Misa ya ufunguzi wa Sindo ya Maaskofu kuhusu Amazonia katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican Misa ya ufunguzi wa Sindo ya Maaskofu kuhusu Amazonia katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican 

Maaskofu wainue mikono yao juu na kuifungua kwa ndugu!

Tarehe 6 Oktoba 2019 Baba Mtakatifu Francisko amefungua Sinodi ya Maaskofu kuhusu Amazonia.Katika mahubiri yake amesisitizia kuhusu uaminifu katika mapya ya roho ya busara.Maaskofu wamepokea zawadi ya moto wa Roho ili wautoe kwa wengine.Watu wengi huko Amazonia wanabeba misalaba mizito na wanasubiri kitulizo cha upendo wa Kanisa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 6 Oktoba 2019 ameongeza Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, lililopambwa kwa rangi nzuri za waamini wa Mungu, kutoka pande zote za dunia hasa asilia ikiwa ndiyo misa ya ufunguzi wa Sinodi Maalum ya Maskofu kuhusu Amazonia, Sinodi iliyotarajiwa sana. Katika mahubiri yake kwa kuongozwa na masomo ya siku amesema, "Mtakatifu Paulo aliye mmisionari mkubwa katika historia ya Kanisa anatusaidia kufanya Sinodi hii kwa “kutembea pamoja”, kama anavyo andika Timoteo, na utafikiri anatueleza sisi Wachungaji katika huduma ya watu wa Mungu. Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na mahubiri anasema awali ya yote, “nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu (2 Tm 1,6)”,  na kwa maana hiyo, anaongeza, wao ni maaskofu  kwa sababu wamepokea zawadi ya Mungu. Wao hawakutia sahini ya mkataba na wala kuwa na mkataba mikononi mwao wa kazi, bali kuupokea kichwani ili mara tu waweze kuinua mikono yao inayoomba kwa Bwana na mikono hiyo iweze kufunguliwa wazi kwa ndugu. Wamepokea zawadi ili waweze kuwa zawadi na kuitoa kwa wengine. Zawadi hainunuliwi, wala kuibadilisha na kuiuza; inapokelewa na ili itolewe. "Ikiwa tuna binafsisha na ikiwa ni kujiweka katikati, badala ya zawadi hiyo, Baba Mtakatifu amesema, wachungaji wanakuwa ni wafanyakazi na kuifanya zawadi hiyo iwe kitu na kupoteza iwe kitu bure huku ikiishia katika kujihudumia binafsi na siyo kuhudumia Kanisa.

Ili maisha yawe zawadi, hudumia

Baba Mtakatifu Franciskio anasema maisha kwa ajili ya kuwa zawadi iliyopokolewa ni kwa ajili ya kuhudumia. Injili imekumbusha juu ya kuwa “watumishi wasiokuwa na faida (Lk 17,10: ni kielelezo ambacho kinamaanisha kuwa watumishi wasio na faida. Maana yake ni kwamba hawakufanya kazi ili kufikia kile chenye kuwa na faida, lakini kwa sababu wamepewa bure na watoe bure(Mt 10,8).Baba Mtakatifu Francisko amesema kwamba furaha yao yote  itakuwa  ni katika  kuhudumia kwa sababu walihudumiwa na Mungu aliyejifanya mtumishi wa wao. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anawashihi wahisi wito huo wa kuhudumia kwa kijikita kuwa kiini cha zawadi ya Mungu.

Kuwa na uaminifu kwa zawadi iliyo pokelewa

Na ili kuweza kuwa waaminifu katika wito wa utume wao  Mtakatifu Paulo amekumbusha zawadi yenye kichocheo. Baba Mtakatifu Francisko anafafanua kwamba : Neno lililotumika ni lile la kushangaza Kuchochea ina maana ni kutoa maisha kwenye moto (anazopurein). Zawadi tuliyoipokea ni moto, ni upendo unachoma kutoka kwa  Mungu na ndugu. Moto hauwezi kuongezeka nguvu peke  yake la sivyo , unazimika,na kufunikwa majivu.  Na kwa maana nyingine iwapo tunabiki hivyo huki tukiitikia ndiyo tu na kuona kwamba kika kitu kimeeoleka hivyo zawadi hiyo inatoweka, inafunikwa na majivu ya hofu na wasiwasi wa kulinda nafasi. Lakini hakuna namna yoyote Kanisa linaweza kuweka vikwanzo vya kubaki na kuhifadhi kwa wale ambao wamekwisha tambua Injili. Ari mpya ya kimisionari ni ishara wazi ya ukomavu wa jumuiya ya Kanisa ( Benedikto XVI , katika Wosia wa Verbum diminum 95) Yesu hakuja kwa ajili ya kuleta upepo mwanana kama wa jioni, bali moto katika dunia!

Moto unatoa uhai wa zawadi ni Roho Mtakatifu

Moto unaoweka uhai wa zawadi ni Roho Mtakatifu ambaye ni mpaji wa zawadi. Kwa maana hiyo Mtakatifu Paulo anaendelea kusema : “Ilinde ile amana nzuri kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu (2 Tm 1,14).  Na pia Mungu hakutupatia roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa busara (2 Tm 1,7). Baba Mtakatifu ametoa mfano, “mwingine anafikiri busara ni fadhila kama ‘mpaka’, ambao unazuia kila kitu ili kutokosea. Hapana! busara ni fadhila ya kikristo, ni fadhila ya maisha na zaidi fadhila ya serikali. Na tumepewa roho hiyo ya busara. Paulo anaweka neno busara kinyume na woga. Je kuwa na busara ya Roho maana yake  nini? Katika Katekesimu ya Kanisa katoliki inakumbusha kuwa , busara isichanganywe na hofu, au woga, bali ni fadhila inayoiandaa akili ya kawaida kupambunua katika mazingira yote mema yetu ya kweli na kuchagua njia zitakiwazo kuyapata (n.1806). Busara siyo kutokuwa na uhakika wala tabia ya kujilinda.

