Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu ameshiriki afla ya ufunguzi maonyesho kuhusu makao, umbo, desturi za mataifa na  wanadamu (Ethnological) Baba Mtakatifu ameshiriki afla ya ufunguzi maonyesho kuhusu makao, umbo, desturi za mataifa na wanadamu (Ethnological)  (Vatican Media)

Baba Mtakatifu:uzuri ni sanaa dhidi ya utamaduni wa chuki!

Baba Mtakatifu Francisko ameshiriki hafla ya uzinduzi wa maonyesho ya sanaa za utamaduni kuhusu Mater Amazonia,katika Jumba la Makumbusho Vatican ambayo imepewa jina Anima mundi ambapo katika hotuba yake amesema uzuri unaunganisha na kutualika kuishi udugu ili kupinga utamaduni wa chuki,ubaguzi wa rangi na utaifa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Nyumba hai inayokaliwa na kufunguliwa kwa wote, milango yote iliyofunguliwa kwa watu wote duniani: mahali ambapo kila mmoja anaweza kuhisi anawakilisha na mahali mabapot mtazama wa Kanisa unaelewa kwa dhati kama mtazamo ambao haujuhi kubagua. Ndiyo maneno ya Baba Mtakatifu Francisko, baada ya salam kwa Kardinali Giuseppe Bertello Rais wa Utawala wa jiji la Vatican, wakati wa uzunduzi wa mchanganyiko wa sanaa za makumbusho za makabila zilizopewa jina: “Anima Mundi” unayowakilisha kama wito ndani ya Jumba la Makumbusho Vatican.   Anayeingia anapaswa ahisi kuwa nyumba ile ina nafasi hata kwa ajili yake,  kwa ajili ya watu wake, tamaduni zake na utamaduni wake, kama ule wa Ulaya, India, China na kama ilivyo hata uasilia wa msitu wa Amazonia, au Congo, Alaska au Jangwa la Austaria na visiwa vya Pasifiki. Watu wote wako mahali hapo, katika kivuli cha Cupola ya Mtakatifu Petro, karibu na moyo wa Kanisa na wa Papa. Na hiyo ni kwa sababu sanaa siyo kitu kichokatwa mizizi yake, badala yake, sanaa inazaliwa ndani ya mioyo ya watu na ndiyo ujumbe kutoka ndani ya moyo wa watu kwenda kufika ndani ya moyo wa watu wengine, amesisitiza Baba Mtakatifu Francisko.

Eneo la majadiliano na makutano;kazi ya sanaa dhidi ya chuki na ubaguzi

Kila mmoja anayeingia katika eneo hili, lazima akute nafasi kubwa inayomsubiri ya majadiliano, yenye ufunguzi wa mwingine na kukutana. Ni lazima  ahisi hata kwamba  sanaa hiyo ina thamani yake, ina hadhi sawa na yake na imelindwa kwa shauku ile ile ambayo inajisimamia kwa kazi bora za sanaa za nyakati mpya au sanamu za kutokufa za Wagiriki na Warumi, ambazo zinavutia mamilioni ya watu kila mwaka. Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na hotuba yake  amesifu wasanii walivyopamba, wataalam wa ujenzi, wafanyakazi na mafundi, katika ishara ya uwezo ambao kila wakati ni nzuri kwa taasisi za kikanisa pia kutoa shukrani kwa maonyesho maalum ya Amazonia, na ambayo yamepewa jina la Mater Amazonia - Pumzi ya kina ya ulimwengu. Baba Mtakatifu Francisko amewatia moyo wa kutazama kila tamaduni, mwingine na kuwa na ufunguzi wa roho na kwa wema huku uzuri ukishinda vile virus ambavuo vinaatarisha udugu. Uzuri unaunganisha. Unatualika kuishi udugu wa kibinadamu, ili kupingana na utamaduni wa chuki, wa ubaguzi na utaifa ambao daima unashamiri. Hizi ni tamaduni za kuchagua, tamaduni za idadi iliyofungwa. Miezi michache iliyopita, Baba Mtakatifu aidha amesema baadhi ya kazi nyingine za sanaa kutoka Peking zililetwa na Wachina na kuwekwa katika jumba hilo. Na kabla ya hizo zilikuwa zimefika nyingine kutoka nchi za Kiislam ... Ni mipango mingapi inayoweza ili sanaa iendelea kuwa na uwezo wa kushinda hata vizuizi na umbali?

Sanaa ya tamaduni zote inaweza kufanya isikike sauti ya Mungu

Akishukuruviongozi wakuu kuhusu Sanaa ya Anima Mundi, Padre Nicola Mapelli, mmissonari wa PIME, Baba Mtakatifu Francisko amehitimisha akionesha matarajio yake kwamba maonyesho hayo yanaweza kuhifadhi kila wakati utambulisho wake maalum na ukumbusho wa  kila mtu juu ya thamani ya maelewano na amani kati ya watu na mataifa. Na Sanaa iliyokusanywa hapo inaweza kusikika sauti ya Mungu kwa wale wote watakaoitembelea na kuiona.

Asili ya maonesho ya makao,umbo,desturi za mataifa na za wanadamu

Asili ya maonyesho kuhusu makao, umbo desturi za mataifa na za wanadamu (Ethnological) ilianza kunako  mwaka 1925 ambapo kwa mujibu wa Papa Pio XI aliweza kuandaa mjini Vatican ili kuweza kuonyesha tamaduni mbalimbali, sana na tasaufi za watu wote. Mwisho wa maonyesho na tukio la muda likageuka kuwa maonyesho ya kudumu. Na ndiyo ilivyozaliwa Maonyesho ya kumbukumbu ya kimisionari kuhusu makao, umbo, desturi za mataifa na za wanadamu (Ethnological) lililopo katika Jumba la Laterano hadi kufikia kuhamishwa kwanza kwenye miaka ya sabini kwenye makao ya sasa ndani ya Jumba la Makumbusho Vatican. Hata hivyo wanasema kwamba, nafasi hiyo kwa wakati, itatembelewa na maelfu ya kazi kutoka ulimwenguni kote. Hata kabla ya upyaisho huo, mkusanyiko wa vitu vilivyoonyeshwa kwenye Jumba la kumbukumbu ya  utamaduni mwingi (Ethnological) lilikuwa tofauti sana. Leo hii  maelfu ya uvumbuzi mwingi wa kihistoria umeongezeka hata na  zawadi nyingi za sasa ambazo Baba Mtakatifu, na ambazo ni kushuhudia utamaduni mkubwa wa roho ya Asia na ustaarabu wa kabla ya Colombia na Uislamu. Na pia uzalishaji wa sanaa za watu wa Kiafrika na wenyeji wa Oceania, Australia na watu asilia wa Amerika.

19 October 2019, 09:30