Tafuta

Tarehe 1 Oktomba yamefanyika maadhimisho ya masifu ya jioni kwa ajili ya kuanza Mwezi Maalum wa Kimisionari 2019 Tarehe 1 Oktomba yamefanyika maadhimisho ya masifu ya jioni kwa ajili ya kuanza Mwezi Maalum wa Kimisionari 2019 

Papa Francisko:Tuishi imani hai kwa furaha ya kutangaza Injili na kushuhudia!

Katika masifu ya jioni,tarehe 1 Oktoba 2019 umefunguliwa Mwezi Maalum wa Kimisionari.Tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko anashauri Kanisa lisitafute sehemu zenye chemchemi inayolindwa,bali liwe chumvi na chachu ya ulimwengu.Tunatumwa kwenda kutoa talanta na kuthubutu katika maisha ambayo siyo mzigo,bali kuwa zawadi ya Kanisa linalotoka nje kama wamisionari ambao ni wafiadini wa kwanza kushuhudia imani.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 1 Oktoba ameongoza masifu ya jioni, wakati wa fursa ya kufungua Mwezi wa Maalum wa Kisimisionari unaoongozwa na mada ya,“ mmebatizwa na kutumwa: Kanisa la Kristo katika utume ulimwenguni, ambao aliutangaza wakati wa sala ya Malaika wa Bwana kunako tarehe 22 Oktoba 2017. Kwa maana hiyo tarehe 1 Oktoba ikiwa  ni siku ya kukumbuka Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu, mwalimu na Msimamizi wa misionari, Baba Mtakatifu amesisitiza juu ya kuwa na  shauku na ubunifu ili kuweza kuzaa matunda na talanta ambazo Mungu amempatia kila mmoja wetu, mali ambazo zisiachwe katika  kasha la fedha, kwa sababu ni moja ya wito.

Baba Mtakatifu Francisko, akianza kufafanua juu ya neno la Injili lililosomwa, anasema Bwana anawajiwakilisha kama mtu ambaye kabla ya kuondoka anaita watumishi na kuwakabidhi mali zake ( rej Mt 25,14).  Kwa maana hiyo ni Mungu anatukabidhi mali kubwa zaidi, ambazo ni maisha yetu na ya  wengine, zawadi nyingi  anazo tukabidhi ni tofauti na  mwingine. Mali hizi na talanta hizi hatupewi kwa ajili ya kuzitunza katika katika kasha la fedha, bali hizo zinawakilisha wito. Bwana anatuita ili talanta ziweze kuzaa matunda kwa shauku na ubunifu. Mungu atatuuliza ni sehemu ipi tuliziweka, katika kuthubutu na labda hata kuaribika sura. Mwezi wa Maalum wa Kimisionari utaka kututikisa ili tugeuke kuwa wabunifu wa mema. Sisi mawakili wa imani na walinzi wa neema, bali wamisionari.

Baba Mtakatifu Francisko anasema kuwa, unageuka kuwa shuhuda ukiwa unashuhudia na maisha hasa ya kumjua Yesu. Ni maisha ambayo yanazungumzwa. Kushuhudia ni ufunguo wa neno, ni neno lenye mzizi kwa maana ya ushahidi. Wamisionari wanatambua kuwa imani siyo propaganda na au itikadi za mawazo,  bali ni heshima ya zawadi ya maisha. Wanaishi kwa kueneza amani na furaha, kupenda wote, hata masikini kwa ajili ya upendo wa Yesu. Na hivyo sisi ambao tumegundua kuwa wana wa baba Mwenyezi, tunawezaje  kunyamazisha furaha ya kuwa wapendwa na  uhakika kwa kuwa  daima sisi ni tunu machoni pa Mungu? Ni hari njema ambayo watu wengi wanasubiri, pia  ni wajibu wetu. Baba Mtakatifu Francisko anasisitizia kujiuliza katika  mwezi huu ya kwamba,  “je ushuhuda wangu huko namna gani?”

Mwisho wa Somo la Injili Bwana anasema “mwema na mwaminifu, mbaya na mvivu. Je ni kwa nini Mungu anakuwa mgumu dhidi ya mtumishi huyo aliyeogopa? Je ni ubaya gani aliufanya? Ubaya wake ulikuwa ni wa kutofanya yaliyo mema, anayo dhambi ya kutotimiza wajibu, Baba Mtakatifu anajibu. Mtakatifu Alberto Hurtado anathibitisha kwamba: “ni vema kutotenda mabaya. Lakini ni vibaya kutotenda wema” na unakuwa na kile ambacho unatoa. Kwa maana hiyo baba Mtakatifu anongeza kusema: “Na siri ya kuwa na maisha ni kuyatoa. Kuishi kwa kutotimiza wajibu ni kusaliti wito wetu; Kutotimiza wajibu ni kinyume  na utume”.

