Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na familia kubwa ya Jumuiya ya Hospitali ya Bambino Gesù tarehe 16 Novemba 2019 katika ukumbu wa Paulo VI Baba Mtakatifu Francisko amekutana na familia kubwa ya Jumuiya ya Hospitali ya Bambino Gesù tarehe 16 Novemba 2019 katika ukumbu wa Paulo VI 

Baba Mtakatifu amekutana na Jumuiya ya Hospitali ya Bambino Gesù

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na jumuiya kubwa ya Hospitali ya watoto Bambino Gesù wakiwa katika maadhimisho ya miaka 150 tangu kuanza kwa Taasisi hii ya Vatican.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Jumamosi tarehe 16 Novemba 2019 Baba Mtakatifu Francisko, amekutana zaidi ya watu 6,000  katika ukumbi wa Papa Paulo VI mjini Vatican kutoka Jumuiya ya Hospitali ya Bambino Gesù wakiwa ni watoto, kutoka sehemu mbalimbali za dunia, wazazi wao na wahudumu wao wote kwa ngazi zote. Ni katika kuadhimisha miaka 150 tangu kuanza kwa Hospitali ya Bambino Gesù inayomilikiwa na kuendeshwa na Vatican. Hospitali ilianzishwa  mwaka 1869 kama Hospitali ya kwanza kwa ajili ya watoto wagonjwa nchini Italia, ambapo miaka inavyokwenda mebele imekuwa na matawi mengi katika duniani. Katika hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko  ameonesha furaha yake kukutana nao kama familia kubwa ya hospitali hiyo katika kaudhimisha miaka 150 tangu kuanza kwake na ambayo ni mali ya Vatican na kusema  kuwa haitakosa kamwe kuweka umakini wake mkubwa kwa ajili ya watoto. Aidha anamshukuru Mwenyekiti wa Hospitali hiyo Bi Enoc na viongozi mbalimbali walikuwamo watu wa kujitolea madaktari na zaidi watoto wadogo wagonjwa na familia zao.

 Asili ya Hospitali ni zawadi ya Famia ya Arabela Salviati

Baba Mtakatifu Francisko amekumbusha asili a hospitali hiyo kwa  , familia ya Jacqueline Arabela de Fitz-James Salviati ambao walikuwa ni wamiliki na wakatoa zawadi kwa Vatican. Ni wazo kunjufu la Mama mwenye akili, utamaduni na imani, aliyeishi katika kipindi cha pili cha matunda ya ukatoliki   kijamii. Na zaidi ya familia karimu ambayo ilifanya kazi kwa ishara kubwa ya uwelewa kwa ajili ya kusaidia watoto wote duniani.  Kwa hakika ile mbegu iliyonza imekuwa na maendeleo zaidi ya mipaka ya Roma, shukrani kwa zawadi aliyo mpatia Papa na ambayo ni ya kichungaji,  inaendelea kila mahali na inaonesha uwepo wa Kanisa. Na kwa maana hiyo hospitali ya watoto imegeuka kuwa urithi na siyo wa jumuiya ya Roma tu bali ya Italia na kimataifa.

Mada ya wakati ujao ni historia ya watoto

Ilizaliwa namna hiyo hali halisi na thamani ya kutunza na ambayo inatazama leo hii kuelekea wakati ujao. Baba Mtakatifu Francisko amefurahishwa sana juu ya ujumbe waliouchagua katika kuadhimisha Jibilei hiyo, unasema “ wakati ujao ni historia ya watoto”. Na kama alivyo sema  msimamizi wa Kanisa dogo la Hospitali hiyo kuwa mamlaka kimaadili ya watoto wagonjwa na wanaoteseka ndiyo utambulisho zaidi wa kweli wa Hospitali ya Bambino Gesu’. Utambuzi huo uwe ndiyo Gia ya utendaji wao wa kazi ya pamoja kwa maelewano na roho ya kijumuiya, huku wakishinda vikwazo na mitafaruko. Mamlaka ya kimaadili ya watoto inaweza kuwa daima mwaliko wa uaminifu katika wito  asili wa Hospitali hiyo na mantiki ya kufanya mang’amuzi kwa ajili ya uchaguzi endelevu.

Ushuhuda wa mama wa Venezuela na mtoto wake aliyepona

Vile vile Baba Mtakatifu Francisko ameelezea juu ya kusikiliza kwa makini na mshangao wa historia ya mama kutoa Venezuela na mtoto wake Jerson ambaye ameweza kupata tiba aliyokuwa anahitaji katika hospitali hiyo. Anashukuru sana Hospitali hiyo kujifungulia katika dunia na kufanya uamuzi wa kuchukua jukumula kubaba mateso  hayo na kwa ajili ya watoto wanaotoa katika nchi mbalimbali. Na kwa kufanya hivyo Baba Mtakatifu anatambua inavyohitajikia rasilimali ya nyingi ya uchuni na kwa maana hiyo anawashukuru wafadhili amba wanachanhia kutoa katika Mfuko wa Banim Gesu.  Ni matarajio yake kuwa Taasisi za Kimataifa zinaweza kupata namna ya kuhamasisha mikondo ya kibinadamu daima katika afdua wakati wa kusubiri kila nchi iweza na uwezo wa kutoa jibu la mahitaji msingi ya afya ya watu.

