Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu katika katekesi ya Jumatano 2 Oktoba 2019  amekazia namna ya kuinjilisha hasa kwa kusikiliza Roho Mtakatifu anayeongoza katika matendo ya utume Baba Mtakatifu katika katekesi ya Jumatano 2 Oktoba 2019 amekazia namna ya kuinjilisha hasa kwa kusikiliza Roho Mtakatifu anayeongoza katika matendo ya utume  (Vatican Media)

Papa Francisko:Roho Mtakatifu ni kiongozi wa uinjilishaji!

Katika katekesi ya Baba Mtakatifu Fracisko,iliyoongozwa na somo kutoka Matendo ya mitume amejikita kufafanua mkutano wa Filipo na mtauwa wa Ethiopia.Baba Mtakatifu anakazia umuhimu wa kutambua Neno la Mungu,na sakramenti kwa ajili ya maisha mapya kwa Mungu.Aidha amesema kwamba bila Roho Mtakatifu hakuna uinjilishaji.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Fracisko, tarehe 2 Oktoba 2019 wakati wa tafakari ya kateksi yake, kwenye  mwendelezo wa Somo kutoka Matendo ya mitume, amefafanua juu ya mateso ya Kanisa, kwa kuongozwa na Somo kutoka Mantendo ya Mitume mahali ambapo Filipo anaingia katika mji wa Samaria kuhubiri Kristo. Baba Mtakatifu amesema, Filipo alitemlemka akaingia mji wa Samaria, akawahubiria Kristo. Na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo, walisikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya. Kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao, wakilia kwa sauti kuu; na watu wengi waliopooza, na viwete, wakaponywa.  Ikawa furaha kubwa katika mji ule. (Mdo 8, 5-8).

 Baada ya kifodini cha Mtakatifu Stefano mbio za Neno la Mungu utafakiri zilianza kusimama kutokaana  na adha kuu kuu ya Kanisa la Yerusalemu na wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume. Baba Mtakatifu Francisko amesema, katika kitabu hca Mtendo ya Mitume, mateso yanaonekana kama tabia ya kudumu ya maisha wafuasi na kuthibitisha kile alichosema Yesu kwamba “Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; (Yh 15,20) Lakini mateso badala ya kuzima moto wa Injili, ndipo unaongeza zaidi. Katika somo, shemasi Filipo alianza kuhubiri katika mji wa Samaria na ishara nyingi zilionekana alizofanya kwa kuwasindikiza kwa njia ya kutagaza Neno la Mungu. Kwa maana hiyo Roho Mtakatifu anaanza  hatua moja ya safari ya Injili . Roho Mtakatifu anamsukuma Filipo kwenda kukutana na mgeni aliye na moyo wazi kwa Mungu.

Filipo anaamka na kwenda na shauku katika barabara ya jangwa na hatari; anakutana na mfanyakazi wa malkia wa Ethiopia , anayeratibu mali zake. Mtu huyo aliyekuwa mtauwa mara baada ya kukaa Yerusalemu kwa ibada zake alikuwa sasa anarudi katika  nchi yake. Alikuwa ni mcha mungu wa Kiyahudi kutoka Ethiopia. Akiwa ameketi katika gari, lake huku anasoma kitabu cha nabii Isaya, hasa wimbo wa nne wa “mtumishi wa Bwana”. Baada ya kuumuliza kama alikuwa anajua anacho kisoma, mtu huyo alijubu ni kwa jinsi gani anaweza kujua ikiwa hakuna anayemwelekeza? (Mdo 8,30-31). Mtu huyo mwenye kunguvu, anatambua ya kuwa anahitaji na kuongozwa ili kuweza kuelewa Neno la Mungu. Ilikuwa anafanya kazi benki, alikuwa ni waziri wa uchumi na alikuwa na kila kitu na  uwezo kifedha, lakini alitambua kwamba, bila ufafanuzi hasingeweza kujua, alikuwa ni mnyenyekevu, Baba Mtakatifu Francisko amethibitisha.

Majadiliano hayo kati ya Filippona mtaua wa Ethiopia unatufanya kutafakari hata juu ya kwamba, haituishi kusoma tu  Maandiko matakatifu, bali kuyaelea maana yake na kupata utamu wa kwenda zaidi ya hayo hasa roho ambayo inaongoza ulewa. Kama alivyosema Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikito XVI mwanzoni mwa Sinodi kuhusu Neno la Mungu  kwamba “ kutafakari na usomaji wa kweli wa andiko takatifu, sio tukio kama la kusoma barua (…) bali ni harakati ya uwepo wangu ( tafakari  6 Oktoba 2008). Kuingia kwa kinda ndani ya Neno la Mungu ni kuwa na utayari wa kuondokana na vikwazo binafsi ili ukutane na Mungu na kufanana na Kristo ambaye ni Neno hai la Baba.

Ni nani aliyekuwa mstari wa mbele, ambaye mtaua alikuwa anasoma na badaye akapata  mwanga kutoka kwa Filipo? Alikuwa ni mnyenyekevu,  mtumwa ambaye alisumbuka kwa upole na ambaye hakujibu uovu kwa uovu, haua kama alihesabiwa kushindwa na tasa, na  mwishowe akaondolewa, na akawaokoa watu kutoka katika dhambi za kutozaa matunda kwa ajili ya Mungu. Ndiye Kristo kweli ambaye Filipo na Kanisa lote wanatangaza! Na kwa njia ya Pasaka sisi sote tumekombolewa.

Hatimaye mtauwa wa Ethiopia anatambua Kristo na kuomba ubatizo  na kukiri imani katika Bwana Yesu. Baba Mtakatifu Francisko amesema kwamba hii ni simulizi nzuri , lakini aliyetoa msukumo kwa Filipo kwenda katika jangwa ili kukutana na mtu hiyo ni nani? Je ni nani aliyemsukuma Filipo kukaribia gari lake? Ni Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ndiye kiongozi wa Unjilishaji. Kwa kutoa mfano amesema iwapo unataka kwenda kuinjilisha, lazima kwenda na Roho Mtakatfiu, pasipo yeye hakuna unjilishaji. Hiy inawezekana kuonekana  katika itikadi fulani za umma… lakini uinjilishaji ni kumwacha Roho Mtakatifu atoe msukumo wa kutangaza, lakini kutangazwa kwa ushuhuda, hata kwa kufiadini na hata kwa neno .

Baada ya mtauwa wa Ethiopia kukutana na mfufuka, alikutana na Yesu Mfufuka na kuelewa ule unabii, lakini ndipo Filipo akatoweka na Roho akampeleka mahali pengine, na kumtuma afanya jambo jingine. Kiongozi wa kwanza wa Uinjilishaji ni Roho Mtakatifu, kwa maana hiyo ni ishara ipi  kama wewe mkristo katika kuinjilishaji unafanya?  Ni furaha hata kufiadini kwa maana Filipo akiwa amejazwa na furaha  ya kuwabatiza wanawake na wanaume alikwenda sehemu nyingine kuhubiri Injili, Baba Mtakatifu amsisitiza.  Hatimaye anasema Roho Mtakatifu atufanye sisi wabatizwa wote tunaotangza  Injili kwa ajili ya kuvutia wengine na si kwa ajili yetu  binafsi bali kwake Kristo na ambao tuweze kujua namna ya kutoa nafasi kwa ajili ya matendo ya Mungu, hata kujua kuwapa huru wengine na kuwajibika mbele ya Mungu.

02 October 2019, 12:30