Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko anaombea taifa la Iraq kusitisha maandamano makali ambayo yamekwisha sabisha vifo na majeruhi wengi nchini humo kuafuatia na ufisadi na ukosefu wa ajira Baba Mtakatifu Francisko anaombea taifa la Iraq kusitisha maandamano makali ambayo yamekwisha sabisha vifo na majeruhi wengi nchini humo kuafuatia na ufisadi na ukosefu wa ajira  (AFP or licensors)

Sala ili kusikiliza kilio na kutafuta suluhisho nchini Iraq

Mara baada ya katekesi ya Baba Mtakatifu kwa waamini na mahuji katika kiwanjia ya a mtakatifu Petro ameomba kusali kwa ajili ya amani Iraq,kutokana maandamano makubwa dhidi ya ufisadi na ukosefu wa ajira na kusababisha vifo na majeruhi.Anawasihi viongozi wa nchi hata jumuiya ya kimataifa kutafuta njia za majadiliano baada ya miaka hii ya vita na ghasia.

Na  Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya katekesi yake tarehe 30 Oktoba 2019 kwa waamini na mahuji kwenye kiwanja cha mtakatifu Petro, amewasalimia wote na kutoa wito mkubwak ufuatia na hali halisi ya ghasia na vurugu zinzaoendelea ulimwenguni na kwa namna ya pekee nchini Iraq. Anawaombea watu wote ili waweze kuwa na maisha yenye hadhi na utulivu, majadiliano na upatanisho na haki ya kutafuta suluhisho ili kufikia amani na msimamo wa nchi ya Iraq nzima.

Maandamano ya kupinga ufisadi 

Baba Mtakatifu  Francisko akifikiria nchi hii ya Iraq na ambayo kwa sasa unaendelea na maandamanotangu mwanzoni mwa Mwei Oktoba kwa ajili ya kupinga hali halisi ya ifisadi na ukosefu wa ajira, anaomba hali hii imeweze kuisha, kwa maana ghasia hizi zimekwisha sababisha vifo vingi na majeruhi. Hadi sasa ni zaidi  ya waandamanaji 250 waliouwawa huko Baghdad na katika miji ya Kusini mwa nchi.

Watu wa Iraq wasaidie Jumuiya ya Kimataifa

Kutokana na hiyo Baba Mtakatifu Francisko anatoa  salam za rambi rambi kwa wanafamilia na waathrika wote majeruhi na kuonesha ukaribu wake. Na wakati huo huo anawaalika mamlaka ya nchi kusikiliza kilio cha watu ambao wanapaza sauti wakiomba maisha yenye hadhi na utulivu.  Anawashauri watu wote wa Iraq wajikite kusaidia haya Jumuiya ya kimataifa katika kufuata njia ya majadiliano na upatinisho wakati wanatafuta suluhisho la haki katika changamoto  na matatizo ya nchi. Anawaombea watu wote wanaoteseka ili waweze kupata amani na msimamo wa nchi baada ya miaka mingi ya vita, vurugu na kuteseka sana.

 

30 October 2019, 13:00