Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amewatumia ujumbe kwa nnia ya video wakati wa kuadhimisha jubileio ya miaka 50 tangu kuanzishwa mji wa Cristobal ya Habana nchini Cuba Baba Mtakatifu Francisko amewatumia ujumbe kwa nnia ya video wakati wa kuadhimisha jubileio ya miaka 50 tangu kuanzishwa mji wa Cristobal ya Habana nchini Cuba 

Baba Mtakatifu Francisko:Imani upendo na matumaini ni nguzo za watu wa Cuba

Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe kwa njia ya video kutokana na fursa ya kuadhimisha jubilei ya miaka 500 tangu kuanzishwa mji wa Mtakatifu Cristobal wa Habana,Cuba.Katika ujumbe huo anasisitizia juu ya nguzo tatu zinazosimamia watu wa nchi hiyo kwamba ni imani upendo na matumaini.

Na Sr. Angela Rwezaula - Rwezaula

Wapendwa kaka na dada wa Habana ninayo furaha ya kuweza kuungana nanyi kwa njia ya ujumbe wa video katika kuadhimisha mwaka wa 500 tangu kunzishwa kwa mji wenu wa Mtakatifu Cristobal wa Habana. Ninapenda kusisitiza katika fursa hii mantiki tatu ambazo zimo tangu mwanzo wa mji wenu na ambazo zinaendelea kuwapo leo hii kama nguzo za wakati huu. Nguzo hizi ni imani,upendo na matumaini. Ndiyo Mwanzo wa ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa njia ya video, aliotuma tarehe 15 Novemba 2019 mjini Habana ikiwa katika mji huo wanaadhimisha jubilei ya miaka 500 tangu kuanzisha kwa mji huo.

Nguzo ya imani ni tabia ya watu wa Cuba

Baba Mtakatifu Francisko akianza kufafanua mantiki alizozitaja hapo kuhusu mji huo amesema imani, ndiyo mzizi wa mji huo. Mizizi ambayo inasaidia kuimarisha maisha na ambayo yanazidi kuendelea, mizizi ambayo inamwilisha, mizizi ambayo inasaidia kukua. Kwa kuongeza Baba Mtakatifu amesema :“msisahau mizizi ile, ushuhuda wa imani wa mababu zenu. Tendo la mwanzilishi wa mji wa Habana lilikuwa ni kuadhimisha Misa Takatifu. Hao ndipo kunapatikana kiini cha maisha ya kikristo. Katika Ekristi, sakramenti ambayo inapokelewa na  wakristo kama watu mbele ya uwepo wa Bwana, ambaye anazungumza nasi, anatulisha, anatutuma tuwe mashuhuda katikati ya ulimwengu. Ushuhuda wa Injili".

Nguzo ya upendo ni tabia ya watu wa Cuba

Bwana Yesu anatualika kuwa mashuhuda wa imani na hata mashuhuda wa sadaka na wa upendo. Upendo ndiyo mantiki inayo watofautisha watu wa Cuba amesisitiza Baba Mtakatifu na kwamba wao wamejifunza kutoka kwa Maria Mama wa Yesu, tangu mwanzo alipojionesha kati yao kwa jina la Bikira wa Upendo wa Cobre. Kwa maana hiyo upendo wa Maria unatufundisha kutoa upendo na kuutoa kwa huruma, kwa kujitoa na kwa kutoa upendo wa maisha ya kila siku. Je wapi? Baba Mtakatifu katika swali hilo pia anatoa jibu lake kwamba "ni katika familia, kati ya watu jirani na nyumba zetu, kazini, na kwa watu wote daima. Haijalishi wakifikiria namna kwa moja au nyingine, lakini la  muhimu ni kutoa upendo na kuwa na maelewano", amesisitiza Baba Mtakatifu Francisko. “Na kwa njia hiyo ndipo unazaliwa umoja wa wakristo wa Quba. Maelewano kati yenu. Kila mmoja wenu”. Baba Mtakatifu mesema: "Maria anatufundisha kutoa upendo huo na kwamba si tu kutoa chochote kwa wengine, bali zaidi ni kujitoa sisi wenyewe. Kuishi urafiki wa kijamii, unasaidia watu kwenda mbele".

Nguzo ya matumaini ni tabia ya Cuba

Na hatimaye katika ujumbe wake kwa njia ya video, Baba Mtakatifu anafafanua nguzo nyingine ya matumaini. Jubilei ambayo wanaadhimisha, iwe sababu ya kupyaisha matumaini anasisitiza: “Kama Mtakatifu Cristobal alivyokuwa anabeba kwenye mabega yake ndugu zake, "hata nyinyi kati yenu, ninawasihi msaidiane, ninawatia moyo ili kwenda mbele, bila kukata tamaa,  na daima kuwa na mtazamo wa kuelekea upeo ule”.  Hata hivyo amebanisha kwamba daima kutakuwa na matatizo ya maisha, watu watakuwa na matatizo, lakini umoja huo wa watu ambao wanaungana katika upendo, katika matumaini ya kwenda mbele yanasaidia watu kukua na nguvu. Baba Mtakatifu amehitimisha akimwomba Bwana ili nguzo hizi za imani, upendo na matumaini ziweze kuwasaidia na kama ilivyo pia furaha ni tabia ya kuendeleza iweze kweli kupyaishwa na kukuzwa katika nyakazi hizi za kipindi cha neema ya Jubilei. Bwana Yesu awabariki, awabariki watu wote wa Cuba na ambao anawakumbuka kwa upendo alipoitembelea nchi hiyo kunako mwaka 2015. Na Bikira Mama Yetu wa upendo wa Cobre, awatunze. Na wasisahau kusali kwa ajili ya Baba Mtakatifu.

15 November 2019, 12:10