Baba Mtakatifu anasema, wakati wengine wanakufa na njaa, mataifa mengine yanakusanya na kutupa mkate wa masikini Baba Mtakatifu anasema, wakati wengine wanakufa na njaa, mataifa mengine yanakusanya na kutupa mkate wa masikini 

Barua ya Baba Mtakatifu kwa Fao:tunakusanya na kupoteza mkate wa masikini!

Katika fursa ya siku ya chakula duniani Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake FAO akibanisha jinsi gani kuna ulazima wa kuwa rahisi na kuwa makini katika uhusiano wa mitindo ya maisha na ili iweze kuwa bora binafsi,kwa ndugu na mazingira.Hata hivyo amebainisha juu ya hathari za uzito kutokana na lishe mbaya hadi kufikia magonjwa na vifo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko, ametuma barua kwa Mkurugenzi Mkuu wa FAO katika Fursa ya siku ya chakula duniani tarehe 16 Oktoba 2019. Katika barua hiyo, Baba  Mtakatifu anasema Siku ya Vyakula dunia inatoa mwangwi kila mwaka wa kilio cha ndugu wengi wanao endelea kuteseka na janga la njaa na utapiamlo. Licha ya jitihada nyingi zilizotimizwa za nyakati za mwisho, Ajenda ya 2030 kwa ajili ya kufikia maendeleo endelevu, bado inabaki nyuma katika mpango wa kutimiza kwenye sehemu nyingi za dunia ili kujibu kilio cha kibinadamu. Hata hivyo kauli mbiu iliyopendekezwa mwaka huu na FAO ni “Matendo yetu ni wakati wetu endelevu”. Chakula bora kwa ajili ya ulimwengu wa “njaa zero”,  na ambyo Baba Mtakatfu anasema inakwenda kunyume na upotoshaji wa mchanganyiko wa lishe ya chakula. Hii ni kutokana na kwamba, “tunaona ni kwa jinsi gani badala ya chakula kuwa zana ya kuishi  na kumbe ndiyo unakuwa  mkondo wa uharibifu binafsi.  Kwa maana hiyo mbele ya milioni 820 ya watu wenye njaa  katika sahani ya mzani, wapo pia  karibia milioni 700 ya watu wenye uzito zaidi,  na ambao ni waathirika wa kula vibaya chakula. Hawa siyo mfano tu wa lishe ya watu wenye kupendeza (PAOLO VI, Waraka wa Populorum progressio, 3), bali hata tabia hii  inaanza kuwepo hata katika nchi za kimasikini maahali ambapo tabia hizi zinaasha kuonekana katika nchi zenye kipato cha chini na  wanaendelea kula kidogo na vibaya, huku wakiiga mifumo ya kula kama ya maeneo yaliyoendelea.

Magonjwa yatokanayo na kula vibaya

Kwa sababu ya utapiamlo, magonjwa yanayohusiana na kula sana yanaweza kuleta matokeo mara nyingi ya ugonjwa wa kisukari, magonjwa ya mishipa na mitindo mingine ya magonjwa yatokanayo na kula vibaya. Vile vile Baba Mtakatifu pia amekumbuka idadi inayozidi kuongezeka ya vifo kutokana na kile kinachoitwa  "anorexia na bulimia" yaani tabia ya watoto hasa wasichana  kukataa kula chakula kwa kuogopa kunenepa. Baba Mtakatifu Francisko anasema ni lazima kuwapo uongofu wa namna ya matendo na lishe ni muhimu na nafasi ya kuanzia. Tunaishi kwa neema ya matunda kazi  ya uumbaji (rej Zab 65,10-14; 104,27-28) na hivyo mambo haya hayawezi kupunguzwa na kuwa matumizi  binafsi. Kwa maana hiyo usumbufu wa vyakula unaweza kupambaniwa tu,  ikiwa ni kuhamasisha mitindo ya maisha ya kuwa na  maono ya kwamba kila kitu tumepewa  na lazima kutafuta utulivu, kiasi, kujizuia, kujidhibiti na mshikamano. Mambo haya ni fadhilia ambazo zinasikindikiza historia ya binadamu.  Kwa namna hiyo tunaweza kujihimarisha juu ya mahusiano ya kidugu ambayo yanatazama ustawi wa pamoja na kuzuia ubinafsi ambao unazaa njaa tu na kuleta ukosefu wa usawa kijamii. Mtindo wa maisha ambao unatuwezesha kukuza uhusiano mwema kati yetu na ndugu na mazingira ambamo tunaishi.

FAO ina nafasi msingi katika maisha ya familia

Ili kuweza kufafana na mtindo wa maisha familia ina nafasi msingi na katika FAO ambayo inajikita kwa namna ya pekee kwenye umakini wa kutetea familia  vijijini na kuhamasisha kilimo cha kifamilia. Katika muktadha wa familia, shukrani kwa umakini wa kike na wamama ambao tunajifunza kuheshimu wema binafsi na pamoja. Kwa upande mwingine, matendo yaliyochukuliwa kati ya mataifa yanaweza kusaidia kuweka pembeni maslahi binafsi kwa namna ya pekee na kukuza imani na uhusiano wa urafiki kati ya watu (Mafundisho ya kijamii ya Kanisa Katoliki 482).Ni matarajio ya Baba Mtakatifu Francsiko kwamba, mwaka huu usadie ili wasisahau kwamba wapo wanaolishwa kidogo sana. Na ni jambo la kusikitisha sana leo hii kuona chakula kipo na kinaweza kutosha wote au bado kuna kanda nyigni duniani ambazo chakula kinaharibiwa, kinatupwa au kutumiwa kwa malengo mengine ambayo hayaendeni na matumizi ya chakula yanavyotakiwa. Ili kuhepukana na suala hili ni lazima kuhamasisha taasisi za kiuchumi na mipango  kijamii ambayo inaruhusu umasikini zaidi waweze kuota chakula kwa namna ya kawaida na  rasilimali msingi ( Wosia Laudato si’, 109).

Mapambano dhidi ya njaa na utapiamlo 

Mapigano dhidi ya njaa na utapiamlo hayatakoma hadi  mantiki ya soko ya pamoja itapoibuka na kutafuta faida tu kwa gharama zote kwa ajli ya wote na  kupunguza chakula kuwa bidhaa ya kibiashara tu, kwa kuzingatia uvumi wa kifedha na kupotosha utamaduni wake, kijamii na kwa nguvu mfano. Wasiwasi wa kwamba Baba Mtakatifu Francisko anaandika ni  lazima na daima uwe wa mwandamu hasa wale ambao wanakosa chakula kila siku na wengine wanapata kidogo kwa ajili ya uhusiano wa kifamilia na kijamii ( Laudato si 112-113).  Iwapo binadamu atawekwa siku moja katika nafasi iliyo yake, ndipo operesheni ya msaada wa kibinadamu na mipango ya maendeleo itakuwa imefanya kazi kubwa na kutoa matokea yanayotarajiwa. Siyo rahisi kusahau kile ambacho tunakusanya kwa wingi na tunatupa mkate wa masikini. Baba Mtakatifu Francisko anahitimisha Bara yake kwa Mkurugenzi wa Mkuu kwamba, hayo ni baadhi ya takafakari ambazo amependa kushirikisha na yeye katika fursa ya Siku hiyo,na wakati huo akiomba Mungu baraka kwa kila mmoja na ili iweze kuleta matunda ya kazi yake kwa namna ya kwamba iendelee kukuza amani katika huduma ya mandeleo ya dhati na fungamani kwa familia ya kibinadamu!

16 October 2019, 11:16