Tafuta

Vatican News
Kuwa na ujasiri,bila hofu:twende kwa kila mtu, na kuwakumbatia wote bila ubaguzi ndiyo mwaliko wa Baba Mtakatifu wakati wa mahubiri katika fursa ya siku ya kimisionari duniani 2019 Kuwa na ujasiri,bila hofu:twende kwa kila mtu, na kuwakumbatia wote bila ubaguzi ndiyo mwaliko wa Baba Mtakatifu wakati wa mahubiri katika fursa ya siku ya kimisionari duniani 2019  (Vatican Media)

Baba Mtakatifu Francisko:Nenda na upendo kuwakumbatia wote bila ubaguzi!

Kuweni jasiri.Yeye anasubiri sana kutoka kwako!Bwana ana wasiwasi kwa ajili ya wale ambao hawajuhi kuwa wanapendwa na Baba,ndugu ambao alitoa maisha na Roho Mtakatifu.Je unataka kutuliza wasiwasi wa Yesu?Nenda na upendo kwa wote,kwa sababu maisha ni thamani ya umisionari.Siyo mzigo mzito,bali ni zawadi ya kutoa.Ni mahubiri ya Papa Francisko.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 20 Oktoba 2019 amedhimisha Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican ambapo, mama Kanisa anaadhimisha Siku ya Kimisionari duniani kwa mwaka 2019 inayoongozwa na kauli mbiu sawa sawa na ile ya Mwezi maalum, Oktoba wa Kimisionari isemayo:"Mmebatizwa na kutumwa”. Kanisa la Kristo katika utume wa kimisionari duniani, ni  kauli inayoangazia Maadhimisho ya Miaka 100 tangu Papa Benedikto XV alipotangaza Waraka wake wa Kitume uitwao"Maximum Illud". Baba Mtakatifu akianza mahubiri yake amesema kufuatia na masomo yaliyosomwa ninataka kufafanua kwa maneno matatu:“nomino”, “kitenzi” na “kivumishi”. Nomino ni mlima, kwani anauzungumzia nabii Isaya, akitabiri  juu ya mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi ( Is 2,2). Suala la mlima pia linazungumzwa katika Injili kuwa Yesu mara baada ya kufufuka, anaelekeza wafuasi wake mahali pa kukutana katika mlima wa Galilaya, na hivyo kwa hakika  katika Galilaya yenye watu wengi wa mataifa, yaani Galilaya ya mataifa ( Mt 4,15).Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na mahubiri amesema kwa hakika utafikiri mlima ndiyo mahali ambapo Mungu napenda kukutana na ubinadamu wote. Ni mahali pa kukutana na sisi, kama Biblia inavyoonesha kutoka Sinai hadi Karmeli,  na kufikia kwa Yesu, ambaye alitangaza Heri juu ya mlima, alijibadilisha sura katika mlima  wa Tabor, alitoa maisha yake  juu ya Karvario na kupaa mbinguni katika Mlima wa Mizeituni. Mlima ni maahali pa mikutano mikubwa kati ya  Mungu na mtu na pia ni sehemu ambayo Yesu alikuwa anatumia masaa mengi anasali (Mk 6,45) ili kuunganisha  kati ya dunia na Mbingu; sisi ndugu zake na Baba.

Je nini maana ya mlima

Je mlima kwetu sisi una maana gani ?  Una maana  kwamba, tumeitwa kumkaribia Mungu na wengine; Mungu aliye juu, katika ukimya, katika sala, kwa kujiweka mbali na magumzo na masengenyo yanayochafua. Lakini hata kukaribia wengine ambao kutoka mlimani na kuwatazama kwa matarajio ya Mungu ambaye anawaita watu wote; kutoka juu kwenda kwa wengine inaonesha upamoja na kugundua kuwa maelewano ya uzuri tumepewa tu kwa sababu ya upamoja.  Haha hivyo Baba Mtakatifu amesisitiza kwamba Mlima unatukumbusha kuwa, kaka na dada hawabaguliwi, bali wanakumbatiwa kwa mtazamo na zaidi katika maisha. Mlima unafungamanosha Mungu na ndugu katika mkumbatio mmoja katika sala. Katika mlima unatupeleka juu mbali na mambo mengi yanayopita; unatualika kugundua yaliyo muhimu na yanadumu  yaani Mungu na ndugu. Utume wa kimisionari unaanzia mlimani, na ndiyo hapo unagundua kile kilicho na  maana. Baba Mtakatifu anasema kwa maana hiyo katika moyo wa Mwezi wa Kimisionari tuombe ili  kujua ni kitu gani ni muhimu kwangu katika maisha? Je ni vilele gani ambavyo ninatazamia?