Tunatenda dhambi ya kutotimiza wajibu yaani dhidi ya utume tunaposhindwa kueneza furaha, kujifunga binafsi na huzuni, kwa kufikiri kuwa hakuna akupendaye na kukuelewa. Tuna dhambi dhidi ya kutotimiza wajibu tunapo angukia katika kujiachie, mfano  kusema kuwa“ siwezi kufanya lolote na sina uwezo”. Je ni kwa jinsi gani? Baba Mtakatifu anauliza,  wakati  Mungu amekupatia talanta na wewe unajiaminisha kuwa masikini wa kutoweza kutajirisha yeyote? Tunatenda dhambi ya kutotimiza wajibu vile kwa malalamishi, kuendelea kusema kuwa kila kitu kinakwenda vibaya, katika dunia na katika Kanisa. Tunatenda dhambi dhidi ya utume tunapokuwa watumwa wa hofu ambayo inagandisha kila kitu na  kutuacha na tabia ya kusema “ tumezoea  daima kufanya hivyo””. Tunatenda dhambi dhidi ya utume, tunapoishi maisha kama vile ni mzigo na siyo kama zawadi; ikiwa tunajiweka katikati na ugumu wetu badala ya  ndugu kaka na dada wanaosuibri kupendwa.

Mungu humpenda yule mwenye kutoa kwa furaha (2 Kor 9,7). Lakini lazima kuwa makini, kwa sababu Baba Mtakatifu amesema, kama siyo kutoka  nje, siyo Kanisa. Kanisa ni kwa ajili ya kwenda njiani; Kanisa linatembea. Kanisa ni lile linakkwenda barabarani, ni ka kimisonari; ni Kanisa lisilopoteza muda katika  kulilia mambo ambayo hayaendi, waamini ambao hawana tena thamani kulilia mambo ya kizamani ambayo hayapo tena. Ni Kanisa ambalo halitafuti chemchemi ya kulindwa ili kukaa kwa utulivu; ni Kanisa linalotamani kuwa chumvi na chachu ya dunia tu. Kanisa hili linajua kuwa hii nguvu yake sawa na Yes una  siyo umuhimu tu wa kijamii au wa kitaasisi, lakini ni  upendo mnyenyekevu na wa bure.

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na tafakari yake amesema, leo hii tunaanza mwezi Oktoba mwezi wa kimisionari unaosindikizwa na sura za watumishi watatu na ambao walizaa matunda mengi. Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu anatuonesha njia  katika kuombea matendo ya kimisionari duniani. Huu pia ni mwezi wa Rosari! Swali, Je tunasali vipi kwa ajili ya uenezaji wa Injili,  kwa ajili ya uongofu wa kutotimiza wajibu wa kitume? Aidha  sura nyingine ni Mtakatifu Francisko Xsaveri, mmoja wa wamisionari wakubwa wa Kanisa. Hata yeye anatuhimiza kuondoka ndani ya nyumba zetu kama zile za konokono; Je tunao uwezo wa kuacha yote mazuri kwa ajili ya Injili? Pia yupo Mtumishi wa Mungu Pauline Jaricot, mfanyakazi aliyesaidia utume wa kimisionari kwa kazi yake ya  kila siku na ambaye alitoa  fedha ya mshahara wake. Na hii ilikuwa ni katika kipindi cha mwanzo wa Matendo ya Kipapa ya Kimisionari. Je sisi kila siku tunaifanya zawadi yetu iweze kushinda nyufa zilizopo kati ya Injili na maisha? Kwa maana hiyo  Baba Mtakatifu Francisko amehimiza kwamba “Tafadhali usiishi imani kama ya kisakrestia”.

Kufuatia na mifano hiyo ya watu watatu, Baba Mtakatifu Francisko amesema “Wanatusindikiza mtawa mmoja, padre mmoja na mlei. Hawa ni kutaka kuelekeza kuwa  hakuna yoyote anayebaguliwa katika Kanisa” . Ndiyo katika mwezi huu, Bwana anakuita hata wewe. Anakuta wewe, baba na mama wa familia; wewe kijana anayeota ndoto ya mambo makubwa; wewe unaye fanya kazi katika kiwanda, katika duka, katika benki, katika hoteli; wewe usiye na ajira; wewe uliyeko kitandani hospitalini…. Bwana anakuomba uwe zawadi mahali ulipo, hivyo kwa jinsi ulivyo na yule uliye naye karibu, usifiche maisha bali kuyatoa; usilie, bali ujiachie ili kutuliza machozi ya  anayeteseka zaidi. Kuwa na ujasiri, Bwana anakusubiri sana wewe. Ndiyo anakusubiri hata kwa mmoja kuwa na ujasiri wa kusafiri kwenda mahali ambapo hakuna matumaini na hadhi, mahali ambapo watu wengi wanaishi bila kuwa na furaha ya Injili.

Swali: Je ninapaswa kwenda peke yangu? Hapana, hii sio sawa. Ikiwa tunakusudia kufanya utume na mashirika ya biashara na mipango ya kazi, haiendi. Mhusika mkuu wa utume ni Roho Mtakatifu. Yeye ndiye mhusika mkuu wa utume wa kimisionari. Wewe nenda na Roho Mtakatifu. Nenda, Bwana hatakuacha peke yako; ukishuhudia, utagundua kuwa Roho Mtakatifu amefika  kabla yake  kukuandalia njia. Baba Mtakatifu amehitimisha akiwataka wawe na ujasiri kaka na dada na Mama Kanisa anapata uzao wao katika furaha ya utume wa kimisionari”.

02 October 2019, 09:32