Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washirki wa Mkutano mkuu wa mwaka wa baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washirki wa Mkutano mkuu wa mwaka wa baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha 

Baba Mtakatifu Francisko:fungua upeo mpya wa kujua nini maana ya mwanamke katika Kanisa!

Baba Mtakatifu Francisko akizungumza na washiriki wa Mkutano Mkuu wa kwanza wa Mwaka wa Baraza la Kipapa la Walei,Familia na Maisha amewaalika wahisi kwa moyo wa Kanisa na kuwashauri wasiwafanye walei kuwa kama makleri na watambue vema nini maana ya mwanamke katika Kanisa kwa maana Kanisa ni Mama

Na Sr. Angela  Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 16 Novemba 2019, amekutana kwa mara ya kwanza na washiriki wa Mkutano wa kwanza wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha na kumshukuru Kardinali Ferrel kwa Rais wa Baraza hilo kwa hotuba yake. Katika hotuba yake amependa kuendeleza mantiki chache bila kuingilia kati kuhusu matatizo  maalum ambayo wajikita nayo  badala yake kutafuta namna ya kuwalekeza baadhi ya mambo muhimu ya kina ambayo yaweze kuwasaidia kwa siku za usoni. Nafasi yao waliyo nayo kama wajumbe na washauri amependekeza picha ya kuhisi kwa moyo wa Kanisa na picha ya udugu

Wanaitwa kushirikiana na Vatican katika safari yake 

Baba Mtakatifuakianza kufafania zaidi anasema wao wameitwa kushirikiana na Vatican ili kusaidia safari yake ya Baraza hilo jipya ambalo limeanzishwa karibu miaka miwili iliyopita, kwa kupokea urithi wa Baraza la Kipapa la Walei na Baraza la Kipapa la Familia kuwa kitu kimoja. Wote kwa pamoja, mapadre, watawa, walei waanalikwa pamoja kwa ajili ya kutoa huduma ya Kanisa la ulimwengu, huku wakihamasisha na kusaidia walei na familia na maisha duniani kote. Kwa maana hiyo ni wazi kila mmoja kufanya kazi kwa moyo wa Kanisa. Na hii inasaidia kuondokana na ubinafsi ili kuweza kuingia katika mantiki mpya na ambayo labda siyo kawaida kwa upande wao. Hii ina maana kwamba Kanisa Katoliki ni la ulimwengu ni pana sana. Kanisa lina moyo mkubwa na  linaheshimu hata mtazamo wa mtu binafsi. Kuhisi kwa moyo wa Kanisa maana yake ni kusikia kwa namna mojaya ukatoliki ulimwenguni na kungalia kila kitu cha Kanisa na katika dunia na siyo tu upande mmoja.

Kwenda mbele zaidi ya taaluma maalum waliyo nayo

Na zaidi kuna haja ya kufanya jitihada za kwenda mbele zaidi ya taaluma maaluum binafsi, ya kitaalimungu, uprofesa, udaktari , mhadhiri, mtoa mafunzo ya kichungaji  na mengine ili kuchukua jukumu la Mama Kanisa. Kanisa ni Mama na wao kama wajumbe na washauri wanao jukumu la  wa utambuzi na uzoefu waliobeba kwa miaka mingi na wanaalikwa kufanya hatua nyingine ya mbele na kujikita mbele zaidi katika mpango wa kiuchungaji, changamoto na matatizo yote. Kanisa kama mama linatamani kuona watoto wake wanakua na kujitegemea, wabunifu na waelewa bila kubaki kama watoto wadogo. Na wakati huo huo waamini wote walei na wana Kanisa wanapaswa kusaidia kukua na kuwa watu wazima, huku wakiondolea mbali ugumu na hofu na kutoka nje kwa namna hai, ya kijasiri, huku wakiweka talanta zao katika huduma ya utume wa kimisionari mpya katika jamii, katika utamaduni, katika siasa  na kukabiliana bila hofu ya ugumu ya changamoto za dunia ya sasa.

Mtazamo wa ndugu

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na hotuba yake, ametazama kipengele cha pili ambacho  ni kuhusu mtazamo wa ndugu.  Anasema mada inayaowaongoza katika Mkutano wao wa mwaka inatazama mafunzo ya waamini walei  ili kuongeza nguvu ndani mwao ya utambulisho na utume wao wa kimisionari duniani. Kufuatia na hiyo picha anayoipendekeza ni ile ya kuwa na mtazamo wa ndugu. Baba Mtakatifu amesema wao siyo mainjinia wa kijamii au kikanisa, ambao wanapanga mikakati ya kufanya katika dunia nzima ili kujieleza kati ya walei kuhuhusu aina ya mawazo ya kidini. Badala yake Baba Mtakatifu anasema, wao wanaalikwa kufikiria na kutenda kama ndugu katika imani kwa kukumbuka kuwa imani inazaliwa daima na kukutana binafsi na Mungu aliye hai na ambaye anashangaza katika kulisha kwa njia ya  Sakramenti ya Kanisa. Kila aina ya mafunzo ya Kanisa lazima isimamie juu ya uzoefu  msingi wa kukutana na Mungu na juu ya maisha ya Kisakramenti. Na zaidi kutokana na uzoefu wao na matatizo yao watatambua vema ugumu wa kila siku wa waamini wengi walei duniani mbao mara nyingi matatizo yamezidi kuongezeka wa hali ya umasikini na ukosefu wa msimamo kijamii, mateso ya kidini, na propaganda za mawazo ya kiitikadi dhidi ya wakristo.

