Tafuta

Vatican News
Mara baada ya katekesi Baba Mtakatifu ametoa salam nyingi kwa mahujaji bila kuwasahau vijana, wazee , wagonjwa na wenye ndoa. Aidha kukumbusha siku kuu ya Malaika Walinzi Mara baada ya katekesi Baba Mtakatifu ametoa salam nyingi kwa mahujaji bila kuwasahau vijana, wazee , wagonjwa na wenye ndoa. Aidha kukumbusha siku kuu ya Malaika Walinzi  (Vatican Media)

Papa:Uwepo wa Malaika walinzi ni sababu ya uhakika wa kusindikizwa na Mungu

Tarehe 2 Oktoba ni siku ya kukumbuka Malaika walinzi,kwa maana hiyo mara baada ya katekesi,Baba Mtakatifu amesema kuwa,uwepo wao uwaongezee waamini nguvu ya kuwa na uhakika kwamba Mungu anawasindikiza katika safari ya maisha yao.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mara baada ya tafakari ya Katekesi yake, tarehe 2 Okotba 2019 Baba Mtakatifu Francisko amewasalimia waamini na mahujaji wote kutoka pande zote za dunia, bila kuwasahau kwa namna ya pekee vijana, wazee , wagonjwa na wanandoa wapya. Kadhalika Baba Mtakatifu Francisko amekumbusha kwamba, leo hii ni maadhimisho ya Siku ya Watakatifu Malaika walinzi. Uwepo wao uwaongezee waamini nguvu ya kuwa na uhakika kwamba Mungu anawasindikiza katika safari ya maisha yao. Awasadie katika kutangaza na kuishi Injili ya Kristo na ili dunia iweze kupyaishwa kwa upendo wa Mungu.

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa sikukuu ya malaika walinzi Okotba  2018 alisema nafasi ya Malaika walinzi katika maisha yetu, bado ni muhimu sana kwa sababu,  si tu wanatusaidia kutembea hija yetu ya maisha vizuri, bali hata kutuelekeza, ni njia gani ya kuweza kufika.  Katika Injili ya Matayo imeandikwa “Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika zao mbinguni sikuzote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni. (Mt 18:1-5,10).

Katika huduma ya Malaika walinzi ipo  hata namna ya kutafakari Mungu Baba, ambaye tunamwomba  atupatie neema ya kuwa na utambuzi huo na ndiyo maana Baba Mtakatifu amethibitisha kwamba Malaika wetu si kuwa yupo nasi tu, bali yeye anatazama Baba Mungu. Malaika anao uhusiano na Yeye. Yeye ni daraja la kila siku, tunapoamka na tunaporudi usiku kitandani kulala, anatusindikiza na kutuunganisha na Baba Yetu wa Mbinguni. Malaika mlinzi ni mlango wa kila siku wa kuelekea juu ili kukutana na Bwana, kwa maana Malaika anatusaidia kwenda katika njia, yeye anatazama Bwana na anajua ni njia gani ya kumfikia Baba. Tusisahau wasindizaji hawa wa njiani. Baba Mtakatifu alihimiza.

02 October 2019, 13:00