019  amekutana na wajumbe wa Baraza la Uchumi Jumuishi ambapo amekuwakumbusha juu ya mkutano na washiriki  wa  Jukwaa kuhusu "fursa ya wakati ulimwenguni", kwamba  aliwasisitizia juu ya kuwa na mtindo wa kiuchumi ambao ni jumuishi zaidi na unaruhusu kila mtu awe na sehemu ya rasilimali ya dunia hii na kuweza kujikamilisha kwa nguvu zake binafsi. Jukwa la 2016 ilikuwa inaruhusu mbadilishano ya mawazo na mafunzo yanayo husu kuunda uchumi wa kibinadamu zaidi na kuchangia mawazo  juu ya kuondoa umasikini kwa ngazi ya kidunia. Mkutano wao ni matokeo ya Jukwaa la 2016 ambapo wamepokea changamoto ya kutimiza maono ya jukwa huku wakitafuta njia za kuweka uchumi kama chombo jumuishi kwa ajili ya wema wa kibadamu fungamani.

Kushinda uchumi wa kubagua na kupunga uwiano uliopo 

Akiendelea na hotuba yake Baba Mtakatifu Francisko amesema hata hivyo hiyo inahitaji kushinda ule uchumi wa kubagua na kupunguza ule  uwiano wa tofauti uliopo unaotenga sehemu kubwa ya watu katika  matazamio ya faida ya wachache (Evagelii gaudium 53-55). Kuongezeka kwa ngazi ya umasikini katika ngazi ya kiulimwengu ni ushuhuda wa ukosefu wa usawa unaozidi kuongeza katika ufungamisho wa maelewano ya watu na nchi. Ni lazima na dharura ya kuwa na  mfano wa kiuchumi wa haki, wa kuaminika na wenye uwezo wa kutoa jibu dhidi ya  changamoto zaidi zenye mzizi  ambapo binadamu na katika sayari hii anajikuta anakabiliana nayo. Baba Mtakatifu Francisko anawatia moyo wa kuenedelea na safari kwa ukarimu na mshikamano ,huku wakitahidi katika shughuli ili kuweza kurudi katika  uchumi na fedha kwa mantiki ya kimaadili na kusaidia kukuza ubinadamu. Ni kweli kwamba shughuli za wasajasiriamali ni wito mkubwa wenye kuelekeza kuzalisha utajiri na kuboresha dunia kwa ajili ya wote na inawezekana kuwa mtindo wa kuleta mwafaka kwa ajili ya kukuza kanda ambazo shughuli hizo zinafanyika hasa zinapotambua kuwa uundaji wa nafasi ya kazi ni sehemu muhimu ya huduma ya wema wa pamoja (Laudato si’, 129).

Maendeleo ya kweli kubaki katika kukuza uchumi tu

Baba Mtakatifu Francisko amesema kwamba hata hivyo kama alivyokumbusha Mtakatifu Paulo VI ni kweli kwamba maendeleo hayawezi kubaki tu katika  suala la kukuza uchumi, badala yake ni kukuza na kuhamasisha kila mtu na kila binadamu (Populorum progressio, 14). Hii ina maana kubwa ambayo inapimwa katika mzani ili kuboresha majengo na kutoa nafasi kubwa za bidha za kutumia. Inahitaji lakini kujipayisha na uongovu na bidii kubwa katika mtindo ya kiuchumi  wenye  msingi juu ya utu wetu wa uongofu na ukarimu mbele ya wenye kuhitaji. Mfumo wa kiuchumi usiyo angaikia maadili hauwezi kufikiria mahangaiko ya kijamii na yenye haki, badala yeke ni kufikiria ule utamaduni wa kutumia na kutupa na takataka. Kinyume chake na  hiyo tunapotambua ukuu kimaadili wa maisha ya kiuchumi, ambao ni moja ya mantiki nyingi za mafundisho ya Kanisa kijamii na ambayo inapaswa kuheshimiwa Baba Mtakatifu anakazia kwamba, iwe na uwezo wa kutenda kwa upendo kidugu, kuwa na shauku, kutafuta na kulinda wema wa wengine na maendeleo yao fungamani.

Kupanua fursa za mafano ya mfumo wa kiuchumi

Katika mkutano wao, Baba Mtakatifu Francisko amesema kwamba wamekusudia kupanua kwa ajili ya wote zile fursa na mafao ya mfumo wa sasa wa kiuchumi. Jitihada zao amesema, zinakumbusha kuwa wale ambao wanafanya juhudi  katika maisha ya kiuchumi na kibiashara, wanaalikwa  kuhudumia wema wa pamoja na kutafuta kuongeza mafao hayo katika dunia hii na kuwezesaha kufikia kwa watu wote (Evangelii gaudium, 203).  Lakini hiyo inahitaji upyaisho wa mioyo kwa kina na akili kwa namna ya kwamba, maisha ya binadamu yanaweza kuwa daima kitovu cha maisha ya kijamii, kiutamaduni na kiuchumi. Baba Mtakatifu Francisko aidha ameongeza kusema kwamba uwepo wao ni matumaini kwa asababu wametambua masuala ambayo dunia inaalikwa kukabiliana nayo na kutenda kwa uamuzi ili kujenga wakati ujao ulio bora.

Shukrani kwa uhamasishaji wa uchumi wa haki na kibinadamu

Anawashukuru Baba Mtakatifu  kwa ajili ya  jitihada hizo za kuhamasisha uchumi wa haki na kibinadamu katika mwendelezo wa misingi ya Mafunzo ya  Kanisa Kijamii na kuzingatia binadamu mzima na zaidi katika kizazi kilichopo na kijacho. Uchumi fungamanishi hauwezi kumwacha mtu nyuma na wala kubagua yoyote kati ya ndugu, kaka na dada na ndiyo matarajio mema  yenye hadhi katika jitihada zao. Amehitimisha kwa kuwashukuru na anawasindikia katika sala zake. Kwao  na juu ya familia zao, wanafanyakazi wenzao amewaombea baraka ya Mungu, kisima cha hekima, nguvu na amani na wakati huo ameomba wasali kwa ajili yake.

11 November 2019, 12:50