Mashemasi wa kudumu waende kutoa huduma na siyo kukaa altareni

Picha ya Mama Maria katika sala akisubiri Roho Mtakatifu ni Mama ambaye anafanya kuishi kama ndugu. Baba Mtakatifu kabla ya kumaliza amekumbusha kuwa wao ni walei na wanapaswa kufanya kazi na wote bila kubagua. Mara nyingi ametoa mfano kuwa, imejitokeza katika jimbo la Buonos Aires, ambapo kuna paroko alikuwa anakuja na kumwambia  kuwa, anaye mlei mmoja wa kiajabu ambaye anajua kufanya kila kitu, je unaweza kumfanya awe shemasi?...  Katika tukio hilo, Baba Mtakatifu ametoa onyo kwamba,  kuna mashamasi wa kudumu ambao badala ya kuwa walinzi wa huduma ya kijimbo, kwa haraka wanatazama kwenda altare na kuishia kuwa kama  au mapadre waliokoswa koswa….mapadre nusu ya njia.  Baba Mtakatifu anawashauri maaskofu kwamba, wawaondoe hao mashemasi wanaopenda kukaa altareni, badala yake waende kutoa huduma. Mashemasi ni walinzi na wahudumu na siyo watu wa kusaidia altareni au kuwa padre wa daraja la pili.

Mwanamke anaweza hata kuongoza baraza

Jambo la pili ambalo limemjia akilini na kuhusu Baraza lao baada ya mapambano yasiyo rahisi na ambapo  Rais wa Baraza hilo anatambua na kuwa na Makatibu wawili waliowekwa wanawake wawili katika Baraza hilo, amesema wawili ni wachache! Lakini inabidi kuendelea mbele kwa ili kuweka wanawake katika nafasi ya Baraza hilo na hata serikali bila kuogopa. La muhimu ni kuzingatia uhalisia. Nafasi ya mwanamke katika Kanisa siyo tu kwa ajili ya kujishughulisha shughulisha tu. Kwa hakika ndiyo anaweza hata kuwa Mkuu wa Baraza la Kipapa. Hata hivyo amekumbuka kuwa  hivi karibuni wakati wa kutangaza mkuu wa Baraza la Kipapa la Uchumi anasema, katika orodha ya mwisho kulikuwapo na wanawake wawili na ambao wangeweza kuwa wakuu wa Baraza, Baba Mtakatifu amethibitisha. Na ndiyo hiyo namna ya utendaji. Lakini ni muhimu sana ushauri wa mwanamke.

Nini maana ya Mwanamke katika Kanisa

Vile vile Baba Mtakatifu Francisko amekumbusha kwamba, mmoja kati ya katibu mkuu msaidizi wa Baraza hilo, wakati wa Mkutano wa Maaskofu wa Mabaraza ya Maaskofu duniani mwezi Februari, kuhusu manyanyaso ya watoto, aliwachangamotisha kwa maana ya kuwa na mtindo mwingine wa kutazama na kufikiria. Na hiyo iliweza kutajirisha, amesema Baba Mtakatifu Francisko. Nafasi ya kuongoza na kushauri lakini ambayo aishii kuwa ya utendaji tendaji tu. Kuhusiana na suala hili Baba Mtakatifu anasema tunapaswa bado kufanya kazi kubwa. Nafasi ya mwanamke katika kuandaa kikanisa, katika Kanisa linakwenda zaidi ya hayo na lazima kufanya kazi juu ya hilo, na kwa sababu mwanamke ni sura ya Kanisa mama;  kwa sababu Kanisa ni mama; na siyo Kanisa tu bali Kanisa ni Mama. Kanisa lina uwezo wa kupeleka mbele hali halisi na mwanamke anayo shughuli nyingine. Na ndiyo mwanzo wa Mama Maria wa kuwa mwanamke: mwanamke katika Kanisa ni picha ya Kanisa mchumba na Mama. Baba Mtakatifu amehimiza kuzingatia mambo mawili: walei wasiwe wakleri na pia kufungua upeo mpya wa kujua vema nini maana ya mwanamke katika Kanisa.

 

16 November 2019, 16:57