Tafuta

Vatican News
Roho Mtakatifu awajalie maaskofu katika Sinodi yao ili kupata njia mpya za unjilishiji kwa ajili ya Amazonia Roho Mtakatifu awajalie maaskofu katika Sinodi yao ili kupata njia mpya za unjilishiji kwa ajili ya Amazonia  (Vatican Media)

Sinodi ya kutafuta njia mpya za uinjilishaji na uhamasishaji!

Kwa wiki tatu Mababa wa Sinodi wanaungana pamoja na mfuasi wa mtume Petro ili kutafakari juu ya utume katika Kanisa la Kanda ya Amazonia,juu ya uinjilishaji na juu ya uhamasishaji wa ekolojia fungamani.Baba Mtakatifu anawaomba waamini wote ili kuwasindikiza kwa sala katika tukio hii la Kanisa na waweza kuishi muungano kindugu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko kabla ya Sala ya  Malaika wa Bwana Jumapili tarehe 6 Oktoba 2019  kwa waamini waliounganika katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican amekumbusha kuwa muda mfupi katika Kanisa Kuu la Mtatifu Petro wamefanya maadhimisho ya Ekaristo ikiwa ndiyo mwanzo wa ufunguzi wa Sinodi maalum ya Maaskofu kwa ajili ya Kanisa la Amazonia. Kwa wiki tatu anasema, Mababa wa Sinodi wanataungana pamoja na mfuasi wa mtume Petro ili kutafakari juu ya utume wa Kanisa la Kanda ya Amazonia, juu ya uinjilishaji na juu ya uhamasishaji wa ekolojia fungamani.

Maombi ya waamini kwa ajili ya Sinodi ya Maaskofu

Baba Mtakatifu Francisko kufuatia na tukio hilo la Sinodi ya  Maaskofu, anawaomba waamini wote ili kuwasindikiza kwa sala katika tukio hili la Kanisa na ili waweza kweli kuishi muungano  wa kindugu huku wakiongozwa na maongozi ya Roho Mtakatifu na  ambaye daima awaoneshe njia kwa ajili ya kushuhudia Injili.

Shukrani kwa mahujaji toka pande za dunia

Aidha Baba Mtakatifu Francisko amewashukuru mahujaji wote waliofika kutoka Italia na sehemu mbali mbali za dunia. Akiwataja baadhi  waamini kutoka Heidelberg, Ujerumani , Poland, wanafunzi kutoka Ujerumani na wengine kutoka Argentina. Amekumbuka mahujaji kutoka Castelli Romani waliofanya matembezi mshikamani wa amani kama vile hata wale wa  Camisano Vicentino. Na kwa wote wanawatakia Dominika njema na kuwaomba kama kawaida yake  wasisahu kusali kwa ajili yake.

06 October 2019, 14:40