Kitenzi kinasindikiza nomino ili kupanda mlimani

Baba Mtakatifu  Ffrancisko akiendelea na ufafanuzi wake kuhusu mambo matatu aidha anasema kitenzi kinasindikiza nomino ambayo ni mlimani ili kuupanda kama anavyoshauri nabii Isaya kuwa: “njooni twenda juu mlimani kwa Bwana (Is 2,3). Na kwa maana hiyo hatukuzaliwa kwa ajili ya kukaa duniani ili kufurahia mambo yaliyosimama, bali tumezaliwa ili kuyafikia yaliyo ya juu, kukutana na Mungu na ndugu. Lakini ili kufanya hivyo ni lazima kuupanda, lazima kuacha maisha yaliyolala  ili  kupambania dhidi ya nguvu za ubinafsi na  kutimiza njia  ile ya kutoka ndani ya ubinafsi. Kupanda mlima kwa maana hiyo ni gharama, lakini ndiyo namna ya kuweza kuona kila kitu vizuri. Ni kama vile unapopanda mlimani  kufika kileleni unaweza kuona vizuri hali halisi ya chini na kutambua kuwa usingeweza hivyo iwapo usingepitia njia hiyo ya mpando.

Kupunguza mizigo mizito ili kupanda katika mlima wa Bwana

Na kama jinsi ilivyo kwamba huwezi kupanda mlimani iwapo umebeba mambo mazito, Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa ndivyo ilivyo hata katika maisha kwamba lazima upunguze uzito wa mambo yasiyo ya lazima. Na ndiyo hata siri ya utume wa kimisionari. Ili kuweza kusafiri ni lazima uache ili kutangaza, na  lazima ujinyime. Tangazo linaloaminika  iwapo halifanywi kwa njia ya maneno mazuri bali kwa njia ya  maisha mema; Maisha ya huduma yanayotambua kujinyima mambo mengi binafsi na  ambayo mara nyingi hufanya moyo kuwa mdogo na ajifunge binafsi; maisha ambayo yanaondokana na mambo yasiyo na maana  ndiyo yenye kukupatia muda kwa ajili ya Mungu na wengine. Tunaweza kujiuliza; je kupanda mlima kwangu kukoje? Je ninatambua kujikana mizigo mizito na isiyo na faida katika ulimwengu huu kwa ajili ya kwenda juu ya mlima wa Bwana?

Kitenzi cha kupanda mlima ni kama vile kufika

Iwapo mlima unatukumbusha chenye  kuwa na umuhimu, yaani Mungu na ndugu, kitenzi cha kupanda mlimani ni kama vile  kufika na ndiyo neno la tatu  ambalo limesikika kwa nguvu zote, anasema Baba Mtakatifu Francisko. Kivumishi” kinachovuma katika somo ni kuhusu “ watu wote. Alikuwa amesema Isaya  (2,2) kwamba “Watu wote” na neno hilo limerudiwa katika Zaburi. "Mungu anataka watu wote waokolewe”; anaadika Mtakatifu Paulo (1 Tm 2,4)  na "enendeni na muwe wafuasi wa watu wote”,  Yesu katika Injili anasema ( Mt 28,19). Yesu anasisitiza neno la “Wote” , kwani Yeye anajua kuwa sisi ni wenye vichwa vigumu ambao wanarudia  kusema “ mimi “ na “ Sisi”; kwa maana ya kusema “ mambo yangu, watu wetu, jumuiya yetu, …., Lakini yeye hachoki kurudia kusema “ wote”. Ni wote kwa sababu hakuna yoyote anabaguliwa katika moyo wake na   wokovu wake; wote kwa sababu ili moyo isiende mbali na mipango ya kibinadamu, kwenda  mbali na mambo yanayojikita juu ya ubinafsi usiompenda Mungu. Wote kwa sababu kila mmoja ni tunu msingi. Na maana ya maisha ni kujitoa tunu hiyo kwa wengine. Na ndipo hapo utume wa kimisionari wa kupanda juu ya mlima ili kusali kwa ajili ya wote na kushuka kutoka mlimani kwa ajili ya kuwa zawadi ya wote.