Fadhila ya kichungaji katika kuhudumia na busara

Fadhila ya Kichungaji ili kuhudumi na busara, inatambua kung’amua mambo mapya ya Roho. Kwa maana hiyo kuchochea zawadi katika moto wa Roho ni kinyume na kukaa au kwenda mbele bila kufanya kitu. Kuwa waainifu katika mapya ya Roho ni neema ambayo Baba Mtakatifu Francisko amethibitisha kuiomba katika sala. Yeye anayefanya mambo yote kuwa mapya aweze kujalia zawadi yake ya ari ya busara: awauishie katika Sinodi yao katika upyaisho wa safari kwa ajili ya Kanisa la Amazonia ili moto wa utume usizimike.

Moto unaorarua unatoka duniani na siyo kwa Mungu

Moto wa Mungu kama unavyoonesha katika tukio la kichaka kinachowaka moto, lakini hakiungui (Kut 3,2). Ni moto wa upendo unaoangaza  unaotia joto na kutoa maisha, siyo moto unaowaka na kurarua. Ikiwa hakuna upendo na bila heshima ,wanararua watu na tamaduni lakizi siyo moto wa Mungu, bali ni katika dunia. Pamoja na hayo Baba Mtakatifu amebinisha kwamba ni mara ngapi zawadi ya Mungu haikutolewa namna hiyo inavyotakiwa badala yake kulazimisha; ni mara ngpi kumekuwapo na ukoloni, badala ya uinjilishaji! Mungu anavumilia tamaa za koloni mpya. Moto unaowashwa kwa ajili ya masuala binafsi na ambao unaharibu, kama vile ule wa hivi karibuni uliochoma Amazonia, siyo moto ule wa Injili anasisitiza Baba Mtakatifu Francisko. Moto wa Mungu ni wenye joto linalovutia na kuunganisha katika umoja. Unakuzwa kwa kushirikishana na siyo kutafuta faida. Moto wa kurarua, badala yake unawashwa wanapotaka kupeleka mawazo binafsi, kikundi, kuchoma tofauti ili kutaka kila kitu kifanane, amethibitisha Baba Mtakatifu.

Lazima kupenda hadi kifodini

Baba Mtakatifu aidha anasisitiza juu ya suala la kuchochea moto, kuupokea kwa hekima na ari ya Roho na kuwa waaminifu katika mapya; na kwamba Mtakatifu Paulo katika maneno yake ya mwisho anatoa ushauri kwamba “msiwe na aibu kutoa ushuhuda, bali kwa nguvu ya Roho mteseke nami kwa ajili ya Injili” , na kwa maana nyingine ni kusmea kwamba kuishi kwa ajili ya Injili, anasisitiza Baba Mtakatifu. Tangazo la Injili ni mantiki msingi kwa ajili ya maisha ya Kanisa. Baadaye kidogo Paulo aliandika “mimi niko karibu kabisa kutolewa dhabihu (2Tm 4,6)”. Kutangaza Injili ni kuishi kwa dhabihu, ni kushuhudia hadi mwisho,; ni “kuwa na hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote, ( 1 Kor 9,22)”, ni kupenda  hadi kifodini. Kwa hakika Mtume wa watu  anasisitiza ni kuhudumia Injili na siyo kwa nguvu za ulimwengu, lakini kwa nguvu tu za Mungu, kubaki daima kwa upendo mnyenyekevu, kwa utambuzi kuwa  njia moja tu ya kuweza kupata maisha ni kuyapoteza kwa ajili ya  upendo. Baba Mtakatifu Francisko anamshukuru Mungu ka sababu ya Baraza la Makardinali  ambao pia baadhi ni wafiadini walioonja katika maisha msalaba wa kifodini.

Ni kuanzia msalabani ili kuhisi kutoa maisha

Aidha anasema ni kuanzia katika msalaba  ili kuhisi kila mmoja kutoa maisha. Watu wengi wa Amazonia wanabeba misalaba mizito na wanasubiri kitulizo cha ukombozi wa Injili ynye uhuru wa upendo wa Kanisa. Aidha Baba Mtakatifu Francisko ameomba watazame kwa pamoja Yesu msulibiwa katika moyo wake uliochowa kwa ajili yetu. Ni kuanzia zawadi inatolewa na Roho Mtakatifu anajipyaisha (Yh 19,30). Ndugu kaka na dada wa Amazonia wametoa amaisha yao. Baba Mtakatifu ameomba kurudia maneno ya mpendwa Kardinali  Hummes, aliye msimulia kwamba, kila mara anapofika katika mji mdogo wa Amazonia anakwenda makaburini  kutafuta makaburi ya wamisionari. Ishara ya Kanisa kwa ajili ya wale wote waliotoa maisha yao kwa ajili ya Amazonia.  Kwa upande wao na kwa wale wote ambao wanaendelea kutoa maisha yao.

06 October 2019, 11:50