Baba Mtakatifu Francisko anasema, katika Siku ya masikini ingekuwa vizuri ninyi mkaenda na mmoja akawapeleka ili kuweza kukaa pamoja na Mama wa Yesu. Baba Mtakatifu Francisko anasema, katika Siku ya masikini ingekuwa vizuri ninyi mkaenda na mmoja akawapeleka ili kuweza kukaa pamoja na Mama wa Yesu.  

Baba Mtakatifu:nendeni nyote Lourdes kukaa na mama Maria,mama wa Yesu!

Umetangazwa ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko katika ukurasa wa Facebook wa Chama cha Ndugu,unaohusiana na maandalizi ya mkutano uliandaliwa huko Lourdes ambao utafanyika kuanzia tarehe 14 -17 Novemba,siku inayoangukia mwaka tatu wa maadhimisho ya Siku ya Masikini Duniani,iliyotangazwa na Baba Mtakatifu Francisko 2017.

Na Sr. Angela rwezaula – Vatican

Kuanzia tarehe 14-17 Novemba 2019 unatarajiwa kufanyia mkutano huko Lourdes nchini Ufaransa uitwao “Raduno Fratello 2019” yaani “mkusanyiko wa ndugu 2019” ulioandaliwa na Chama cha “Fratello” yaani “Ndugu “ kinachojikita na masuala ya kuhamasisha shughuli zinazotozama kwa ukaribu maskini zaidi na waathirika wa kila aina, katika fursa hii ya kuadhimisha mwaka wa 3 wa Siku ya Masikini duniani, ambao sasa unafanyika kila tarehe 17 Novemba ya kila mwaka, siku  iliyanzishwa  na Baba Mtakatifu Francisko kunako mwaka 2017. Kufuatia na maandalizi hayo, Chama cha “Ndugu” kupita ukurasa wao wa Facebook, wametangaza ujumbe kwa njia ya Video wa Baba Mtakatifu Francisko ambao amewatumia Chama hicho kikiwa katika harakati za maandalizi.

Ujumbe wa  Baba Mtakatifu anasema kuwa:

Ninayo kumbukumbu za Siku ya Masikini Duniani ambayo ilifanyika hapa Roma. Hapa ilikuwa kijimbo lakini wote wamekuwa na utambuzi zaidi wa umasikini na ambao hata Yesu mwenyewe aliuishi katika kipindi ambacho yeye aliwekwa pembeni na hakukubaliwa.  Na nyinyi mnaishi umaskini ambao una chanzo chake   na sababu zake,  ambazo mnazifahamu. Lakini ni vizuri kuungana na kukaa wote pamoja”. Aidha Baba Mtakatifu anaongeza kusem: “Ninatambua kuwa, Siku ya Masikini duniani itafanyika huko Lourdes Novemba 2019, kwa maana hiyo ingekuwa vizuri ninyi mkaenda na hata mmoja akawapeleka ili kuweza kukaa pamoja na Mama wa Yesu. Na Bikira Maria awalinde, awatunze ninyi nyote na mkae na Mama wa Yesu ambaye pia alikuwa masikini na anatambua lugha ya umasikini. Na kwa maana hiyo furahini na enendeni katika Siku ya Masikini huko Lourdes. Ninawabariki na kuwasindikiza nikiwa hapa. Asante”. Amehitimisha Ujumbe wake kwa njia ya video uliotangazwa katika ukurasa wa Facebook wa Chama cha “Ndugu”.

 

17 October 2019, 13:07