Kupanda na kushuka

Ni kupanda na kushuka, kwani Mkristo daima yuko katika mwendo wa kutoka nje. Kwenda kwa hakika ndiyo neno kuu la Yesu katika Injili.  Siku zote tunakutana na watu wengi, lakini tunaweza kujiuliza,  je tunakwenda kukutana na watu tunaokutana nao? Tunatoa mwaliko kama wa Yesu au tunafanya shughuli zetu tu? Mashuhuda wa Yesu hawana deni kamwe la kuwahabarisha wengine, lakini wana deni la upendo kwa yule hasiyemjua Bwana. Shuhuda wa Yesu anakwenda kukutana na wote, si tu kwa ndugu zake binafsi, au katika kikundi chake. Yesu anasema hata kwako kuwa  "nenda, usipoteze fursa ya kushuhudia! Kaka na dada, Bwana anasubri kutoka kwako ule ushuhuda ambao hakuna yoyote anaweza kutoa katika nafasi yako. Baba Mtakatifu Francisko amesema" ninataka mbingu iweze kutambua, kuwa kuna  neno lako, ujumbe ule wa Yesu ambaye Mungu anatamani kusema duniani kwa njia ya maisha yako. (…) kwa njia ya thamani ya utume wako  wa kimisionari na hautapotea ( Wosia wa Gaudete et exultare,24)

Fundisho gani anatupatia leo hii ili kwenda kwa Bwana?

Ni mafundisho gani Bwana anatupatia ili wote twende kwake? Ni moja tu  anabainisha Baba Mtakatifu na rahisi sana la kujifanya wafuasi. Lakini kuweni  makini,  anaonya -ya kuwa wafuasi wake  tu na siyo kwa watu, Kanisa linatangaza vizuri tu iwapo linaishi kama mfuasi. Mfuasi amfuata kila siku Mwalimu wake , huku  akishirikishana na wengine furaha ya kitume.  Yeye halazimishi au kufanya propaganda, bali anashuhudia, kwa kijikita katika nafasi sawa sawa na mfuasi kwa mfuasi, ya kujitoa kwa upendo ule ule ambao tumepokea. Huo ndiyo utume wa kwanza wa kimisionari, wa kutoa hewa nzuri itokayo juu kwa wale wanaoishi kwenye dunia iliyochafuka: kupeleka amani diniani inayojaza furaha mara moja tunapokutana na Yesu juu ya mlima na katika sala; kuonesha kwa njia ya maisha, hadi kufikia kuelezea maneno ambayo Mungu anawapenda wote na hachoki kamwe mtu yoyote.

Baba Mtakatifu Francisko kwa kuhitimisha  amesema kuwa kila mmoja ni mmisionari duniani (Evangelii gaudium, 273).  Sisi tupo hapa kwa ajili ya kushuhudia, kubariki, kufariji, kuonesha uzuri wa Yesu. “Kuweni jasiri”,  amehimiza, “Yeye anasubiri sana kutoka kwako! Bwana ana wasiwasi mkubwa  kwa ajili ya wale ambao hawajuhi kuwa wanapendwa na Baba, ndugu ambao alitoa maisha na Roho Mtakatifu. Je unataka kutuliza wasiwasi wa Yesu? Nenda na upendo kuelekea kwa wote, kwa sababu maisha ni thamani ya umisionari. Siyo mzigo wa kuelemewa, lakini ni zawadi ya kutoa. Kuwa na ujasiri, bila hofu: twende kwa kila mtu!

 

20 October 2019, 11:00