Kuhusu baraka na mikono iliyobarikiwa

Baba Mtakatifu Francisko amelezea juu ya neno alilolutumia mama wa Venezuela. Yeye amazungumza juu ya baraka ya Mungu na mikono iliyobarikiwa na mchango ambao ulimpokea na kumtibu mwanae. Madaktari wote, na mabingwa, wauguzi wanatumia mikono kama chombo cha kutibu. Daima wawe na uwezo wa baraka hii ya Mungu katika mikono yao.  Uwezo wao na kutibu  namna hiyo ni zawadi kwa ajili yao na kwa ajili ya watu ambao wanakabidhiwa. Na wakati huo huo madakrita na wauguzi wasikikose kuwa na uhusiano wao wa kitaalumua na ari zao ili waweze daima kuhifadhi ile tabia ya Taasisi hiyo. Inahitaji jitihada ya wote ili Hospitali  ya Watoto Bambino Gesu’ iweza kuonesha umaalum mkuu wa Vatican kwa ajili ya utoto, kwa njia ya mtindo wake wa kutibu kwa upendo walio wadogo, kwa kutoa ushuhuda wa dhati wa Injili ambao umejaa maelewano na kila ambacho Kanisa inafundisha.

Ushuhuda wa muuguzi nchini Siria

Ushuhuda wa muuguzi ambao ameutoa na kutenda katka mfululizo wa utume wa kimisionari kwa muda mrefu nchini Siria , umeonesha wazi mantiki nyinyi ya shughuli za kibinadamu katika hospital ina ule ufunguzi wazi wa dunia. Hii ni uwezekano wa kushirikishana na taaluma fani mbalimbli za ujuzi wa kiafya katika nchi zisizo na fursa. Ni upendo wa fahamu ambao unajenga amani kama alivyosema Mtakatifu Yohane Paulo II ( Hotuba kwa wanasayansi, 12 Novemba 1983). Hii pia inajikita katika utaalam wa Bambino Gesu , kwa kurithisha kil ambacho kinainga na kupokea kwa mabadilishano ya utajiri mkubwa wa kibinadamu. Kila mmoja anamfundisha mwingine kitu. Na ndicho  kinachotokea katika Hospitali ya Bambino Gesu nchi za nje.

Utafiti ni kama jiwe la pembeni

Aidha Mkurugenzi wao wa kisayansi, amesimulia kwa shauku kubwa juu ya hatua utafiti kama jiwe la pembeni la shughuli za Hospitali.  Jinsi utafiti ulivyo bora ndivyo hata huduma ilivyo bora. Haiwezekani kupata tiba bila kuwa na utafiti. Hakuna wakati endelevu katika madawa bila utafiti. Kwa upande huo, Hospitali ya Bambin Gesu kwa kipindi kirefu imekuwa na maono hayo ya wakati ujao kwa kuwa na matokeo muhimu katika uwanja wa vipim vya magonjwa nadra na tiba za magonjwa magumu sana  , kwa njia ya maandeleo ya tiba na usahihi. Baba Mtakatifu anaonesha kushangazwa na shauku yao kwa kila juhudi wanayoifanya ya  kutibu a utafiti. Anatamani kwamba wasiweze kupoteza ule uwezo wa kutambua uso unaoteseka kwa mtoto  na hata kwa urahisi ya hatua moja wapo ya ugunduzi wanao ufanya na kusikiliza kilio cha mzazi hata ndani ya maabara zao.  Fumbo la mateso ya watoto hayachoki kzungumza katika dhamiri zao na kuwa sababu ya jitihada  za kibinadamu na taaluma. 

Hatimaye

Baba Mtakatifu Francisko amesifu kusikiliza yote waliyosimulia juu ya mambo yanavyokwenda katika hospitali pamoja na kwamba hapakosi matatizo lakini ni fursa ya kwamba katika miaka mingine ijayo wanaweza kuendelea kutoa  huduma kwa kila mgonjwa kwa  tiba, na hata mmoja hasiweze kukataliwa. Shughuli hiyo inahitaji rasilimali nanafasi za kutosha. Mahitaji ya utafiti wa kisayansi na kukua kwa mombi ya kusaidia hata katika nchi za nje, itafanya kuwa na ulazima kwa miaka ijayo kuweza kuwekeza katika katika mahitaji  na teknolojia. Hii ni kazi mgumu lakini muhimu ni kwamba daima kuhakikisha  ushirikiano na kusaidiana kwa sababu hospitali iweze kuendelea kuwa maalum kwa ajili ya shughuli ya upendo wa Kanisa. Anawatia moyo wasikate tamaa na wakati huo huo kuwa na ukrimu na busara.Wawe na imani kwa watoto na viongozi wa kimaadili kwa watoto wanaoteseka wakati wakikumbuka daima kwamba: “Yote mliyo fanya mmenitendea mimi (Mt 24,40)

 

 

 

 

 

16 November 2019, 14:12